Barua: Zitto akataa posho za vikao

Barua: Zitto akataa posho za vikao

...............Acha uhuni mkuu,nimejaribu kufuatilia hayo majibu ya Zitto siyaoni...acha kudanganya umma mkuu....crap!!

Hayo ya umaarufu wa kisiasa mimi sijui chochote , ila kuwa shangingi limerejeshwa ndio na kwa wiki mbili za mwisho wa Bunge alikuwa analitumia John Joel ambaye alikuwa ni kaimu katibu wa Bunge na dereva alikuwa ni yule yule wa Mbowe ndio alikuwa anamwendesha huyo kaimu katibu wa Bunge.

Nafikiri kuliachia ulikuwa ni uamuzi wa Kambi kwani walikaa kama kambi na kukubaliana kuwa alikabidhi na ndio maana siku ya kulirejesha walikuwa wabunge wote hivyo ni kitu walichokuwa wanakijua na ilikuwa ni majira ya saa mbili usiku , mengine baadae .

Hapo sawa. Sasa hizo posho imekuwaje? Kama walikubaliana ilikuwaje ZZK peke yake ndio atekeleze uamuzi wao lakini akina Mnyika, Regia, Mwalimu wangu Kaihula, nk. wamekumbatia hizo posho. Bado mimi nawaona wanafiki tu hao.

Mangi, Zitto ha-sign mahudhurio na mwanzoni kulikuwa na malumbano kidogo kati ya ofisi ya spika na zitto maana kanuni zinasema kama mbunge hatohudhuria vikao vitatu mfululizo bila idhini ya Spika basi aweza kupewa adhabu ikiwa ni pamoja na kufukuzwa. Shida imekuwa kwenye tafsiri ya neno 'vikao', je vikao kwa maana ya jumatatu, jumanne n.k? au vikao kwa maana ya msimu e.g kikao jun, jan or nov? Hapa ndio issu huku watu wakivuta pumzi.

Na hapa ndio nasema inawekezekana kabisa kama wabunge wote kwa ujumla wao hawaku-sign mahudhurio kwa kanuni za sasa kukawa na madhara, hasa ukizangatia CHADEMA ndio wanaunda kami rasmi ya ubunge na Mbowe ndio kiongozi wa kambi ya upinzani buneni. Hata hivyo mara kadhaa wamekuwa wanasisitiza kuwepo kwa vitabu viwili vya mahudhurio kimoja kwa wale wanaokubaliana na posho na kingine kwa wale wanaokataa posho. Ofcourse hii imekataliwa. Kwa ujumla hii issue bado kuna vizingiti wanatakiwa wavuke.

John Mnyika ni msomaji mzuri hapa jamvini, ningependa niamini atatolea ufafanuzi zaidi na complications zilizopo kwa sasa.

Nilisema tokea zamani, ifikapo kwenye pesa wote ubadilika! Kama wote wamezichukua na kuzitia mifukoni mwao wana tofauti gani na Shibuda aliyetaka posho zipandishwe mpaka 500,000/=?!!!!!

Ningeelewa kidogo, endapo watasema ziliingizwa kwenye akaunti zao na zimekusanywa hivyo zitatumika kuwasaidia watanzania maskini badala ya kuzila na kusingizia "Eti si unajua ukishasaini karatasi ya maudhuria basi posho zinapalekwa kwenye akaunti yako"!

Kama wamezichukua na kuzitumia kama pesa zao nyingine basi ni WANAFIKI period

Zitto pamoja na kuwa controvertial figure, lakini vilevile ni steadfast kwenye kile anachokisimamia.

Zitto kwenye hili la posho ameonesha ukomavu wa juu kabisa kisiasa kwa ku WALK THE TALK.

Haijalishi kama ni mkakati wake wa kufikia malengo ya uongozi wa juu au vipi, sababu kila mwanasiasa
ultimately angependa afike kwenye highest position possible. Sema wengine wana limitations za uwezo.

Kwa hili nasema tena BIG UP Zitto, wasiokukubali waache maana hawaijui siasa, wakikua watakukubali.

Kimsingi tunachohitaji kwenye taifa letu changa ni katiba mpya itakayojenga STRONG INSTITUTIONS.

Hii habari za vyama, sikuwahi kuamini kuna chama cha wanamageuzi wa kweli, wanaokua willing kushiriki
uchaguzi kwenye katiba hii hii miaka nenda miaka rudi. Maana yake ni kuwa wako tayari na wao kutawala
kwa katiba hii hii na kuleta usiri uleule kwenye mambo nyeti, na unyonyaji uliotukwamisha miaka yote.

Na habari hii imezidi kucement what i already knew about our politicians, wengi ni wachumia matumbo tu.

Tofauti ni kuwa wengine wameona CCM kumebana "kuna wenyewe", nawao wakaamua waanzishe chama mbadala
na huko nako utasikia "kuna wenyewe"...kama anavyoshambuliwa Shibuda na wakati wote wamelamba posho!!!

Hapo nilipo highlight ndio kunanifanya nishindwe kuelewa unafikiria na kuya tathimini mambo kwa kutumia nini? Hebu niambia huyu wa chama tawala na mkuu wetu alivyo fikia hiyo goli yake. sasa hivi yeye mwenyewe, washirika wake kwenye kufikia hiyo ultimate gol na hata chama chake wana suffer consiquence gani? Kwa mikakati inayofanana na hii ya zitto. Acha kabisa kutetea upuuzi huu.

Acheni kisingizio cha kutenganisha fomu kuwa kigezo cha kuendelea kupokea hizo posho.

Kwani akiisha saini mahudhurio ni lazima achukue pesa yote? Si achukue ile anayoona ni halali yake na kuacha ile anayoiona ni haramu???

CDM ni Unafiki mtupu!

....Kwani akiisha saini mahudhurio ni lazima achukue pesa yote? Si achukue ile anayoona ni halali yake na kuacha ile anayoiona ni haramu???...

Mkuu usichangie kinafiki kama mbumbumbu asiyejua kitu!
Wabunge hawachukui posho au mishahara dirishani, zinaingizwa kwenye account zao moja kwa moja.
Unawezaje kutenganisha hela kwenye account moja!? Acha kutumia masaburi!

Nitauafiki msimamo wa ZITTO endapo tuu atajua wapi fedha yake itaenda tujue hii nchi ya kifisadi kususia fedha kutafanya mafisadi watanue nadhani kwasasa wachukue fedha ili ziwasaidie katika kukuza CDM kichujue dola and thereafter ndio wafute chini ya usimamizi wa CDM chama makini. HUKUNA MAANA KUSUSIA MIFUPA KWA FISI.

Nitauafiki msimamo wa ZITTO endapo tuu atajua wapi fedha yake itaenda tujue hii nchi ya kifisadi kususia fedha kutafanya mafisadi watanue nadhani kwasasa wachukue fedha ili ziwasaidie katika kukuza CDM kichujue dola and thereafter ndio wafute chini ya usimamizi wa CDM chama makini. HUKUNA MAANA KUSUSIA MIFUPA KWA FISI.
Naunga mkono! maana hoja ya msingi haikuwa kususia posho bali zifutwe ili kupata pesa za kisaidia nchi katka vipaumbele muhimu vya kijamii. maadam hilo lilikataliwa na magamba, hakuna sababu ya kuziacha kwa sababu mnamuachia nani wakati mlikotaka ziende magamba wamekataa zisiende?

waache wachukue kwani ni haki yao kikatiba kama inavyonukuliwa ibara ya 73 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977
. 73'' Wabunge wote wa aina zote watashika madaraka yao kwamujibu wa Katiba hii, na watalipwa mshahara, posho na malipo
mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge''.

na kumbuka mbunge wa chadema mh. shibuda alisema ''hii sio posho bali ni ujira wa mwiha! posho wanapewa manamba bwana!''

Katika mpango wa miaka 15 uliozinduliwa na Kikwete pale Dodoma, moija ya mpango ni kuzipitia upya posho zote na kuziondoa au kuzipunguza inapobidi. Nawashangaa magwanda kuidakia hiyo hoja na kuipiga zumari kama vile ni hoja yao. Hii ni plagiarism at its best. Mnawazuga majuha wenzenu, wengine saa sita kamili.

Chuchu?

Butola, huwezi kusema eti Mbowe ameshindwa kuachia posho ya shilingi 70,000 kwa siku ambayo kwa siku 50 za ubunge ni sawa na shilingi milioni tatu na nusu 3,500,000 kwa kipindi chote cha bunge la bajeti halafu ujenge hoja hapa.

Pamoja na kumpa pongezi Zitto , ila Mbowe anapaswa kupewa pongezi pia kwani alipinga mashsngingi na kuamua kuliacha bila masharti na nafikiri kuna haja kuliangalia hili pande zote.

Si unajua ata Rostam anaingia zaidi ya Billion 60 kwa mwezi lakini bado anaendelea kupiga deal za kifisadi? kiasi cha fedha anachochukua sio issue hapa bali suala la muhimu ni je anaweza kutembea kwenye maneno yake au anapiga domo tu??

...Mbowe amechemsha big time, ebu tuwe wakweli, Mbowe aliongea haya kuhusu posho.....

Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema wabunge wamekuwa wakilipwa mishahara kwa mwezi pamoja na fedha za kujikimu (per diem) wanapokuwa nje ya majimbo yao kikazi na kwamba wanachopinga ni "posho za vikao" (sitting allowance) ambazo ni kikwazo cha utekelezaji wa kazi za Serikali na majukumu mengine katika ofisi za umma.

"Kwa mfano, mimi ni mjumbe wa Kamati ya Uongozi (ya Bunge), nasaini 'sitting allowance' katika kikao cha Bunge, nikiitwa katika kikao cha kamati ya uongozi nasaini tena sitting allowance na hata kama kutakuwa na kikao kingine jioni naweza kulipwa, sasa kama huo siyo wizi ni nini?"

"Huu ni wizi wa fedha za umma"

Sasa mtu anayeongea maneno kama haya na kisha akaendelea kussign kimyakimya kuendelea kuchukua hizo posho kama usipomwita mnafiki utamwita vipi?hivi kesho utamwamini vipi mtu kama huyu kama mengine anayoyaongea ni mambo anayoyaishi au ni just politics za kiswahili?umakini upo wapi? huu ni ukosefu wa umakini uliovuka mipaka, kumpongeza hapa utakuwa ni unafiki mwingine...

Ebu tuache kuita chongo-kengeza na tuwe wakweli, MBOWE NA WABUNGE WENZAKE WANAOENDELEA KUCHUKUA POSHO NI WANAFIKI, utamwambiaje Magale Shibuda kuwa amekiuka msimamo wa Chama kuhusu posho kama Mwenyekiti na Kiongozi wa Upinzani Bunge anayepaswa kuongoza kikao cha kumchukulia hatua za kinidhamu anapokea hiyo posho?huu ni unafiki na ukosefu wa maono ya kiuongozi...

Safi sana Mhe. Zitto kwani huo ni mwanzo na wengine watafuata Nakitakia kila kheri kwenye shughuli zako. Fedha kwenda kwenye NGO yake ni sawa kwa sababu haina sehemu nyingine ambako iytatumika kusaidia Jamii tena amefanya vizuri imekwenda jimboni kwake. Au mlitaka aipeleke WAMA au EOTF?

Habari ni ya kweli imeandikwa katika gazeti la mwanainchi 29/8/2011 kichwa cha habari JUSSA ANG'ARA MBELE YA MARANDO, NAPE. soma habari hiyo hadi mwisho.

zitto kukataa kuchukua posho ni kuvunja katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 73 ambayo inasema:

73 ''Wabunge wote wa aina zote watashika madaraka yao kwamujibu wa Katiba hii, na watalipwa mshahara, posho na malipo​
mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge''

lakini pia kumbuka maneno ya hekima ya mh. shibuda ''huu ni ujira wa mwiha'', hivyo ruksa kudakua

Back
Top Bottom