Napenda nifafanue masuala kadhaa hapa.

Moja, sisi kama Kambi ya Upinzani inayoundwa na CHADEMA tulikwishaamua kwamba posho za vikao sio stahili sahihi kwa Mbunge. Mnadhimu Mkuu wa Kambi alikwishaandika kwa Spika wa Bunge kutaka kutenganisha fomu za mahudhurio na fomu za posho. Mbunge wenje pia katika moja ya michango yake alisema Bunge litengenishe fomu hizi mbili.

Kuhusiana na mimi kama an indivual MP, nilipewa kazi na chama kama Waziri kivuli Fedha na tangazo la posho alilitoa Naibu wangu ndugu christina Lissu. Mie nikalitolea ufafanuzi kwa vyombo vya habari. Wabunge wa CCM wakaanza kunishambulia na kusema ni unafiki kwamba ninatangaza posho zifutwe ilhali nazichukua. Nikamwandikia Spika barua kuwa posho zangu ziende kwenye charity org jimboni kwangu. Hili nalo likaonekana kama ni unafiki pia. Nikaamua kuzikataa kabisa. Hivyo toka tarehe 8 Juni mimi sipokei posho ya vikao. Njia ninayotumia ni kutosaini mahudhurio Bungeni ili wasipate sababu ya kunilipa.

Sasa kuna mchangiaji hapa kasema usiposaini ndani ya siku tatu unaadhibiwa. Kanuni inasema Mbunge asipohudhuria MIKUTANO mitatu ya Bunge anakuwa amejifukuza ubunge. Tutofautishe mikutano na VIKAO. Kikao ni kila siku na mkutano ni session nzima, mfano session iliyopita ilikuwa ni mkutano wa 4 wa Bunge nk.

Sasa, ikitokea sitasaini pia katika mkutano wa 5 na wa 6 wanaweza kuanza mchakato wa kunifukuza Ubunge. Lakini je mchakato huo utategemea karatasi za mahudhurio tu? Kwa mfano, nikiwa Bungeni ninauliza swali au kuchangia hoja, hansard inarekodi kuwa nilikuwepo Bungeni. Karatasi ya mahudhurio inaonyesha sikuwepo Bungeni. Audio na video records zinaonyesha nilikuwepo Bungeni, watanifukuza kwa vigezo vipi?

Katika harakati lazima ni lazima kuchallenge rules ili zibadilike. Nadhani katika hili tutafanikiwa.

Hivyo, wabunge wa chadema sio wanafiki kwani tayari wameandika rasmi kutaka fomu tofauti za kujaza mahudhurio. Pili, Zitto hasaini kama njia ya kutoa changamoto kwa rules. Lakini pia ninaamini kwa dhati kabisa kwamba posho ya kikao (sitting allowance) sio stahili halali (legitimate?)Kwa mbunge anayelipwa mshahara kwa kazi ile ya kukaa na kutunga sheria, kuisimamia serikali na kuwakilisha wananchi.