Barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli

Habari Mh rais Dr John Pombe Joseph Magufuli, Pole kwa majukumu mazito ya nchi kwa maana ya kitaifa na kimataifa kwa ujumla.

Awali ya yote tunatoa pongezi za dhati kabisa kwa serikali yako ya awamu ya tano, chini ya uongozi wako kwa kazi nzuri ulizozifanya na unazoendelea kuzifanya katika kuliletea maendeleo taifa letu, tunaona miradi mikubwa ya kimaendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo usafirishaji na uchukuzi kama vile ufufuaji wa shirika letu la ndege ATCL ikiambatana na ununuzi wa ndege mpya kabisa.

Ujenzi wa reli mpya kabisa ya umeme (SGR), uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara kuunganisha mkoa na mkoa na kurahisisha mawasiliano,ujenzi wa barabara za juu (flyovers), Upitiaji upya wa mikataba na uboreshwaji wa sheria za madini hii ni kuhakikisha tunalinda rasilimali zetu na kunufaika kama nchi, mradi wa usambazaji wa umeme vijijini REA kupitia wizara ya nishati, haya ni machache tu katika yale mengi unayoyafanya.

Dhamira yako ya dhati na hulka ya kujitoa bila kujali hali hii inadhihirisha kua wewe ni mzalendo wa kweli.

Barua hii ya wazi imeandaliwa na sisi vijana 305 wa JKT tulioshiriki katika miradi mbalimbali ya kitaifa ikiwemo ujenzi wa UKUTA wa Mererani, nyumba 41 za kikosi cha ulinzi wa Rais Buigiri Dodoma, ukuta wa Ikulu Dodoma na ujenzi wa ghorofa 12 za askari Magereza Ukonga Dar es Salaam uliyoikabidhi JWTZ kupitia kamandi ya JKT. Kama unakumbuka mnamo April 13, 2019 wakati wa makabidhiano wa nyumba za mji wa kiserikali pale Mtumba Dodoma ulifurahishwa na kazi nzuri tulizozifanya ukaguswa na kutoa zawadi ya ajira kwa vijana tulioshiriki katika miradi.

Mnamo mwezi wa tisa agizo lako lilitekelezwa na vijana tulipelekwa shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi RTS Kihangaiko Sept 7, 2019 mchakato wa usaili ulianza na kumalizika Oct 19, 2019. Hatutosahau Nov 28, 2019 vijana 305 tulisomwa kama UNFIT na kurudishwa nyumbani, lakini la kuumiza zaidi ni kauli ya kuambiwa tukajitibie, swali la kujiuliza tutajitibia vipi na uwezo wa kifedha ni mdogo?

Ukizingatia matatizo tuliorudishwa nayo ni yale tuliyoyapata moja kwa moja kwenye miradi kwa maana ya kimazingira na kazi ngumu tulizokua tukizifanya.

Lengo la kukuandikia Mh rais kama baba yetu na kama mzazi wetu tunaomba utusaidie vijana wako na utufikirie, sio tu kwa kurudishwa kule RTS tulipotoka la hasha bali kwa sehemu yeyote ile utakayoguswa na kuona tunaweza kufit, baba yetu wengi wetu sisi ni watoto wa masikini na wazazi walitutegemea sisi katika kuwainua ila matokeo yake tumekua mzigo kwa familia zetu.

Hatukupenda kufikisha kwako ujumbe huu kupitia huku lakini tulifanya jitihada nyingi kufikisha kilio chetu toka mwezi wa kumi na moja na kipindi upo mapumzikoni Chato kwa kutumia viongozi na wakubwa wa kiserikali na kupitia vyombo vyako vya usalama lakini mambo yalikua magumu na vikwazo vingi ila kupitia barua hii ya wazi tuna amin utalipata nakulifanyia kazi.

Tuna kutakia kazi njema na afya njema baba yetu kipenzi na raisi wetu mpendwa Dr John Pombe Joseph Magufuli

Mungu ibariki Tanzania.


View attachment 1361142
Kwanza polen sana vijana,suala lenu nlilisikia toka mwez wa kumi na mbili mwaka jana kuna dogo nae n muhanga WA hili,aliniambia ukweli kuhusu hili suala ,kwanza ni utata WA usaili kwa maana ya kusailiwa watu ambao hawakushiriki kwenye miradi au Ambao hawakua kwenye idadi ya raisi mpendwa Dr John pombe Joseph magufuli aliyoitoa pale dodoma,pili ni matatizo mliorudishwa ni yale ambayo mliyapata mkiwa kwenye miradi, so sad ila aliniambia mlipeleka malalamiko kwa kumfuata raisi akiwa chato lakn wawakilishi wake walikua wanaleta vizingiti taharifa zisifike kwa mzee,. polen Sana ile ilikua zawadi kwenu lakin imekua maumivu kwenu kama kweli raisi anapitia hapa naomba awa angalie kwa jicho lingine mchango wenu ni mkubwa hamkupaswa Kulipwa hik walichowafanyia raisi ana dhamira ya dhati kuwapa zawadi ya ajira ila shida ni kwa wale anaowapa majukumu kusimamia sio wazalendo ni wabinafsi wa kutaka ndugu zao na familia zao zifaifike ,ifike Mahala viongozi wanaopewa dhamana kusimamia maagizo ya amri jesh mkuu watumie busara na hekima katk kutekeleza majukumu.polen sana Mungu atawalipia
 
Basi kama ni hivyo kwa kuwa wana taarifa zao tayari basi kuna fursa nyingine wataitwa tena.Tuwape muda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa jinsi mambo yalivyo ebu fuatilieni mana agizo lilikua wazi kwa raisi vijana opp magufuli wapatiwe ajira na alisema idadi yenu haizidi mia nane iweje wachukuliwe baadhi wengine waachwe? Ndo yale yale raisi ana dhamira ya dhat kbsa kwa wananchi wake ila wawakilshi wake wanamuangusha
 
Back
Top Bottom