Barua ya wazi kwa Askofu Fred Shoo

Barua ya wazi kwa Askofu Fred Shoo

Mbona haujataja huo ukiritimba unao fanywa na huyo Askofu Shoo wenu...[emoji45]
Hapa naona umelalamika tu pasipo kuelezea nini hasa kinacho wasibu hao watumishi wa Mungu.
 
Salam katika jina la bwana wetu Yesu Kristo.

Kwa mara ya kwanza kanisa letu linapitia ugumu kutokana na mtindo wako wa mkono wa chuma na ubinafsi wa maoni na fikra.

Baba askofu kanisa ni chombo "laini" (delicate) hivyo kuwa makini kwani waumini wana mitazamo yao na mararajio kutoka katika kanisa lao.

Usiturudishe tuliko toka hasa sisi waumini wa DMP kwani ilituchukua takribani miaka kadhaa ya mgogoro enzi za Jerry Mngwamba hadi kumpata Dr.Malasusa ambaye kwa kiwango kikubwa katuunganisha wana DMP.

Zama hizo za akina Jerry Mngwamba wewe ulikuwa bado upo Uswaaa,Machame.Tunajua huna cha kupoteza zaidi ya kupigania maslahi yako kuwafurasha rafiki zako.

Kuna mambo mengi binafsi unayafanya na kuamua na kisha kujificha kwenye kivuli cha baraza la maaskofu.

Hakika muda unafika na hayo yote unayoyafanya kulibomoa kanisa yatakurudia kwa mtindo wa karma.

Wito wangu kwako ni ujirekebishe kwani muda bado.Siku zote hila mbaya haidumu kwani hudhihirika.Pia jitahidi kuficha hisia zako kisiasa kutokana na nafasi yako kwani utadharaulika na utajuta.

Askofu Shoo lolote ovu dhidi ya Malasusa na DMP halitafanikiwa na mtaumbuka kama wajenzi wa mnara wa babeli.DMP ni kioo cha KKKT hivyo hatutaruhusu wahuni kutaka kuibadilisha DMP kama genge lao kupiga soga.

Mungu ndiye mtetezi wa DMP dhidi ya wote wenye nia ya kutuvuruga na kuibadilisha iwe Chama cha siasa.

Tunamkabidhi MUNGU ole kwao wenye nia ovu.
Nijibu maswali haya, ni kweli Dr. Malasusa alipanda gari ya Ikulu kuwahi ufunguzi wa upanuzi wa uwanja wa ndege, kama ndio alifanya hivyo kwa minajili ipi na kama nani?

Ni kweli Dr. Malasusa walikaa meza moja na Makonda ilikupinga walaka wa maaskofu wa KKKT?
 
Mbona haujataja huo ukiritimba unao fanywa na huyo Askofu Shoo wenu...[emoji45]
Hapa naona umelalamika tu pasipo kuelezea nini hasa kinacho wasibu hao watumishi wa Mungu.
Tuliza akili soma tena.Hakuna mahala nimeandika Shoo ni mkiritimba
 
Huu ni waraka wa wazi kwa Askofu Shoo ni matumaini yangu atabadilika
Mbona hujaandika chochote kwa maana ya content? Hujasema amefanya nini mpaka kufikia kwenye hilo hitimisho lako.
 
Kunguru wengi mnaojaribu kuwajibu maaskofu hamjui hata chembe ya mifumo ya kkkt au katoliki....!!

Kanisa linapokubaliana jambo na wewe ukapinga hata kwa mtazamo ukiwa sahihi kanisa lina haki ya kukutenga hata kufukuzwa...

Hapa kkkt wametumia busara za hali ya juu...ingekuwa ni waislamu wameamua afu anajitokeza mtu mmoja akapinga ingekuwaje..!!?

Tusikaze vichwa vyetu.
 
Nimeandika kwa Shoo sababu yeye ndiye Mwenyekiti wa Maaskofu KKKT hivyo kwa dhamana hiyo abadilike
Ukiwa m/kiti na akaibuka shetani miongoni mwenu inabidi ufumbe macho ili DMP isigawanyike? Nadhani Malasusa nae anastahili barua ya kutambua collective responsibility na kama alikuwa na dukuduku lingemalizwa kwenye vikao vyao.

J2 njema mtumishi!!
 
Halfu hii hajaandika wakudadavuwa bali kapewa aliweke hapo. Akili yake haina uwezo hu.
 
Kunguru wengi mnaojaribu kuwajibu maaskofu hamjui hata chembe ya mifumo ya kkkt au katoliki....!!

Kanisa linapokubaliana jambo na wewe ukapinga hata kwa mtazamo ukiwa sahihi kanisa lina haki ya kukutenga hata kufukuzwa...

Hapa kkkt wametumia busara za hali ya juu...ingekuwa ni waislamu wameamua afu anajitokeza mtu mmoja akapinga ingekuwaje..!!?

Tusikaze vichwa vyetu.
Hujui uliandikalo
 
Back
Top Bottom