Barua ya Wazi kwa Mkuu wa Mkoa Amos Makala juu ya Panya Road na namna ya kuwatokomezaa pasipo kujirudia

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,272
9,716
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwanza nikupe Hongera ya kuendelea kuaminiwa kuendelea kuwa RC wa DSM, Ni heshima kubwa kwako kwa kuwa Mkuu wa mkoa wa jiji la kwanza kiuchumi na kibiashara, kiuwekezaji na hata mchango wake katika Pato la Taifa,

Ni mkoa ambao ndio Tanzania yenyewe ambapo hata sisi wa mikoani ukitoka dar unahis umetoka Washington au New york marekani au Paris ufaransa au London uingereza, Ni mkoa ambao viongozi wote wa kitaifa wa serikali au hata wale wa vyombo vya ulinzi na usalama wapo hapo, Ni mkoa ambao Balozi zote au Taasisi zote za kimataifa zipo hapo, ni lango la kibiashara kwa nchi za Sadc, Ni mkoa wenye kila kitu, Lakini Ni mkoa ambao Rais wa nchi na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama anaishi hapo pamoja na wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama, Kiufupi ndio Tanzania yenyewe hapo

Mkuu wa Mkoa nimeyaeleza hayo ili ujuwe unaongoza mkoa wa namna gani na hadhi yako ipoje ukilinganisha na mikoa mingine, Dar ndio Taswira ya nchi yetu na hata ukitaka kuharibu uchumi wa nchi Basi wewe haribu DSM, ukitaka Tanzania ichafuke Basi wewe ichafue DSM,

Mh mkuu wa mkoa hivi karibuni kumejitokeza suala la vitoto vinavyojiita Panya Road vikitesa kuumiza kupiga kujeruhi na hata kuuwa watu wa maeneo tofauti tofauti ya DSM, japo ni vitoto lakini madhara yake yamekuwa makubwa na kuleta hofu kwa wananchi, Nataka nisema kwako kuwa Jambo Hilo limeleta hofu na wasiwasi kwa wakazi wako hapo DSM

Ushauri wangu kwako ni kuwa kuanzia ngazi ya mitaa kuundwe vikundi vya kisiri vya sungusungu vitakavyofahamika kwa Mwenyekiti na wajumbe wake pekee, uchaguzi wa vijana hao uwe pia wa Siri baada ya kuwatathimini tabia na mienendo yao ili isije tokea wahalifu wanakuwa sehemu ya vikundi hivyo na kupelekea kuvuja kwa Siri na mikakati ya vikundi vya sungusungu,

Pili mh mkuu wa mkoa hakikisha kuwa Doria za jeshi la polisi zinaongezeka na kuwepo muda wote na vitendea kazi vinakuwepo muda wote hasa magari ili kuweza kufika kwa haraka maeneo ya matukio yanapokuwa yameripotiwa na wananchi au viongozi wa serikali za mitaa, Polisi wafike kwa wakati na kwa mikakati na mbinu sitahiki ili ikiwezekana hao vibaka wasipate nafasi ya kutoka eneo la tukio pasipo kukamatwa

Tatu wananchi waelimishwe juu ya kushirikiana katika kujilinda na kupambana na hao vibaka pale wanapokuwa wamebaini nyumba fulani imevamiwa, Hilo sis wananchi wa mikoani mbona tumeliweza? Sisi huku hatuwakimbii vibaka Ila vibaka ndio wanawakimbia wananchi kuogopa kutiwa mikononi maana wanajuwa hakuna huruma kwa wahalifu

Nne mh mkuu wa mkoa pia naunga mkono kauli yako, Nasema hivi hao vibaka ni lazima waonyeshwe kwa matendo kuwa gharama ya matendo yao Ni kubwa Sana, lazima wajuwe Ni hatari na nijambo lisilowezekana kumwaga damu ya mtu asiye na hatia kwa tamaa ya kupora Mali, lazima wajuwe nafasi yao ya kuwa salama Ni ndogo Sana au haipo wakibainika na kukamatwa kwa ushahidi wakifanya vitendo hivyo vya kinyama, lazima waonyeshwe njia ya kupita kwa watu wa aina yao, lazima waonyeshwe na kufundishwa kuwa hawawezi wakabaki na mapanga mikononi wakati serikali IPO ni lazima wapokonywe silaha zao na vitu vyao walivyoshika mikononi mwao kujeruhia na kuulia watu wasio na Hatia

Wakazi wa DSM wamechoka kuteswa,kuishi kwa hofu, kudhalilishwa, kujeruhiwa, kuuwawa, kuporwa vitu vyao,kuvunjiwa mirango na kufanya waishi Kama wapo uhamishoni, wanataka Hatua zichukuliwe, wanataka amani itawale, wanataka kuona vitendo hivyo havijirudii kila mara, wanataka kuona adabu inatawala, wanataka kuona matendo na siyo maneno, wanataka kuona jiji linapitika muda wote na maeneo yote yanafikika kwa amani, wanataka utulivu wa jiji ili watulie kwa amani warejeapo toka makazini kwao, wanataka wasisikie milango ikigongwa kwa mawe na mateke, wanataka Amani kwa kuwa no Haki yao kulindwa na serikali yao

Mk mkuu wa mkoa matumaini ya wanadaresalaamu yapo kwako, wote wanakutazama wewe, wote wanakusikiliza wewe, wote wanafuatilia kauli zako, wote wanataka uchukue hatua, Ni wakati wako kuingia kazini kwa nguvu kuwakabili hao vibaka kimya kimya maana umeshazungumza tayari, ingia kazini maana vyombo vyote unavyo, Rasilimali watu unao, Amri ipo mikononi na kinywani pako, Tuliza jiji litulie Kama bahari,

Kwa Sasa iwe mwanzo na mwisho kwa hao vibaka kujitawala hapo DSM maana umepewa kila kitu, unataka Nini kingine ambacho hao vibaka wamekuzidi wewe na vyombo vyako vya ulinzi na usalama? Ni Mimi Lucas Mwashambwa, kijana toka mkoani mzalendo na mpenda nchi yangu
 
Wazaramo, wamatumbi na wakwere pamoja na watu wa kusini mbadilike sana. Nimeishi na kukulia hapo dsm nashuhudia life style yenu ni ya kiswahili kweli. Mnazaa mnapeleka watoto shuleni lkn darasa la saba ndiyo kikomo chenu.

Msisitizo katika elimu hakuna na hatimaye mnajenga kundi kubwa la vijana wasio na elimu mtaani hata ajira pia.

Kumbukeni kuwaandaa vijana wajitegemee wenyewe watakapofikia rika la utu uzima.

Watoto wenu wengi ni wanywa pombe za kienyeji na dawa za kulevya na wazazi mkiambiwa ukweli mnawatetea watoto wenu.

Mjue kuzaa na kusomesha (kuwaandaa watoto wenu vizuri)
 
Iambie na serikali iwekeze nguvu kuzuia idadi ya ongezeko la watu, elimu na huduma za uzazi wa mpango ziimarishwe. Watu wasizae hovyo hovyo tu.
 
Hizo ndizo athari za maamuzi mabaya ya kiuchumi ya awamu ya tano. Private sector ilikua suffocated ikashindwa ku-absorb vijana kwa kuwapatia ajira
 
Hilo Ni jukumu lako pia maana Kama Ni juu ya serikali ilishafanya Sana kazi hiyo ya kutoa Elimu kuanzia mitaani Hadi mashuleni, Sasa unataka serikali ije iseme wewe na wewe msizae Tena?
 
Serikali ya dsm imeshindwa kazi..iruhusu raia wamiliki gun tu uone kama kuna cha panya road atakatisha mitaani

#MaendeleoHayanaChama
 
Magufuli alisema zaeni tu msiogope mabeberu.

Hao mliozaa ndio wanawatahiri kwa mapanga.
 
Hizo ndizo athari za maamuzi mabaya ya kiuchumi ya awamu ya tano. Private sector ilikua suffocated ikashindwa ku-absorb vijana kwa kuwapatia ajira
Jiulize mbona hawakujaribu kufanya huo ujinga hawamu ya Tano ,ukiwa na akili timamu Hauwezi kupata matatizo Kwa miaka sita uchukue hatua mwaka wa saba,wakati wa Jiwe hata mtu kumuua mpenzi wake Kwa wivu wa mapenzi anaogopa huyo ndio mtawala.
 
Huyo marehemu aliwashika pabaya sana, you cant think straight

Serikali ya dsm imeshindwa kazi..iruhusu raia wamiliki gun tu uone kama kuna cha panya road atakatisha mitaani.

#MaendeleoHayanaChama
Panya Road au vibaka hawawezi ishinda serikali hii na muda siyo mrefu naamini utaona matokeo yake ya kusambaratishwa kwa hao vibaka
 
Njia ni mmoja tu kamata panya road wote vulisha nguo wazamishe kwenye tanuru la moto mpaka wawe majivu hiyo ndiyo njia iliyo bora nayo pendekeza.

Halafu tazama ndani ya mwezi mmoja tu kama kuta kuwa na huo utitiri wa kijinga uitwao panya road.
 
Unaonekana uko vizuri pale ubongo wako unapokuwa huru kufikiria mambo kwa ujumla wake, tatizo lako kwenye issue ya siasa umejibana mind yako iwe ya kusifia tu, ndio maana huwa unaandika vitu visivyoeleweka kwasababu unajilazimisha kumsifia Samia tu, hata kwa yale yasiyostahili sifa.
 
RC adili na wanao fadhili hawa watoto wahuni, wakipata wanao watuma, naamini kuna mtu yuko nyuma ya hawa watoto, na huyo mtu ashughulikiwe na afungwe na kunyongwa, pia watoto hawa wakikamatwa wafungwe maisha, hatuwezi kuwa na nchi kikundi cha kihuni kinafadhiliwa labda na mtu fulani na kuumiza wananchi tena wanaua kabisa, mm nasema serikali ina macho makali sana, ipate mfadhili hata mmoja tu wa hawa watoto, huu ujinga utaisha milele, i wish i could be IGP, weeee, yaani, huu uchafu uchafu ningesafisha in a day.
 
Umeandika ndefu sana, wanajeshi, JKT na polisi watoke makambini kwa kutumia waliokamatwa mtandao upatikane na wanigwe wote juu kwa juu hautaona panya wala nguchiro, utakuja kunishukuru
 
Unaonekana uko vizuri pale ubongo wako unapokuwa huru kufikiria mambo kwa ujumla wake, tatizo lako kwenye issue ya siasa umejibana mind yako iwe ya kusifia tu, ndio maana huwa unaandika vitu visivyoeleweka kwasababu unajilazimisha kumsifia Samia tu, hata kwa yale yasiyostahili sifa.
Hapana mimi huwa naandika mtizamo wangu ambao natoa Uhuru wa kukosolewa kwa hoja
 
RC adili na wanao fadhili hawa watoto wahuni, wakipata wanao watuma, naamini kuna mtu yuko nyuma ya hawa watoto, na huyo mtu ashughulikiwe na afungwe na kunyongwa, pia watoto hawa wakikamatwa wafungwe maisha, hatuwezi kuwa na nchi kikundi cha kihuni kinafadhiliwa labda na mtu fulani na kuumiza wananchi tena wanaua kabisa, mm nasema serikali ina macho makali sana, ipate mfadhili hata mmoja tu wa hawa watoto, huu ujinga utaisha milele, i wish i could be IGP, weeee, yaani, huu uchafu uchafu ningesafisha in a day.
Naamini katika hili hakuna jiwe litaachwa bila kufunguliwa ili watu waishi kwa amani na utulivu
 
Njia ni mmoja tu kamata panya road wote vulisha nguo wazamishe kwenye tanuru la moto mpaka wawe majivu hiyo ndiyo njia iliyo bora nayo pendekeza.

Halafu tazama ndani ya mwezi mmoja tu kama kuta kuwa na huo utitiri wa kijinga uitwao panya road.
Lazima Hawa vibaka waonyeshwe gharama ya matendo yao
 
Back
Top Bottom