Baraza la Mawaziri, sura mpya, uchakachuaji unaendelea

Yaani mnataka kusema mtu aliyetangazwa Rais wiki iliyopita mpaka leo hana orodha kamili ya Baraza lake la Mawaziri?

Probably YES maana nakumbuka ilisemwa baraza litatangazwa last Friday lakini mpaka leo holaaaa!!
 
Yaani mnataka kusema mtu aliyetangazwa Rais wiki iliyopita mpaka leo hana orodha kamili ya Baraza lake la Mawaziri?

Yuko twisheni maana kapata mfadhaiko na shinikizo Chadema walipotoka nje ya Bunge akihutubia Bunge na Taifa!
 
Kuna taarifa kwamba JK amejifungia kuchakachua mapendekezo ya watu wa usalama na washauri wake (sio Sheikh Yahya na Maji Marefu).

Wizara zinazoumiza vichwa ni Mambo ya Nje, Mambo ya Ndani, Fedha na Uchumi, Maliasili na Utalii, Elimu, Afya na Ardhi.

Prof Anna Tibaijuka alitaka kumpa Mambo ya Nje,watu wakasema anafaa ardhi na makazi maana kuwa UN haina mana ni mwanadiplomasia. Hoja hiyo inatokana na Membe kuzidiwa na mizengwe ya kutaka kumtoa, kwa kigezo kile kile cha kumtoa Sitta kwamba eti makundi na wakose yote Membe na Lowassa!!!

Jina la January Makamba nalo liko juu, huku majina mapya ya vijana kibao yakijitokeza, baadhi wakiwa ni kutoka visiwani na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Bado tatizo la ukubwa wa baraza haliepukiki kwa sasa. Ila kwa kweli kundi la mafisadi lina nguvu kubwa kwa CCM na JK anapata shida sana kujitenga na nguvu hizo na sasa zinamtesa sana.

Wizara ya Miundombinu nayo inatakiwa na mafisadi kwa nguvu zote.

More to come from Msoga.

Muda utasema....!
 
Hivi kweli, kwa akili zenu zooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooote, mlitegemea kwamba JK angemuacha swahiba yake, kipenzi chake, msiri wake, mshkaji wake, Januari Makamba? (Mie sipendi kuandika jina lake kwa staili ya kizungu, maana watu wengi washamba siku hizi wanaona uzungu ndio tija! Jina lake ni JANUARI MAKAMBA, jina la Kiswahili. Hiyo JANUARY ni Kiingereza! Kama anataka, ABADILI URAIA!)

Kwa kuwa Jakaya (hili huwezi kulibadilisha kuwa la Kizungu hata kwa DAWA za Mlingotini!) hatamuacha Januari kwenye Baraza la Mawaziri, tusitarajie MABADILIKO yoyote yale ya MAANA na MSINGI kwenye Serikali ya Awamu ya Pili ya Jakaya (ati wengine wanamuita Jah-Kaya! DU!)!

Mambo yatakuwa ufisadi kwa kwenda mbele. Mie nimeshadili na hawa watu.... mnakumbuka lile zoezi la wasanii wa filamu walipotaka kumuona JK wamueleze shida zao? Mnakumbuka ilikuwaje? Mnakumbuka jinsi ile hoja ilivyopotezwa? Siku hizi mambo ni DILI tu, wana-JF! DILI, DILI, DILI na DILI!

Kudadadadadeki!

> Mwana wa Haki

P.S. Mama Mkwe, Meghji, naye atarudi Barazani! Si mnajua kwamba hii ni First Family? LOL
 
...hapo tu kwenye Januari Makamba ndi nahisi kizunguzungu!! atapewa uwaziri kwa kulipa fadhila au? simchukii ila hakuwa mshauri mwema kwa mtawala. Januari Makamba tujiulize aliupataje ubunge kule kwao, Januari Makamba akh! WACHENI LIZAME TUGAWANE MBAO:teeth:
 
Advise: Usiwe hata siku moja uwe na matumaini kutoka kwa mawaziri kama Rais ni mpuuzi, kihiyo, kichwamaji etc. What do you expect from a cabinet while a president is stupid? Mininisters go by orders from the President; a good job is directed by the president! I don't expect anything new from this cabinet even if an angel is appointed a minister!

Another 5 years wasted!!!!

Mnaongelea kufail kwa akina masha na Ngeleja pekee! Hivi mnajua hata Mizengo Pinda ni mzigo kama mnabisha hebu fuatilieni records za mawaziri wakuu waliopita ukianzia Kawawa,Sokoine na waliofuatia kuna vitu walifanya ambavyo mpaka leo they get credits for from the people...yaani Pinda kashindwa kufikia hata kiwango cha utendaji wa Magufuri au hata Lyatonga Mrema...yaani huyu jamaa ni mpuuzi sana tu,kazi yake naye ni kulalamika kama mwananchi wa kawaida hata baada ya kufanya kazi katika awamu zote 4 eti bado hajui nani katuloga na huu umaskini wetu...hovyo kabisa huyu halafu watu nao wanampamba eti ohoo Pinda mtoto wa mkulima while is benefing kutokana na mfumo mbovu
 
Sina shaka na uwezo wa mawaziri wote wa JK akiwamo Masha na Ngeleja, tatizo ni Influence ya mafisadi ktk CCM na serikali


Kama tatizo ni hao mafisadi wa ccm basi hao ndio wameathiri uwezo wa Masha na Ngeleja! Kumbuka huyu Ngeleja alikuwa muajiliwa wa Kampuni ambayo Rostam anainfluence kubwa sana na pia Masha aliwekwa pale mambo ya ndani ili wakubwa waweze kunufaika na commissions [ 10%] watakazolipwa baada ya kupitisha tenda kwa kampuni husika!! Ndio maana nguvu sizizokuwa za kawaida zilizotumika kumtaka Masha arudi bungeni ili kuendeleza juhudi za kutaka kuvila vitambulisho!!
 
Kuna kitu wachumi wanaita "Scale of Preferences" ikiwa na maana orodha ya vitu muhimu. Sasa ukianza na Afya, ukaja Elimu, maji, barabara, ulinzi, n.k. je swala la vitambulisho liko namba ngapi?? Ni Tatizo la mapato tuliyonayo, yako limited kulinganisha na idadi ya matatizo yanayotukumba.. Ngereja Kiwira ulitaka afanyeje?? acha ushabiki hata kwenye mitandao, kubali kusahihishwa

Na scale of preference kwa Wizara ya Mambo ya Ndani sio Elimu wala Afya, NI VITAMBULISHO!
 
Ngeleja ni kati ya mawaziri walioshindwa kabisa katika wizara hiyo. Angalia Sheria Mpya ya Madini ya 2010 iliyopitishwa mwanzoni mwa mwaka huu lakini imeshindwa kutumika mpaka sasa. Ina makosa yasiyo na hesabu, haitekelezeki ndiyo maana wizara yake imeshindwa kutoa 'regulation' mpaka leo. Sasa hivi wanaomba tena wadau mbalimbali kutoa ushauri utakaoweza kusaidia sheria hiyo iweze kufanya kazi bila ya kubadilisha sheria yenyewe kitu ambacho kinaonekana ni kigumu kwa vile baadhi ya mambo yaliyopo katika sheria hiyo ni lazima yabadilishwe ili sheria hiyo iweze kutumika bila kusababisha migogoro katika sekta ya madini.
 
Kuna taarifa kwamba JK amejifungia kuchakachua mapendekezo ya watu wa usalama na washauri wake (sio Sheikh Yahya na Maji Marefu).

Wizara zinazoumiza vichwa ni Mambo ya Nje, Mambo ya Ndani, Fedha na Uchumi, Maliasili na Utalii, Elimu, Afya na Ardhi.

Prof Anna Tibaijuka alitaka kumpa Mambo ya Nje,watu wakasema anafaa ardhi na makazi maana kuwa UN haina mana ni mwanadiplomasia. Hoja hiyo inatokana na Membe kuzidiwa na mizengwe ya kutaka kumtoa, kwa kigezo kile kile cha kumtoa Sitta kwamba eti makundi na wakose yote Membe na Lowassa!!!

Jina la January Makamba nalo liko juu, huku majina mapya ya vijana kibao yakijitokeza, baadhi wakiwa ni kutoka visiwani na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Bado tatizo la ukubwa wa baraza haliepukiki kwa sasa. Ila kwa kweli kundi la mafisadi lina nguvu kubwa kwa CCM na JK anapata shida sana kujitenga na nguvu hizo na sasa zinamtesa sana.

Wizara ya Miundombinu nayo inatakiwa na mafisadi kwa nguvu zote.

More to come from Msoga.

Add a caption
Madarasa yetu haya!!





 
Kuangushwa kwa Masha kule mwanza ni matokeo ya kukimbilia siasa za kitaifa na kuwaacha waliokuchagua juani.

Binafsi muda wote nimekuwa nikiamini kwamba mbunge bora ni yule anayetumia angalau miaka miwili ya kwanza kujijenga jimboni kwake. Akitumia muda huo kusoma changamoto na fursa mbalimbali zilizopo, akiandaa taratibu mbalimbali za namna ya kushughulia matatizo ya wananchi na akianda process nzuri ya uwajibikaji na ambayo anaweza akaitumia hata kama yuko mbali.

Lakini ukitumia ubunge as a stepping stone ya kukimbilia uwaziri bila ya kujali kwamba hayo mawe yamejimbia vya kutosha kiasi kwamba hata ukirudi utayakuta na kuyatumia kuwafikia wananchi basi matokeo yake ndio kama hayo ya Masha. Huyu kijana masha ni katika wabunge wachache ambao walikuwa karibu na nyenzo zote za kuwasaidia kutimiza wajibu wao kwenye majimbo yao, kuanzia elimu, uwezo, connections, exposure nk. Lakini vyote hivyo havifanyi kazi kama huna process in place ya kuhakikisha unajua nini kinatokea jimboni kwako na una uwezo wa kushughulikia matatizo hayo hata kama uko mbali. Kuandaa process kama hiyo sio kazi rahisi na huwezi kuitengeneza kwa kutumia simu maana kule majimboni kuna wasanii na waongo wa kutupwa. Usipokuwa makini kila kitu utakachokuwa unaambiwa ni uwongo tu na ukweli unafichwa pembeni.

Kwahiyo kwa njia moja nakubaliana na anachosema mzee Mwanakijiji kwamba hawa wabunge wafikirie kwanza kujenga misingi yao kule chini kabla ya kukimbilia juu. Lakini kwa TZ kila mtu hajali sana kazi bali power na wengi wako tayari kutumia njia zozote kupata hiyo power.

Ila pia naona mnawapa mafisadi nguvu kubwa ambayo huenda kwa kweli hata hawana. Kila kitu mnakimbilia ni nguvu ya mafisadi wakati ukweli ni uwezo mdogo na tamaa binafsi za wahusika.

Kama mtu ambaye nimeshiriki hizi chaguzi, naweza kusema from my experience kwamba kwa kweli mnawakuza mno hao mafisadi. Madhara ya utendaji mbovu na umimi ni kubwa mno hata kuliko madhara ya ufisadi wa kitaifa. Kwenye halmashauri kuna mabilioni ya pesa zinapotea shauri ya utendaji mbovu na makosa katika usimamizi wakati nguvu zote za magazeti zimeelekezwa kwenye personalities za wanasiasa wa kitaifa.

Ufisadi umeshageuka mtaji wa kisiasa Tanzania huku wananchi maskini wanabaki pale pale walipo bila juhudi za maana za kusaidia ili waondokane na umaskini pamoja na ujinga wa kutisha.

Nashangaa hata mkuu Halisi ambaye namheshimu sana kutokana na michango yake ya huko nyuma naye siku za karibuni ameingia kwenye hizi speculative politics badala ya kujikita kwenye investigative journalism ambayo najua anaiweza sana. Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kugeuka kuwa kama Yahaya bali kwa kukaa chini na kufanya analysis na kujiangalia wenyewe kwanza na kutafakari kwanini makundi mbalimbali ya Watanzania yanapiga mark time pale pale?

Hizi nguvu kubwa sana tunazowapa mafisadi si ajabu wenzetu wana enjoy mno maana hiyo kwao tayari ni source of power. Inaweza ikafika mahali vijana wetu wengi wakaamini hawawezi kufanya jambo lolote bila ya nguvu ya mafisadi. Hiyo ndio hatari ya hizi kelele tunazopiga kila siku hata mahali ambapo hapana ukweli.
 
Lakini kwa nini tunaendeleza upumbavu ule ule wa kudai tuwe na wasomi hata vijana lakini hakuna wanalozalisha? Kama kuna baraza la mawaziri lilikuwa limejaa wasomi ni hili lilokwisha, sasa mjiulize ni vipi wameshindwa kazi. Je ni Usomi, Jinsia, Ukabila, Umri au?

Ufanisi hauna umri, elimu, jinsia, dini wala rangi. Ni ufanisi tuu na hakuna lingine!

Tumetumia miaka miaka mitano kuwajadili hawa mawaziri wako karibu na nani zaidi badala ya kujadili uwezo wao.

Sijaona waziri yeyote ambaye anaweza kusema kashindwa kutimiza kazi zake kwasababu ya kukwamishwa na kundi fulani. Wao wako interested zaidi kujipanga na kundi fulani na kutumia hayo makundi kama mtaji wa kisiasa.

Kwasababu na sisi Watanzania tumejichimbia kwenye makundi hayo hayo basi malengo yao yanafanikiwa.

Mrema kokote alikokuwa anapelekwa alikuwa ana perform. Hata alipopelekwa wizara ya kazi ambako wajanja walifikiri wamemficha asifurukute, bado aligundua kuna uozo na akaanza kuusafisha.

Kwa Tanzania ukiwa mchapa kazi utafanikiwa tu maana kuna kazi nyingi mno za kufanya. Kila ukipita mitaani unaona mambo mengi mno ambayo yanaweza kurekebishwa huku waliokabidhiwa hizo kazi wakiwa hawana habari kabisa. Aliyesema fortune favours the prepared mind hakukosea, watendaji wetu wengi hawako prepared kukabiliana na changamoto za kila siku.
 
Hii yote itategemea na JK kama anania njema na hii nchi. Kama hana nia njema hataweza kusimamia subodinates.

TUSIJIDANGANYE WOTE TUNAFAHAMU KUWA CCM HAINA WATU WASAFI AMBAO WANAWEZA KUKABIDHIWA UWAZIRI WAKAWA WATUMISHI WA WEMA WATANZANIA PASIPO KUJINUFAISHA WAO NA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ZAO TU!

MAENDELEO YA WATANZANIA YAKO MIKONONI MWA JK WALA TUSIANZE KUSINGIZIA WASAIDIZI WAKE.
KAMA BABA WA NYUMBA ANAJUA KUSIMAMIA FAMILIA YAKE VIZURI USTAWI WA FAMILIA HIYO NI DHAHIRI PASIPO SHAKA.

AMINI USIAMINI KAMA USIMAMIZI WA JK UTAKUWA ULEULE WA KIPINDI KILICHOISHA, TUSITEGEMEE ANY CHANGE BALI MAUMIVU TUUUUUUUUUUUUUUU!
 
Nyerererist:Hapana mkuu, mstari wa kwanza una maanisha hivyo, uko wazi kabisa, pia kuna sehemu umemtaja Ngeleja as if naye alishindwa. Point yangu iko pale pale, vijana wapewe nafasi, wazee wa-step down the front offices hasa katika vyama vya siasa na sehem zote zinazoshiriki katika maamuzi ya mstakabali wa taifa letu. Pili, sioni kama Masha na Ngeleja walishindwa kazi, unless mtu anipe vigezo 1,2,3.. kisayansi, sio kihisia. Ndio tunavyoenda siku hizi.. Pia wazee Wameshashindwa, ni wakati wetu vijana kujitawala sio kutawaliwa na mitazamo ya wachache kwa kisingizio cha uzoefu.

Tuanze na CCM,kwani safu nzima ya uongozi inajengwa na wazee. Makamba,Msekwa,Chiligati na Mkwere are all 55+ yrs old! Makinda is also 60+ yrs old! Pinda,katibu wa ikulu...the same narration goes on. Sasa wewe kikweterist (u don't deserve to be nyerererist) unaposema wazee wastep down anza kwa kuishauri serikali ya CCM ianze huu mchakato.
 
Tabia ya makundi na uswahiba yameipeleka pabaya sana CCM, kuna watu (Bashe, Shelukindo nk) wamejeruiwa na bado wana makovu ambayo hawayatasahau katika historia yao ya kisiasa,
Lakini baada ya uchaguzi angalau CCM walijitahidi kujiweka pamoja tena, na watu wakawaona ni wamoja,
Mchakato wa kutafuta Spika wa Bunge kupitia CCM ulikuja kuamsha makundi yaliyoonekana kama yamekufa na Samwel Sitta akajeruwiwa vibaya na Chenge huku CCM ikikaa kimya kana kwamba alichokiongea Chenge kilikuwa ni sahihi, na Mwisho wa siku Spika akapatikana (Makinda) ingawa watu wana imani kidogo na uwezo binafsi wa Spika mteule.

Baraza la Mawaziri ambalo linatarajiwa kutangazwa na JK nadhani ndilo litakalo tuonyesha uwezekano wa CCM kuwepo ama kupotea katika medani za kisiasa za Tanzania, JK ana changamoto kubwa na ngumu mno katika kuchagua Baraza lake la mawaziri,

Ni ukweli usiofichika kuwa ili kuwe na ufanisi na matumizi madogo ya serikali inambidi (JK) achague baraza dogo la watu wachache wenye uwezo na ambao wako committed
matatizo makubwa anayo-face JK katika uteuzi wake ni
1) Kuna Mwaswahiba zake ambao angependa wawepo kwenye baraza (Ngereja, Lowassa, nk)
2) Kuna wale wa shinikizo (January, Mathayo nk)
3) Kuna watendaji (Magufuli, nk)
4) Kuna wa shinikizo la kuepuka makundi (Sitta, Mwandosya, Mwakyembe nk)
5) Kuna kutoka CUF (kuulinda muafaka)
6) Kuna group la wawakilishi kutoka Zanzibar (Nahodha)
7) Kuna chaguo binafsi (Pinda, Megji)

Kwa mtazamo wangu ikiwa JK atashindwa kucheza karata zake vizuri hapo, ndipo unaweza kuwa mwanzo wa mwisho wa CCM
 
It is true Kawambwa as a minister, is a serious disaster!! The only qualification he has so far to deserve a ministerial appointment is his Bagamoyo connection!!
 
25 watajwa Baraza la Mawaziri Send to a friend Saturday, 20 November 2010 20:46 0diggsdigg

Sadick Mtulya
SIKU chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kudokeza ataunda serikali ya watu waadilifu, makini na wachapakazi hodari, wabunge kadhaa wametajwa kuwamo katika baraza jipya la mawaziri linalotarajia kutangazwa hivi karibuni.

Akitoa hotuba ya kuzindua Bunge la Kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, Alhamisi iliyopita, Rais Kikwete alisema ataunda serikali ya watu wachache ambao wataondoa urasimu watakaokuwa karibu na wananchi na kushirikiana vizuri na wabunge wote bila kujali vyama vya siasa wanavyotoka.

Vyanzo vyetu vya kuaminika, vimeeleza kuwa mbali na sifa alizodekeza Rais Kikwete katika kuteua mawaziri pia amezingatia umri, uzoefu pamoja na uwiano wa mikoa.

“Pamoja na mambo mengine baraza jipya la mawaziri litakuwa na watu wapya, wakongwe pamoja na idadi ya wanawake kuongeza,’’ kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kimemtaja wabunge wanataria kuwmeo kwenye serikali mpya ya Rais Kikwete na majimbo wanayotoka katika mabano kuwa ni Samuel Sitta(Urambo Mashariki) ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dk Harrison Mwakyembe (Kyela), Anne Kilango (Same Mashariki), Januari Makamba (Bumbuli) ambaye alikuwa Msaidizi wa Rais Ikulu katika awamu ya kwanza ya utawala wa Rais Kikwete.

Wengine ni Bernard Membe (Mtama) ambaye katika serikali iliyopita alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa na Emmanuel Nchimbi (Songea Mjini) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Mawaziri wengine waliokua katika Serikali iliyopita wanaotajwa kurejeshwa katika kipindi hiki cha mwisho cha utawala wa Kikwete ni Ezikeil Maige (Msalala) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Wiliam Ngeleja (Sengerema) aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini na Adamu Malima (Mkuranga) aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na madini.

Chanzo chetu kimetajwa pia Celina Kombani (Ulanga Mashariki) ambaye alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Profesa Juma Kapuya (Urambo Magharibi), aliyekuwa Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Christopher Chiza (Buyungu) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika.

Wengine ni Profesa Mark Mwandosya (Rungwe Mashariki), ambaye alikuwa Waziri Maji na Umwagiliaji, Dk Hussein Mwinyi(Kwahani), aliykuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Shukuru Kawambwa (Bagamoyo), aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na John Magufuli (Chato) ambaye alikuwa Waziri wa Maendeleo Mifugo na Uvuvi.

Wabunge wanaotajwa kuingia katika baraza la mawaziri kwa mara ya kwanza ni Anna Tibaijuka (Muleba Kusini), Salehe Pamba (Pangani), Steven Masele (Shinyanga Mjini), Gerson Lwenge(Njombe Magharibi) na Nyambari Nyangwine (Tarime).

Wengine Shamsi Vuai Nahodha (Mbunge kuteuliwa) na alikuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Angela Mkwizu (Viti Maalum) na Amos Makala(Mvomelo) ambaye ni Mweka Hazina wa CCM, Said Bwanamdogo (Chalinze), Lazaro Nyarandu (Singinda Kaskazini).

Chanzo hicho kimebainisha kuwa Rais Kikwete amedhamiria kuunda baraza dogo la mawaziri litakalo kuwa na tija ikilinganishwa na alilounda wakati akiingia madarakani mwaka 2005, ambalo alilivunja Februari 2008 lilolokuwa na jumla ya mawaziri 60.

Rais Kikwete alilivunja baraza hilo kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kutokana na kashfa ya zbuni tata ya kufuaji umeme wa dharura iliyotolewa kwa kampuni ya Richmond.

Hata hivyo, baraza jipya aliloliunda baadaye chini ya Waziri Mkuu mpya, Mizengo Pinda lilikuwa na mawaziri 27 na manaibu mawaziri 21.

Kati ya mawaziri hao wapo walioanguka katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM na wengine waliangushwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Sasa wabunge hao wanasubiri huruma ya kuteuliwa na rais katika nafasi kumi ambazo tatu amekwisha zijaza kwa kumteua aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa zamani wa Fedha, Zakia Meghji na Profesa Makame Mnyaa Mbarawa.

Walioanguka katika uchaguzi ni mawaziri watano na manaibu wane, wawili kati yao walishindwa kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM na wengine saba wakikumbwa na kimbunga cha Uchaguzi Mkuu kwa kubwagwa na wagombea wa vyama vya upinzani.

Mawaziri walioshindwa kutetea viti vyao vya ubunge ni Dk Batilda Burian, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) ambaye alipigwa kumbo na mgombea wa Chadema kwenye Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema.

Mwingine ni Lawrence Masha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, yeye alishindwa kutetea kiti chake mkoani Mwanza katika Jimbo la Nyamagana alipoangushwa na mgombea wa Chadema, Ezekiel Wenje.

Katika kundi hilo yumo mwanasiasa mkongwe Philip Marmo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbulu mkoani Manyara kwa miaka mingi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), ambaye aliangushwa na mgombea wa Chadema.

Shamsa Mwangunga, ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Diodorus Kamara aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na mbunge wa Jimbo la Nkenge, walioanguka katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.

Kwa upande wa manaibu walioanguka katika uchaguzi huo ni Mwantunu Mahiza ambaye alikuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Aisha Kigoda, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Joel Bendera Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk James Wanyancha ambaye alikuwa Naibu Wazara wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Wakuu wa mikoa ambao walikuwa pia wabunge walioanguka ni Mohamed Abdul Azizi (Iringa) ambaye alishindwa kutetea jimbo lake la Lindi Mjini kwa kuangushwa na mgombea wa CUF na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbega aliyeangushwa na mgombea wa Chadema katikaJimbo la Iringa Mjini.

Uchaguzi wa safari hii pia uliwatupilia mbali wabunge wakongwe akiwamo Getrude Mongela ambaye aliwahi kuwa waziri kwenye serikali ya awamu ya kwanza na kushika nafasi mbalimbali kwenye taasisi za kimataifa. Pia aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Afrika. Katika uchaguzi wa mwaka huu aliangushwa na mgombea kutoka Chadema katika jimbo la Ukerewe.

Wengine waliwahi kuwa mawaziri ambo hawakurudi bungeni ni Anthony Diallo aliyewahi kuwa Waziri wa Biashara na Viwanda), Kilontsi Mporogomyi (Naibu, Afya na Ustawi wa Jamii), Lucas Siame (Naibu, Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu), Nazir Karamagi (Waziri, Nishati na Madini) na Ibrahim Msabaha (Waziri, Ushirikiano wa Afrika Mashariki).


source :mwananchi
 
Back
Top Bottom