Barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli

sidhani kama atasoma we tafuteni mawasiliano na CDF
ba kama mafunzo ya jeshi yamewashinda matofali juu ya ghorofa mlipandishaje
au mlimuuzia mkula mbuzi kwa gunia
Hayo ni maswali ambayo unaweza kujiulza na ukapata majibu waz kwa kufkri tu.
 
Viongozi wa JWTZ wako sawa. Ili uingie pale lazima uwe umetimiza masharti yao yote. Mfano hata urefu wa mtu ni kigezo, alama yeyote mwilini ni kigezo nk. Tuwe na wanajeshi ambao wana vigezo vyote vyote vinavyotakiwa. Hapa hakuna cha upemdeleo.
 
Kiwarhoapandenga.
Maono yako yanaweza kuwa sahihi kwa unavyoona ila wakubwa wanajua yote haya, tatizo pia wanalijua kwa nini hawawezi kuwekeza kwa vijana kama hao.

Pili kama unasafiri nchini basi utakuwa umepita njia ya Bagamoyo kutokea msata pale kati kuna vijana wetu waliamua kuingia kwenye kilimo na wanafanya vizuri, lakini mpaka kufikia pale wamekumbana na dhoruba mbalimbali.

Ila kwa hawa nimewapa wazo lile ikishindikana waungane kuomba aridhi kisha benki, sisi tupo tutawadhamini.
China inawekeza kwa wafungwa mnashindwa nini kuwekeza kwa hawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari Mh rais Dr John Pombe Joseph Magufuli, Pole kwa majukumu mazito ya nchi kwa maana ya kitaifa na kimataifa kwa ujumla.

Awali ya yote tunatoa pongezi za dhati kabisa kwa serikali yako ya awamu ya tano, chini ya uongozi wako kwa kazi nzuri ulizozifanya na unazoendelea kuzifanya katika kuliletea maendeleo taifa letu, tunaona miradi mikubwa ya kimaendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo usafirishaji na uchukuzi kama vile ufufuaji wa shirika letu la ndege ATCL ikiambatana na ununuzi wa ndege mpya kabisa.

Ujenzi wa reli mpya kabisa ya umeme (SGR), uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara kuunganisha mkoa na mkoa na kurahisisha mawasiliano,ujenzi wa barabara za juu (flyovers), Upitiaji upya wa mikataba na uboreshwaji wa sheria za madini hii ni kuhakikisha tunalinda rasilimali zetu na kunufaika kama nchi, mradi wa usambazaji wa umeme vijijini REA kupitia wizara ya nishati, haya ni machache tu katika yale mengi unayoyafanya.

Dhamira yako ya dhati na hulka ya kujitoa bila kujali hali hii inadhihirisha kua wewe ni mzalendo wa kweli.

Barua hii ya wazi imeandaliwa na sisi vijana 305 wa JKT tulioshiriki katika miradi mbalimbali ya kitaifa ikiwemo ujenzi wa UKUTA wa Mererani, nyumba 41 za kikosi cha ulinzi wa Rais Buigiri Dodoma, ukuta wa Ikulu Dodoma na ujenzi wa ghorofa 12 za askari Magereza Ukonga Dar es Salaam uliyoikabidhi JWTZ kupitia kamandi ya JKT. Kama unakumbuka mnamo April 13, 2019 wakati wa makabidhiano wa nyumba za mji wa kiserikali pale Mtumba Dodoma ulifurahishwa na kazi nzuri tulizozifanya ukaguswa na kutoa zawadi ya ajira kwa vijana tulioshiriki katika miradi.

Mnamo mwezi wa tisa agizo lako lilitekelezwa na vijana tulipelekwa shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi RTS Kihangaiko Sept 7, 2019 mchakato wa usaili ulianza na kumalizika Oct 19, 2019. Hatutosahau Nov 28, 2019 vijana 305 tulisomwa kama UNFIT na kurudishwa nyumbani, lakini la kuumiza zaidi ni kauli ya kuambiwa tukajitibie, swali la kujiuliza tutajitibia vipi na uwezo wa kifedha ni mdogo?

Ukizingatia matatizo tuliorudishwa nayo ni yale tuliyoyapata moja kwa moja kwenye miradi kwa maana ya kimazingira na kazi ngumu tulizokua tukizifanya.

Lengo la kukuandikia Mh rais kama baba yetu na kama mzazi wetu tunaomba utusaidie vijana wako na utufikirie, sio tu kwa kurudishwa kule RTS tulipotoka la hasha bali kwa sehemu yeyote ile utakayoguswa na kuona tunaweza kufit, baba yetu wengi wetu sisi ni watoto wa masikini na wazazi walitutegemea sisi katika kuwainua ila matokeo yake tumekua mzigo kwa familia zetu.

Hatukupenda kufikisha kwako ujumbe huu kupitia huku lakini tulifanya jitihada nyingi kufikisha kilio chetu toka mwezi wa kumi na moja na kipindi upo mapumzikoni Chato kwa kutumia viongozi na wakubwa wa kiserikali na kupitia vyombo vyako vya usalama lakini mambo yalikua magumu na vikwazo vingi ila kupitia barua hii ya wazi tuna amin utalipata nakulifanyia kazi.

Tuna kutakia kazi njema na afya njema baba yetu kipenzi na raisi wetu mpendwa Dr John Pombe Joseph Magufuli

Mungu ibariki Tanzania.


View attachment 1361142
Habari nimesoma vma barua hii au ujumbe huu polen san vijana kwa kuumia kwa kazo ngumu za kujenga taifa na kuwa wazalendo wa nchi yetu na tumaini rais aliwapa pongezi na kuwatakia ajira ili muwez kupambania nchi yetu lakini naumia sana kuona watu 305 wote kutolewa katka ajira wakati wote mlikuwa mnajenga nchi imeniuma sana nilipoona hii barua naomba mungu asimamie kuna secta nyingi sana za kuwaweka angalau maisha yaendelee mungu ampe moyo mwepesi rais aweze kutoa maamuz sahii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wa JWTZ wako sawa. Ili uingie pale lazima uwe umetimiza masharti yao yote. Mfano hata urefu wa mtu ni kigezo, alama yeyote mwilini ni kigezo nk. Tuwe na wanajeshi ambao wana vigezo vyote vyote vinavyotakiwa. Hapa hakuna cha upemdeleo.
Vijana wako sahihi,sema ujui lile ni Agizo la Rais uwa alipingwi wala kujadiliwa ilo usemalo wew n sahihi kuna watu walijenga daraja kilosa na wengine kujenga majengo baadhi pale Dodoma walipewa Ajira pale pale bila shuruti wala kubaguliwa,polen ndg zangu bhana dah.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wap wakilishi wafikish jambo hil
Kiwarhoapandenga, ulichoongea ni sahihi lkn watapita km hawaoni ifike mahala taasisi za kifedha wa invest kwenye idea...km.....nje na serikali iweke mkono wake....mfumo wa scheme plantation urudishwe usimamiwe chakula kiuzwe nje pesa ipatikane watu walipwe naisha yaende wakati mwingine tuige mawazo ya waliotunyanyasa(wakoloni) serikali ikiweka kambi kama wafanyavyo jkt kwenye kilimo.

unabeba watu mtaani wanapiga kazi kwann tuwe maskini wakati tunakila kitu...kwann tuwe na tamaa kwa kujiangalia mimi...ebu ona hawa vijana wameachwa baada ya wao ma alwatani kunufaika wamesha wadump!...siasa ziwekwe pembeni tuishi uharisia wa maisha....mnataka watu wawe wezi kwann hatumuogopi MUNGU ifike mahala wanasiasa waache kuroga wasimamie ukweli na wakifanyie kazi na MUNGU atafungua njia.

Sio kupata uongozi wa madawa afu mnabaki kujiineemesha wenyewe....mpk hapa TZ ikiamua kujismamia wenyewe tunafika mbali ila mpango wa kilimo ni sanaa tupu hakuna kiongozi tena hawa wanojiita wana PHD. hakuna wanaozungumzia kupaumbele kwenye kilimo wote ni kujineemesha na kufidia jinsi alivyosota kusoma shuleni.

hakuna elimu inayomnufaisha mwanafunzi,mtaani hakuna kinachomnufaisha mwananchi serikali inataka watu wafanyenn haya maisha mpk lini...kila siku nafuu ya jana....nini dhamila ya serikali kwa wananchi wake...ebu angalieni hawa vijana ndio tegemeo katika nchi yoyote tuwe wazalendo kwenye nchi yetu.

tuingiwe roho ya upendo na kuthamini nchi yetu tujivunie kile tulichonacho na kukisimamia...utaona pesa hakuna lkn kipindi hiki cha uchaguzi pesa ipo kuhadaa watu....ebu tuweni wazalendo...kuanzia RAISI MPAKA MWANANCHI WA MWISHO tuipeperushe bendera ya TANZANIA popote pale kwa manufaa, mnisamehe kutofata alama za uandishi na MUNGU anisamehe nmeandika kwa hasira sana....ila naipenda nchi yangu TANZANIA.

HOT

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo swala la nyie kuwa UNFIT shida ilikuwa ni nini hata???...maanake it doesnt make sense vijana 305 wote muwe na mapungufu...kama mlikuwa UNFIT hiyo miradi mlifanikisha vipi....?????
Aise neno UNFIT kabla ya kuwa recruited katika vyombo vya ulinzi na usalama huwa inamaisha nini? Huwenda hawako physical fit na hapa huwa ni papana pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika Dunia hii wanaojitoa sadaka kwa ajili ya wengine hufanya hivyo kwa kuutoa hata uhai wao.
Kumbuka wakati wa Vita ya Tanzania na Uganda, vijana wengi wa mgambo walichukuliwa vijijini kwenda kupigana. Wengine walipoteza maisha, wengine walipata ulemavu na waliorudi salama hawakufaidika sana zaidi ya kurudi kijijini na kuendelea na maisha ya kawaida.
Tunamwomba Rais wetu afanye fadhila na kuwapa shake hand au mkono wa pole na kwaheri kwa kuwatunuku na kuwapa msaada kidogo.
Hata kupewa heshima tu ya medali ina maana zaidi kuliko pesa.
Katika Inchi yetu Waathirika wa aina hii ni wengi na kuna wakati wanajiona kama wao si Watanzania ukilinganisha na wengine ambao wanafaidi matunda ya Inchi hii kwa kwenda mbele.
Kuna Double standard nyingi sana katika kuwapa haki Watanzania walio wengi.
Rais aliyeko madarakani anajitahidi sana kuondoa kero hizi kwa mtu moja moja na kwa makundi ya watu.
Kwa mfano kwenye swala Zima la nyumba za umma, Kuna watumishi wengi wa Serikali wametumia nafasi ya kuuziwa nyumba Watanzania walioko kwenye nyumba hizo kwa kuwanyanyasa na kuwatoa ili wao wanunue nyumba hizo.
Rais wetu amekemea hili na kumekuwa na utulivu kidogo ingawaje mbinu chafu bado ziko pale pale.
Mafao ya Watumishi yanatofautiana sana. Wengine wanapewa mamilioni ya pesa lakini wengine hawalipwi kabisa kwa sababu viongozi wao wa juu waliiba mali ya umma na kufanya mashirika hayo ya umma kufilisika.
 
Ukizingatia matatizo tuliorudishwa nayo ni yale tuliyoyapata moja kwa moja kwenye miradi kwa maana ya kimazingira na kazi ngumu tulizokua tukizifanya.


Malipo ya kuoka kwa Mungu ndiyo malipo yenye thamani kubwa kuliko kingine chochote
 
Back
Top Bottom