Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,022
- 9,285
Wananchi wa Dar es salaam tumechoka na migao ya maji
Ndugu Waziri na Ndugu Mkurugenzi wa DAWASA
Mimi ni mkazi wa Dar es salaam, maeneo ya Mlalakuwa.
Napenda nikutaarifu kuwa, sasa katika maeneo yetu na mengine ya Jiji la Dar es salaam kumekuwepo na hali mbaya sana ya upatikanaji wa maji ya bomba. Hali hii imekuwa ni kero kubwa sana kwetu wananchi hasa ukizingatia hili suala limeanza kuwa kama "norm" au kawaida hivi wakati halikubaliki hata kidogo.
Maji yamekuwa yakija kwa vipindi vifupivifupi na wakati mwingine yasiwepo kabisa.
Ndugu Waziri na Mkurugenzi wa DAWASA
Haiwezekani haya mambo yanatokea, huku wizara ikiwa kimya na DAWASA nao wakiwa kimya bila kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu nini kimejiri na ni lini hili suala litaisha. Wananchi hatukubaliani kabisa na aina hii ya kuendesha mambo.
Ukosekanaji wa maji unatuathiri sana kiafya na hata kiuchumi kwa sababu tunakosa maji safi ya kunywa, Tunashindwa kuoga ipasavyo, tunashindwa kufua ipasavyo lakini kibaya zaidi ukosefu huu wa maji unatufanya tutumie pesa nyingi kununua maji ya madumu ambayo hatujui yanapatikana wapi na usalama wake ni upi!.
Ndugu Waziri wa Maji na Mkurugenzi wa DAWASA
Wananchi wa Dar es salaam tunataka maji, tena ya uhakika, hatutaki Ukimya au kauli za kisiasa.
Haiwezekani Taifa linalofikiria kuweka Bima ya Afya kwa wote halafu maji katika jiji kubwa kama Dar bado ni ya kuungaunga.

Kama mkishindwa kuleta maji tutawasagia kungunu kwelikweli mbele ya mheshimiwa rais maana haiwezekani miezi yote hii Dar es salaam maji yanakuwa ya manati na nyie mpo, hamseni chochote, ni kama kwamba mmeridhika hivi na status quo wakati sisi wananchi tunaumia. Hili halikubaliki.
Mheshimiwa Waziri na Mkurugenzi wa DAWASA
Wakati sisi tukiumia kwa kukosa maji lakini DAWASA bado inaleta bili za kila mwezi za matumizi ya maji na bili zenyewe kwa kiasi kikubwa huoni zikiwa ndogo kwa sababu ya ukosefu wa maji katika miezi husika. Sasa tunajiuliza, inamaana hata bomba lisipotoa maji bili iko palepale?, Haya ni maajabu ya DAWASA.
Ndugu Waziri,
Wananchi tunataka maji tena tunayataka Sasa
CC:
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
CC
Wabunge wote wa Mkoa wa Dar es salaam