Barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli

Hapo sasa wakati wale wazee weru wa zamani hawakwenda shule lakini silaha walizishika na kutumia vizuri tuu siku hizi wanaajiri wasomi kujifanya tecnokojia imekua mwisho wa siku hao hao wasomi wanakuja wasumbua kama nijeria hapo.mi naona jeshi lingebalace n wenye elimu ndogo hata nidhamu inaongezeka siku hizi askari nidhamu bure kabisa
Ila wawafikirie waende tu RTS kama watashindwa au kufa juu yao maana ni wamependa wenyewe vijana

Ninawaona maafisa wengi tu wa nyota mbili wakiwa na miili ya magonjwa hayo ya Bp, moyo wakati Mtu Wa nyota mbili ni mpiganaji Kama private tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiwarhoapandenga.
Maono yako yanaweza kuwa sahihi kwa unavyoona ila wakubwa wanajua yote haya, tatizo pia wanalijua kwa nini hawawezi kuwekeza kwa vijana kama hao.

Pili kama unasafiri nchini basi utakuwa umepita njia ya Bagamoyo kutokea msata pale kati kuna vijana wetu waliamua kuingia kwenye kilimo na wanafanya vizuri, lakini mpaka kufikia pale wamekumbana na dhoruba mbalimbali.

Ila kwa hawa nimewapa wazo lile ikishindikana waungane kuomba aridhi kisha benki, sisi tupo tutawadhamini.
 
Huwa nawaonea sana huruma walioko uraiani unakuta mtu mzalendo kweli kweli karudi nyumbani.
Yaani kwa mfano serikal iseme iwarudishe jeshini alafu hakuna posho utumikie jeshi bure miaka hata 10 ndio uanze kula mshahara vijana wazalendo wapo tayari wanaumia sana basi tuu
God's plan.
 
Hapo sasa wakati wale wazee weru wa zamani hawakwenda shule lakini silaha walizishika na kutumia vizuri tuu siku hizi wanaajiri wasomi kujifanya tecnokojia imekua mwisho wa siku hao hao wasomi wanakuja wasumbua kama nijeria hapo.mi naona jeshi lingebalace n wenye elimu ndogo hata nidhamu inaongezeka siku hizi askari nidhamu bure kabisa
Halichukui elimu kubwa siku hizi ni six kushuka chini
 
Thamani yenu imeshaonekana,tafuteni kazi nyingi mfanye,au mnataka malipo ya kuwa wazelendo?
UNFIT maana ake tuna matatzo ya kiafya.

Ni suala gum kdg kulizungumzia kiundani zaid, lakn kikubwa tunazd kumuomba mwenyez mung siku moja bas ifke na sisi ionekane thamani yetu na mchango wetu katika kulijenga Taifa.
Ahsante sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi kama hiyo amri ya wao kuajiriwa haikufuatiwa na ongezeko la bejeti ya mishahara ya waajiriwa wapya? Na wale wengine wamejitolea sehemu nyingine kwa muda mrefu ambao hawakapata fursa ya kuonekana na Rais wao nani awatetee waweze kupewa kipaumbele? Sakasaka Mao,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unawaza kwa akili nyepesi sana, hiyo pesa ya serikali kujengea watu viwanda itatoka wapi? Hao vijana wanaweza kuendesha kiwanda kibiashara kizalishe na kisife bila kutegemea ruzuku ya serikali? Kama ni mashamba si wangeachwa huko huko walipokuwa waendelee kulima? Kiwarhoapandenga,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulijufunza nini huko ukiacha hizo nyimbo na morali?
Nakumbuka enzi hizo sisi tulikuwaga tunaimbaga kawimbo haka “” KATOTO KADOGO KANALI****a Jimama “”.

Chenja zile sitokaa nizisahau aisee, full morali,

TANZANIA YANGU EE, NAKUPENDA.

Poleni sana vijana, na imani mweshimiwa litamfikia hili ombi lenu, Mnasitahili kwakweli .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi kama hiyo amri ya wao kuajiriwa haikufuatiwa na ongezeko la bejeti ya mishahara ya waajiriwa wapya? Na wale wengine wamejitolea sehemu nyingine kwa muda mrefu ambao hawakapata fursa ya kuonekana na Rais wao nani awatetee waweze kupewa kipaumbele?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tunazungumzia point moja tu inayohusu maagizo ya rais kuajiri vijana wa Jkt, intake flani waliojitolea na kufanikisha kujenga majumba ya kiserikali kwa wakati.

Rais hakutoa maagizo ya kuajiri vijana wote wa Jkt ama kada zote zilizokuwa zikijitolea nchini wakati akitoa maagizo hayo, ni baadhi.

Haya malalamiko ya hawa vijana yana mashiko sana, sema hayajamfikia Jpm mwenyewe.

Kauli ya rais huwa ni kauli ya mwisho ambayo haijadiliwi, kupindishwa ama kupuuzwa kwa namna yoyote ile.

Kwa mfano hao kama ni unfit kweli kwenye jeshi, hawajawa unfit kwa kila sekta ya ajira nchini, zawadi hiyo ya ajira waliyopewa na mheshimiwa ni haki yao, siyo kubakia wakilalamika na kuzungushwa.

Wakati akitoa tamko la zawadi hiyo ya ajira kwa vijana hao pale Dodoma, nilimsikiliza kwa makini sana , namna ambavyo alikuwa aki emphasize maangizo yake, nikagundua kwamba kuna ubabaishaji na upendeleo mkubwa katika kutekeleza maagizo hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari Mh rais Dr John Pombe Joseph Magufuli, Pole kwa majukumu mazito ya nchi kwa maana ya kitaifa na kimataifa kwa ujumla.

Awali ya yote tunatoa pongezi za dhati kabisa kwa serikali yako ya awamu ya tano, chini ya uongozi wako kwa kazi nzuri ulizozifanya na unazoendelea kuzifanya katika kuliletea maendeleo taifa letu, tunaona miradi mikubwa ya kimaendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo usafirishaji na uchukuzi kama vile ufufuaji wa shirika letu la ndege ATCL ikiambatana na ununuzi wa ndege mpya kabisa.

Ujenzi wa reli mpya kabisa ya umeme (SGR), uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara kuunganisha mkoa na mkoa na kurahisisha mawasiliano,ujenzi wa barabara za juu (flyovers), Upitiaji upya wa mikataba na uboreshwaji wa sheria za madini hii ni kuhakikisha tunalinda rasilimali zetu na kunufaika kama nchi, mradi wa usambazaji wa umeme vijijini REA kupitia wizara ya nishati, haya ni machache tu katika yale mengi unayoyafanya.

Dhamira yako ya dhati na hulka ya kujitoa bila kujali hali hii inadhihirisha kua wewe ni mzalendo wa kweli.

Barua hii ya wazi imeandaliwa na sisi vijana 305 wa JKT tulioshiriki katika miradi mbalimbali ya kitaifa ikiwemo ujenzi wa UKUTA wa Mererani, nyumba 41 za kikosi cha ulinzi wa Rais Buigiri Dodoma, ukuta wa Ikulu Dodoma na ujenzi wa ghorofa 12 za askari Magereza Ukonga Dar es Salaam uliyoikabidhi JWTZ kupitia kamandi ya JKT. Kama unakumbuka mnamo April 13, 2019 wakati wa makabidhiano wa nyumba za mji wa kiserikali pale Mtumba Dodoma ulifurahishwa na kazi nzuri tulizozifanya ukaguswa na kutoa zawadi ya ajira kwa vijana tulioshiriki katika miradi.

Mnamo mwezi wa tisa agizo lako lilitekelezwa na vijana tulipelekwa shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi RTS Kihangaiko Sept 7, 2019 mchakato wa usaili ulianza na kumalizika Oct 19, 2019. Hatutosahau Nov 28, 2019 vijana 305 tulisomwa kama UNFIT na kurudishwa nyumbani, lakini la kuumiza zaidi ni kauli ya kuambiwa tukajitibie, swali la kujiuliza tutajitibia vipi na uwezo wa kifedha ni mdogo?

Ukizingatia sio wote ambao tuliokua na matatizo na hata wale tuliokua na matatizo ni matatizo yaleyale tuliyoyapata moja kwa moja kwenye miradi kwa maana ya kimazingira na kazi ngumu tulizokua tukizifanya.

Lengo la kukuandikia Mh rais kama baba yetu na kama mzazi wetu tunaomba utusaidie vijana wako na utufikirie, sio tu kwa kurudishwa kule RTS tulipotoka la hasha bali kwa sehemu yeyote ile utakayoguswa na kuona tunaweza kufit, baba yetu wengi wetu sisi ni watoto wa masikini na wazazi walitutegemea sisi katika kuwainua ila matokeo yake tumekua mzigo kwa familia zetu.

Hatukupenda kufikisha kwako ujumbe huu kupitia huku lakini tulifanya jitihada nyingi kufikisha kilio chetu toka mwezi wa kumi na moja na kipindi upo mapumzikoni Chato kwa kutumia viongozi na wakubwa wa kiserikali na kupitia vyombo vyako vya usalama lakini mambo yalikua magumu na vikwazo vingi ila kupitia barua hii ya wazi tuna amini utalipata nakulifanyia kazi.

Tuna kutakia kazi njema na afya njema baba yetu kipenzi na raisi wetu mpendwa Dr John Pombe Joseph Magufuli

Mungu ibariki Tanzania.

IMG_20190117_103901.jpg
 
sidhani kama atasoma we tafuteni mawasiliano na CDF
ba kama mafunzo ya jeshi yamewashinda matofali juu ya ghorofa mlipandishaje
au mlimuuzia mkula mbuzi kwa gunia
 
Back
Top Bottom