Barua Wazi ya Mwanafunzi kwa Walimu Wake Wawili. 1 ni kwa Dean wake, na 2. TA wa Kipindi chake c Kwanza. Please Watendeni Watanzania Haki Hii!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,103
Reaction score
128,722
Wanabodi
N.B:Wakati bandiko hili linaandikwa kumbe tayari CJ。Prof. Ibrahim Juma ameisha staafu rasmi na Jaji Mkuu mpya ameisha teuliwa, hivyo hoja ya CJ Prof. Ibrahim Juma is by passed by events!

1. Utangulizi
Binadamu hatufanani, kuna watu ni wenye bahati, very fortunate, wengine wako kama Midas touch!, everything they touch turns to gold. Mimi ni mmoja wa watu hao very fortunate!. Kati ya Wakuu 3 wa Mihimili yetu 3, ya Serikali Bunge na Mahakama, Wakuu wa Mihimili 2 ni Waalimu wangu!.

2. Mkuu wa Mhimili wa Mahakama, Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, ndiye alikuwa Dean wangu, wakati nikiwa mwanafunzi wa Sheria pale FoL ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, wakati huo akiwa kijana akiwa Dr. Ibrahim Juma.

3. Mkuu wa Mhimili wa Bunge, Spika wa Bunge, Dr. Tulia Akson, ndiye mwalimu wangu wa Kipindi changu cha kwanza, somo la kwanza, siku ya kwanza ya masomo, wakati huo akiwa TA, binti mdogo, sasa ndie Mkuu wa Mhimili wa Bunge Spika wa Bunge

4. Kitendo cha kufundishwa na waalimu wawili,waliokuja kuwa wakuu wa mihimili,sio jambo dogo,wakati wengine wanaogopa kumkabili Jaji Mkuu, CJ,kutokana na uhimili wake,mimi kama mwanafunzi wake,ninaweza kumwambia lolote kwasababu kwangu huyu sio Jaji Mkuu tuu,kwangu mimi, huyu ni yule yule mwalimu wangu na Dean wangu,Dr Ibrahim Juma, pale FoL.

5. The same applies to Dr. Tulia,japo anaheshimika na kuogopwa kwa uhimili wake,kwangu huyu ni yule yule TA aliyenifundisha,hivyo nakuwa niko free kumwambia lolote kama hivi
View: https://youtu.be/ZM_D9HAPi5M?si=yTiMm7f27zM4NhZQ
6. Kitu cha kwanza muhimu kabisa katika taifa lolote ni watu, wananchi ndio wenye nchi na kila kitu kilichomo, wananchi wameweka katiba yao ya jinsi ya kuendesha mambo yao,hivyo ukiondoa watu,wananchi,kitu muhimu cha pili ni katiba,ndio kila kitu!。Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni nini, ya nani, ya kazi gani? Msemo "Katiba ndio kila kitu" Una maana gani? Katiba ina umuhimu gani?
7. Hawa wananchi wenye nchi wameipa katiba ukuu wa kila kitu,hakuna aliye juu ya katiba. Katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote inayokinzana na katiba,inakuwa ni sheria batili!。
8. Katiba ya JMT,imetoa haki mbalimbali za kikatiba,na kisheria za kisiasa,kiuchumi na kijamii.
9. Haki kuu mbili za kisiasa ni haki ya kuchagua na haki ya kuchaguliwa。

10. Haki ya kuchagua inatekelezwa kwa haki ya kupiga kura kwa uhuru wa kuchagua viongozi unaowaoenda kwa mujibu wa ibara ya 5。
11. Haki ya kuchaguliwa inatekelezwa haki ya uhuru wa kugombea nafasi yoyote ya uongozi toka serikali ya mtaa hadi serikali kuu kwa mujibu wa Ibara ya 21 ya katiba.
12. Rais wa JMT, na mihimili yote mitatu ya Serikali,Bunge na Mahakama, ni zao la katiba, na wote wako chini ya katiba,ila wote kwa nyakati tofauti wamekuwa wakijiinua juu ya katiba!。
13. Serikali imekuwa ikitunga miswada batili kinyume na katiba,mmoja wa miswada hiyo ni muswada wa sheria ya uchaguzi iliyopita!Bunge linatimiza wajibu wake kikamilifu utungaji wa Sheria na kuismamia Serikali?. Nani kati Bunge na serikali anayetutungia hizi Sheria Batili?!

14. Bunge likatunga sheria batili,Mhimili wa Mahakama Kuu,inazibatilisha hizo sheria batili,serikali ikagoma。
15。 Serikali ikafanya mabadiliko batili ya katiba,ikauchomekea ubatili huo ndani ya katiba yetu!
16. Mahakama Kuu ikashikilia msimamo,mabadiliko hayo ya katiba ni batili na sheria ya uchaguzi ni batilifu!
17。 Mahakama ya Rufani ikazibariki kwa kujinyenyekeza chini ya mhimili wa Bunge,kulibembeleza Bunge ndio liuondoe ubatili huo!。Niliwahi kuuliza Bunge Letu Kibri na Jeuri ni Bunge Kweli la Kutunga Sheria au ni Bunge Ruber Stemp ya Serikali? Kwanini Linaogopwa Hivi na Mhimili wa Mahakama?
18. Bunge licha ya kuamriwa na mahakama,kuuondoa ubatili huo, haija uondoa ubatili mpaka leo!。Hii maana yake hili ni Bunge kiburi?Bunge letu, Bunge Kibri, Jeuri? Linawezaje kutunga tena Sheria batili? Limeamriwa kuondoa ubatili huo, linapata wapi jeuri ya kuidharau Mahakama?
19. Matokeo yake,katiba yetu bado ina ubatili,sheria mpya ya uchaguzi ina ubatili ule ule ulioshabatilishwa na mahakama!
20. Hata sheria iliyounda Tume Huru ya Uchaguziu,INEC
ni batilifu kwasababu katiba inaitambua Tume ya Uchaguzi NEC.

Hitimisho
Mimi kama mwanafunzi wa Dr Tulia Akson,namuomba mwalimu wangu,kabla ya kuvunjwa kwa Bunge hili,nakuomba mwalimu TA wangu, Tulia Akson,ambaye sasa ni Dk na Spika wa Bunge la JMT,tunaomba Bunge lako lifanye minimum reforms za katiba kuwatendea Watanzania haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwa kuuondoa ule ubatili wa sheria ya uchaguzi,na kuihalalisha INEC!. Kwa lengo la kutanguliza mbele maslahi ya taifa,kuna vitu Bunge linapaswa kuvifanya kuwafanyia Watanzania,na。moja ya vitu hivyo ni kuwatungia sheria za haki na sio Bunge kuendelea kuwa a rubber stamp ya serikali Je, Bunge Litimize Wajibu Wake KikamiliIfu Ikiwemo Kutunga Sheria, Au Liendelee Kuwa "Rubber Stamp" ya Kupitishia Miswada ya Serikali Bila Kuhoji?

Mungu Mbariki Spika Dr Tulia Aweze!

Mungu Libariki Bunge Liweze!

Mungu Ibariki Tanzania。

Paskali
 
Kwa hiyo unatutisha ama?
Ok umefaidi nini kwao🤣
 
Kumbe ndiyo maana ilikuchukua miaka mingi kumaliza hiyo shahada yako ya sheria. Maana walimu wako wote walikuwa ni mamluki kwenye hiyo tasnia ya sheria.

Wewe ulitakiwa kufundishwa sheria na watu kama Tundu Lissu, Peter Kibatala, au Rugemalaza Nshala.
 
Kwa hiyo unatutisha ama?
Ok umefaidi nini kwao🤣
Mtu mkiwa mnajuana,unapata kitu kinachoitwa preferential treatment,huhitaji kufanya appointment kupita kumsalimia mwalimu wako,unafanya walk in appointment kwa PS wake,fulani yupo?,kuna mwanafunzi wake anataka kumsalimia!, ukiisharuhusiwa,huko unasema yote!
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…