Barua ya wazi kwa baadhi ya mabalozi wa nje wanaowakilisha mataifa yao nchini Tanzania

Besta Mlagila

Senior Member
May 29, 2018
101
191
NINASTAAJABISHWA sana na mwenendo wa kushtusha wa baadhi ya Mabalozi walioko Tanzania kwa kusigina kiwazi wazi maadili ya kazi zao.

Tanzania ni nchi yenye upendo mwingi. Watu wake ni wakarimu sana na wanawaamini wageni, ikiwa ni pamoja na Mabalozi wa Mataifa ya kigeni hapa nchini.

Mabalozi hao wanalijua hili fika. "We are peaceable and welcoming." Lakini, baadhi ya Mabalozi hao wanatuchukulia poa sana.

Niliwahi kumfukuza mgeni, tena nilimshikia panga, alipokuja nyumbani, siku ya kwanza, ya pili nikamkuta anachungulia chumba changu cha kulala, mke wangu alikuwa hajarudi kutoka kazini. Urafiki uliisha siku hiyo hiyo na alienda kulala guest. Hovyo kabisa.

Ukarimu wetu ndio umetufanya hata tusishupalie sera na protokali za kidiplomasia zinazowataka Mabalozi watoe taarifa kila wanapotaka kufanya ziara mahali popote nchini. Lakini, mtu muungwana, hahitaji kumbushwa kila wakati. Anatakiwa ajue wajibu wake na kuutekeleza.

Wapo Mabalozi hapa nchini ambao wanajiona kana kwamba ni sehemu ya raia wanaharakati wa Kitanzania. Wapo wanaokiuka Azimio la Vienna kwa matendo yao yasiyozingatia matakwa ya uwakilishi wa nchi zao hapa kwetu.

Mfano, ni ajabu sana kwa Balozi kuamua kwenda Mahakamani kusikiliza kesi ya kiongozi wa Chama cha Upinzani bila kutoa taarifa kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Mahakama utadhani wao pia ni Mawakili.

Mbona kesi za akina Rugemalila, Singasinga, Mzee Yona na Marehemu Basil Mramba, ambazo zilikuwa zinavuta hisia kubwa za Watanzania walikuwa hawaendi? Kwanini upinzani ghafla uwe swahiba kiasi hicho? Kuna nini nyuma ya pazia?

Ninaomba Serikali iifanyie kazi kadhia hii ya kuchungulia hadi katika vyumba vya kulala bila hata hodi. Aidha, mimi mwananchi wa kawaida nakerekwa sana na uhuru huu wa Mabalozi wetu, usiozingatia makubaliano ya Kimataifa na staha ya Kidiplomasia.

Ndio maana, hivi karibuni, Waziri wetu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mwanadiplomasia Nguli, Liberata Mulamula, Agosti 20 mwaka huu, aliwataka wazingatie Sheria na taratibu au protokali za kidiplomasia, inapotokea wanataka kwenda kusikiliza kesi za Wapinzani Mahakamani.

Alikumbusha kuwa wana wajibu wa kutoa taarifa katika Mamlaka husika iwapo wanapenda kwenda Mahakamani kufuatilia mwenendo wa kesi.

Mwanadiplomasia mmoja nguli, anasema kuwa, Mabalozi hawa wanapaswa kuomba ridhaa (consent) ya Mahakama kama wanaweza kuhudhuria kesi flani.

Badala ya kufuata protokali hizo, wao wanakubaliana tu na Mawakili wa Washtakiwa, Diplomasia gani hii?

Wananchi wengi wenye uelewa wa mambo ya kidiplomasia, wanalaani usiginaji huo wa Sheria na taratibu za kidiplomasia huku wenyewe wakiwa mstari wa mbele kukosoa pale taratibu zinapoonekana kukiukwa kwenye maeneo mengine.

"Wanakwenda Mahakamani kutaka kuona kama haki inatendeka wakati wao wenyewe hawatendi haki pale wanapokiuka Sheria na taratibu za Kidiplomasia ya Kimataifa. Ninaomba Mamlaka husika, hasa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, pamoja na Mahakama, wachukue hatua.

Mabalozi hawa wanaonekana kuwa na kiherehere, wanaosigina taratibu husika na kudai wengine wafuate taratibu, wajitathmini.

Mashaka Masinde, mchambuzi wa Diplomasia ya Kimataifa, Cardiff, United Kingdom.
 
kama unaishi huko kwa malkia kaa kimya bloo, usijifanye mzalenzo ukimbizini.
 
shida jiko hapa mkuu wazungu juwa kuwa hawawezi kufanya kitu kisicho na maslahi mapana ya nchi zao ndicho kinachofanyika unategemea pesa wanazotoa ili kuupa upinzani uje uingie madarakani wanapoona unataka kufeli ni hasara kubwa sana kwao wanapenyeza pesa nyingi sana kwa hao watu wanategemea siku wachukue nchi wafanye yao kuna rasilimali nyingi sana hapa nchini wanazitamani wanashindwa waanzaje
 
..Na sisi tuwaagize mabalozi wetu wakasikilize kesi mbalimbali zinazoendelea ktk mahakama za nchi ambazo mabalozi wao wanakwenda mahakamani kusikiliza kesi ya Mbowe.
 
Ngoja kwanza tutembee na martin martin kule twitter tuupate uhondo wa mawakili wanavyokaangana,english versus swahili.
 
Povu lote la nini? Hebu tuachie waende wkt Fulani mwalim aliwahi kusema police wasiwakataze wananchi kubeba wanasiasa wao baada ya mikutano Zaid wasiwaangushe tu

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Hata SSH na Mulamula watauita huu kwa jina lake kutokana na harufu kali ulio nao.
 
Besta pamoja na msambwanda wako umeshindwa kupambana walau upate nafasi hata ya Ukuu wa wilaya mpaka wakina niki wa pili wamekupita . Hamia upinzani tu sasa
 
Tanzania is fucked up and the next thing you will see is those ambassadors taking seats in a Tanzanian parliament,, Tanzanian leaders can't speak nor voice their concerns openly on the faces of those ambassadors who show their true colours or intentions in their so called representation. TANZANIA IS FUCKED TO APOINT THE GERMANYS AND AMERICANS CAN DO ANYTHING THEY WANT
 
Balozi kwenda mahakamani umepungukiwa nini au asipokwenda utaongeza nini?

Kama huna makando kando hofu yako nini?

Unachukia tu balozi kwenda mahakamani ila balozi wa china alivyovyaa kofia ya ccm na kupanda jukwaani hilo halikuudhi?

Kunya anye kuku akinya akinya bata.
 
Kinachowapeleka si Chadema bali ni swala nyeti la ugaidi ili watafakari uwepo wao nchini kama ni salama. Mabalozi wengi nchi husika ikiwa na ugaidi huondoa raia wao na hubaki wachache sana ambao ni walazima tu.

Unachotakiwa ni kuomba Mbowe ashindwe kesi ili Tanzania iingie rasmi kwenye nchi hatarishi.
 
Back
Top Bottom