Bashungwa awaasa Vijana kutotumia Pombe muda wa kazi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa, ametoa wito kwa vijana kuacha tabia ya kutumia Pombe na Vilevi ndani ya muda wa kazi kwani kufanya hivyo kunaathiri kufanya kazi kwa ufanisi.

Bashungwa ametoa wito huo wakati akizungumza na Kijana anayeshona viatu katika Mji wa Kayanga wilayani Karagwe, Moladius Masinde na kujionea akitumia kilevi katika eneo la kazi.

“Baada ya kufanya kazi, jioni unaweza kunywa kiasi lakini sasa hivi ni asubuhi upo kazini na ikifika mchana utakuwa umelewa na utashindwa kushona viatu na unaweza kujitoboa”, Waziri Bashungwa akimshauri Moladius.

Katika kuhakikisha anawasaidia vijana kujikwamua kiuchumi, Bashungwa mara baada ya kuongea na kijana huyo, Moladius amemuongezea mtaji wa kazi yake ya ushonaji wa viatu ili umuwezeshe kutekeleza majukumu yake.

 
Back
Top Bottom