Barua ya wazi kwa Askofu Fred Shoo

Barua ya wazi kwa Askofu Fred Shoo

Salam katika jina la bwana wetu Yesu Kristo.

Kwa mara ya kwanza kanisa letu linapitia ugumu kutokana na mtindo wako wa mkono wa chuma na ubinafsi wa maoni na fikra.

Baba askofu kanisa ni chombo "laini" (delicate) hivyo kuwa makini kwani waumini wana mitazamo yao na mararajio kutoka katika kanisa lao.

Usiturudishe tuliko toka hasa sisi waumini wa DMP kwani ilituchukua takribani miaka kadhaa ya mgogoro enzi za Jerry Mngwamba hadi kumpata Dr.Malasusa ambaye kwa kiwango kikubwa katuunganisha wana DMP.

Zama hizo za akina Jerry Mngwamba wewe ulikuwa bado upo Uswaaa,Machame.Tunajua huna cha kupoteza zaidi ya kupigania maslahi yako kuwafurasha rafiki zako.

Kuna mambo mengi binafsi unayafanya na kuamua na kisha kujificha kwenye kivuli cha baraza la maaskofu.

Hakika muda unafika na hayo yote unayoyafanya kulibomoa kanisa yatakurudia kwa mtindo wa karma.

Wito wangu kwako ni ujirekebishe kwani muda bado.Siku zote hila mbaya haidumu kwani hudhihirika.Pia jitahidi kuficha hisia zako kisiasa kutokana na nafasi yako kwani utadharaulika na utajuta.

Askofu Shoo lolote ovu dhidi ya Malasusa na DMP halitafanikiwa na mtaumbuka kama wajenzi wa mnara wa babeli.DMP ni kioo cha KKKT hivyo hatutaruhusu wahuni kutaka kuibadilisha DMP kama genge lao kupiga soga.

Mungu ndiye mtetezi wa DMP dhidi ya wote wenye nia ya kutuvuruga na kuibadilisha iwe Chama cha siasa.

Tunamkabidhi MUNGU ole kwao wenye nia ovu.
Kilichotokea siyo maamuzi ya Dr. Shoo ila ni maamuzi ya baraza la maaskofu. Wewe nani hata uingilie maazimio ya kikao cha maaskofu, wenyewe ndo wameamua na sisi waamini tumewakilishwa kila mmoja na Askofu wake. Ikiwa humwamini Askofu wako nenda kashiriki hicho kikao usifanye siasa kwa masuala ya kanisa.
 
Huo waraka upo magazetini na kila pahala si lazima kupoteza muda wa ibada
Kwa hiyo logic kwamba waraka huo upo magazetini ndo ulimfanya Malasusa azuie usisomwe kwenye dayosisi yake, kinyume na makubaliano na maaskofu wenzake?
 
Kweli nimeendelea kujifunza kwenye maoni yenu wachangiaji jinsi siasa inavyowagawa waumini kama vile ushabiki wa mpira vile yanga huku na simba kule!!
 
Hiyo waraka wako upeleke pale Lumumba ambapo upo kwenye payroll yao......

Hivi hawa watumishi wa Mungu kuueleza ukweli kuwa nchi yetu haiendi sawa ndiyo kunakofanya muwaandame kiasi hicho??
Na je Maaskofu ambao walio uacha waraka wanakosa gani hado huyo shoo awaondoe kwenye baraza
 
"Kamanda" maandamano yenye ni ya kuua watanzania 200/300 ni mpango wa Mbowe pale Kinondoni
Naibu waziri hivi unatambua kuwa ukinenacho ni sawa na serikali kusema? Kama serikali mliutambua huo mpango wa Mbowe kuandaa hayo mauaji mlichukua hatua gani kwake?
Nilikuwa namshangaa musiba kwa kauli zake, kumbe waasisi wa kauli hizi ni ccm wote na au wale "sema na sifu" ili ushibe!
Shoo na Mbowe ni level ya juu sana kwako na badala ya kuhangaika nao fikiri jinsi ya kupata tena kiti maalum!
 
Huyu malasusa aamue moja kuitumikia CCM au kulitumikia kanisa
 
Naibu waziri hivi unatambua kuwa ukinenacho ni sawa na serikali kusema? Kama serikali mliutambua huo mpango wa Mbowe kuandaa hayo mauaji mlichukua hatua gani kwake?
Nilikuwa namshangaa musiba kwa kauli zake, kumbe waasisi wa kauli hizi ni ccm wote na au wale "sema na sifu" ili ushibe!
Shoo na Mbowe ni level ya juu sana kwako na badala ya kuhangaika nao fikiri jinsi ya kupata tena kiti maalum!
Jielekeze kwenye barua kama unataka kumsaidia Shoo
 
Jielekeze kwenye barua kama unataka kumsaidia Shoo
Kwani barua hiyo niliandikiwa mimi hadi niijibie? Ingependeza kama ungemwandikia barua ya kiofisi ili naye akujibu kiofisi. Kuileta humu na kuiita barua umepotoka! Itumie nafasi naibu kama kweli unamaanisha kumgombolezea homeboy wako malasusa!
 
Huo waraka upo magazetini na kila pahala si lazima kupoteza muda wa ibada
Mkuu usitoe majibu marahisi kwenye issue nzito kama hii,
Behind the scene lazima kuna watu walimu-approach askofu wetu na yeye aka-give in into their demands,this is not a coincidence eti ilikuwa kwenye mitandao ndo maana haikusomwa,No one will buy this.
Just know the church will never be compromised na askofu will lose.
 
"Kamanda" maandamano yenye ni ya kuua watanzania 200/300 ni mpango wa Mbowe pale Kinondoni
Magufuli ana Amrisha Askari wauwawe Mamia kwa mania ya wananchi anasema anawasapoti wakiwauwa kwa visu wakubwa Yong a ama bunduki anawapa sapoti amewaambia waamuwe watakavyo wanasapoti yake video ya maagizo ipo dunia nzima shame
 
Kunguru wengi mnaojaribu kuwajibu maaskofu hamjui hata chembe ya mifumo ya kkkt au katoliki....!!

Kanisa linapokubaliana jambo na wewe ukapinga hata kwa mtazamo ukiwa sahihi kanisa lina haki ya kukutenga hata kufukuzwa...

Hapa kkkt wametumia busara za hali ya juu...ingekuwa ni waislamu wameamua afu anajitokeza mtu mmoja akapinga ingekuwaje..!!?

Tusikaze vichwa vyetu.
Du, kumbe haya mambo yanahamia Siasa ni!!! Hatari sana.
 
HIVI WARAKA ULIKUWA WA BARAZA LA MAASKOFU AU ULIKUA NI WA ASKOFU SHOO ALIANDIKA MWENYEWE.
 
Back
Top Bottom