Barua ya wazi kwa Askofu Fred Shoo

Barua ya wazi kwa Askofu Fred Shoo

Salam katika jina la bwana wetu Yesu Kristo.

Kwa mara ya kwanza kanisa letu linapitia ugumu kutokana na mtindo wako wa mkono wa chuma na ubinafsi wa maoni na fikra.

Baba askofu kanisa ni chombo "laini" (delicate) hivyo kuwa makini kwani waumini wana mitazamo yao na mararajio kutoka katika kanisa lao.

Usiturudishe tuliko toka hasa sisi waumini wa DMP kwani ilituchukua takribani miaka kadhaa ya mgogoro enzi za Jerry Mngwamba hadi kumpata Dr.Malasusa ambaye kwa kiwango kikubwa katuunganisha wana DMP.

Zama hizo za akina Jerry Mngwamba wewe ulikuwa bado upo Uswaaa,Machame.Tunajua huna cha kupoteza zaidi ya kupigania maslahi yako kuwafurasha rafiki zako.

Kuna mambo mengi binafsi unayafanya na kuamua na kisha kujificha kwenye kivuli cha baraza la maaskofu.

Hakika muda unafika na hayo yote unayoyafanya kulibomoa kanisa yatakurudia kwa mtindo wa karma.

Wito wangu kwako ni ujirekebishe kwani muda bado.Siku zote hila mbaya haidumu kwani hudhihirika.Pia jitahidi kuficha hisia zako kisiasa kutokana na nafasi yako kwani utadharaulika na utajuta.

Askofu Shoo lolote ovu dhidi ya Malasusa na DMP halitafanikiwa na mtaumbuka kama wajenzi wa mnara wa babeli.DMP ni kioo cha KKKT hivyo hatutaruhusu wahuni kutaka kuibadilisha DMP kama genge lao kupiga soga.

Mungu ndiye mtetezi wa DMP dhidi ya wote wenye nia ya kutuvuruga na kuibadilisha iwe Chama cha siasa.

Tunamkabidhi MUNGU ole kwao wenye nia ovu.
Hakuna kitu kibaya kama kutengwa na wenzako.
Kuzuia waraka usisomwe lilikuwa ni kosa kubwa sana.
Mkuu wakudadavua hakuna jinsi tena lazima ang'oke.
 
Chadema nao wafungue makanisa wamuite Shoo ajiunge nao kwenye ibada za kisiasa na kuandika nyaraka za kisiasa.hapo watakuwa wamefaulu.
 
Hivi kanisa ka KKKT waumini wake wote ni CHADEMA? Wanalilia Democrasia, hapo demokrasia iko wapi kama wao tu kama kanisa wameshindwa tu kuheshimu mawazo ya Askofu mwenzao na kumuita msaliti? Kwahiyo demokrasia ni kuunga mkono
 
Hakuna kitu kibaya kama kutengwa na wenzako.
Kuzuia waraka usisomwe lilikuwa ni kosa kubwa sana.
Mkuu wakudadavua hakuna jinsi tena lazima ang'oke.
Huo waraka upo magazetini na kila pahala si lazima kupoteza muda wa ibada
 
Hivi kanisa ka KKKT waumini wake wote ni CHADEMA? Wanalilia Democrasia, hapo demokrasia iko wapi kama wao tu kama kanisa wameshindwa tu kuheshimu mawazo ya Askofu mwenzao na kumuita msaliti? Kwahiyo demokrasia ni kuunga mkono
Ndio hapo sasa
 
We shetani huwezi kumfunza mpakwa mafuta namna njema ya kuliongoza kanisa, malasusa ni mwasherati na msaliti,alishiriki kutengeneza waraka wa KKKT, bashite na watu wa ikulu wakamvurura na kavurugika kama pengo alivyovurugwa na tumbo baada ya kula maharagwe, pia shoo syo aliyetoa adhabu kwa wavurugwa wako bali maaskofu KKKT ndo walowapa adhabu kuwa makini utavurugwa ki mombasa
Sio wote muliitalo jina la Bwana mtauona ufalme wa Mungu.Mimi nina dhambi lakini sipo katika nafasi ya kuhukumu
 
Ha

Haswaaa, Nakumbuka katika biblia kuna mstari unaosema
" Lakini mimi najua mtetezi wangu yu hai,naye atasimama katika nchi..."
Nami naamini mtetezi wa DR.Malasusa yu hai.Kwa kazi nzuri aliyoifanyia DMP
Mungu atamtetea,Wanaodhani kakosea warudi kwenye maandiko wakajifunze.

Nasema tena kwako Dr.Malasusa, wanadamu wakipambana kukuvua
nguo ili uaibike,Mungu unayemtumikia atakuvika nguo.
na Damu ya Yesu inenayo mema ikutetee katika yote.

Yesu akawaambia " ambaye hana dhambi awe wa kwanza kumpiga mawe.."
maaskofu mnaosimama kuhukumu,je ni kweli Mungu akishuka kuwapima
ni kweli mtaonekana safi?
Hakika
 
Hii yote kisa tu Dr.Malasusa kachukuliwa hatua za kinidhamu na Kanisa? Pengine hamwelewi, Mamlaka ya Kinidhamu kwa Dr.Malasusa ni Kanisa na wala siyo CCM, amepewa nafasi ya kutubu, ni juu yake kuamua kutubu au kuiga tabia ya Rais Magufuli na wana-CCM ya kubishana na wito unaomtaka afanye toba!
Ni Mungu si akina Shoo
 
WanaCCM wa mitandaoni awamu hii ya tano wanatia kinyaa,wamepoteza uwezo wa kujenga hoja kabisa.
 
Back
Top Bottom