Baraza la Mawaziri, sura mpya, uchakachuaji unaendelea

Napingana na Mtazamo wa mwanakijiji

Mie binafsi sijaona kama Ngeleja na Masha walishindwa kazi,, kwa sayinsi ipi uliyotumia mwanakijiji?? Hizo analysis za kizamani za kujudge mtu kwa kuangalia mvuto wake wa kuongea na vyombo vya habari na umma kwa ujumla. Mie nadhani Masha na Ngeleja walifanya kazi vizuri sana na hukukutokea matatizo yoyote yaliyosababishwa na wao,, hizo judgement za hisia kwa vile mtu haumpendi binafsi sio nzuri.

Tukikubaliana na analysis, hisia na mtazamo wako, basi Kina David cameron, kina Obama, Kina Nick Craig, Ed Milliband, n.k n.k ni wabovu. Kitu ambacho utakipinga kwa sababu hao unapata information na utendaji wao ki-sayansi na kimahesabu. sio ki hisia. mambo ya kizamani. Vijana ni muhimu na wacha wapewe wachape kazi. Wazee wabaki kua consultants tu. Na hii pia iende mpaka CHADEMA, CCM, TLP, NCCR n.k maana kuna majina tumekua tukiyasikia yapata miaka 20 na hayajatusaidia chochote badala yake wamegeuza siasa biashara. Ni wakati wa Dr Slaa, Mrema, Msekwa, Mbowe, Kihwelu, Mbatia, Marando, Lipumba, safari, nk wote hawa they have to step out of the front offices of our political parties. Ni wakati wa siasa na uongozi kwa ujumla kuachiwa vijana ambao wanaonyesha wanaweza.

Mitizamo na uongozi mpya ndio kitu tanzania inachohitaji. Sio kuendeleza siasa na mitazamo ile ile ambayo imekua ikitumiwa kwa miaka 50. Eti wazee, ooh Uzoefu. Obama, Cameron, Tony Blair, walikua na uzoefu gani?? Kwa bahati mbaya sana falsafa hii imedakwa na kukumbatiwa na vyama vyote vya siasa. Kuanzia CHADEMA hadi TADEA, wote wanaendekeza mawazo mabovu yaliyojaa ubabe wa kizee.

Its time waachie hizo kazi, zimeshawashinda kwa miongo kibao. Tena kwa kutoa mfano, napendekeza aanze Dr Slaa ambaye amekua katibu wa CHADEMA karibia miaka 200 iliyopita. Kila siku ubabe na kufukuza vijana wanaoleta mitazamo mipya au wanaopingana nae.
 
JK atafanya kosa kubwa sana kuwapa vijana wanaoingia Bungeni kwa mara ya kwanza uwaziri au Unaibu Waziri kama alivyofanya kwa Masha. Mimi binafsi ninaamini ni muhimu kuwaacha vijana hawa wajijenge kama wabunge kwanza kwa karibu miaka miwili hivi kitu ambacho Masha alinyimwa kwa kweli. Lakini hatari zaidi naamini kuwa madaraka makubwa kama uwaziri yanakuja na kile kinachoitwa "trappings of power".. na ina hatari sana ya kuwaharibu.. tumeona ya Ngeleja. Waacheni wajijenge kama viongozi wa kisiasa, waacheni waweze kuconnect na wananchi, kujifunza vurugu za Bungeni n.k

Ninaamini, kinyume na wengine wanavyoaamini binafsi ninaamini tatizo la serikali iliyopita halikuwa kwenye umri (wazee vs vijana). Ninaamini ni tatizo la uwezo. Hivyo, licha ya hilo nililolisema hapo juu ni muhimu kupima viongozi wanaokuja kwa kuangalia uwezo. Uwezo hauji kwa sababu ya elimu tu bali unakuja kutokana na uzoefu wa muda mrefu, uthabiti wa kushughulikia maatizo, ubunifu na maono yaliyo nje ya sanduku la yale yaliyozoelekea. Hivyo, hana budi kurudi nyuma na kuangalia uwezo kuliko majina na umri.

Sasa hivi hana udhuru tena "wa sikufahamu" na hatakuwa na udhuru wa kuwa "tunajaribu". Ni lazima apange kikosi kinachoenda kufanya kazi na siyo kitakachoonesha malipo ya kisiasa. Na hapa ninaamini ni bora arudishe baraza la wakongwe walioonesha uwezo kuliko kuingiza baraza la vijana ambalo halijawahi kujaribiwa hasa ukizingatia changamoto za taifa letu.

Pamoja na hilo, safari hii tunakokwenda Watanzania hawatawalalamikia tena "wasaidizi wake" kama walivyofanya miaka hii mitano; huko mbeleni wateule wake wakianza kuboronga guess nani atabebeshwa lawama squarely?

JK amepata fursa nyingine adimu ya kuamua kufanya tofauti. Bado ngwe hii ya lala salama anaweza kuonyesha tofauti kubwa na ngwe iliyopita kama ataamua kwa dhati kubadili mfumo mzima wa namna alivyounda timu ya wasaidizi wake. Wengi walikuwa kama hawajui wanalolifanya vile.
Kwa watu wacha Mungu, wanaoogopa matokeo ya matendo mabaya wanayofanya, fursa kama hii huwa wanajifungia ndani wakitafakari kwa umakini nini cha kufanya huku wakikesha wakiomba hekima ya kimungu inawaonyeshe mambo sahihi ya kufanya. Kama msaada ni wa mafisadi guess what???? Itakuwa ni fursa ya kujifungia na kutengeneza kikosi kazi cha maangamizi. Well, kila mtu anautashi wa kuamua nini cha kufanya!!!
 
Sijasema hata mahali pamoja kuwa Masha na Ngeleja walishindwa kazi.. au kusema walifanya kazi vizuri...
 
Hapana mkuu, mstari wa kwanza una maanisha hivyo, uko wazi kabisa, pia kuna sehemu umemtaja Ngeleja as if naye alishindwa. Point yangu iko pale pale, vijana wapewe nafasi, wazee wa-step down the front offices hasa katika vyama vya siasa na sehem zote zinazoshiriki katika maamuzi ya mstakabali wa taifa letu. Pili, sioni kama Masha na Ngeleja walishindwa kazi, unless mtu anipe vigezo 1,2,3.. kisayansi, sio kihisia. Ndio tunavyoenda siku hizi.. Pia wazee Wameshashindwa, ni wakati wetu vijana kujitawala sio kutawaliwa na mitazamo ya wachache kwa kisingizio cha uzoefu.
 
Masha vitambulisho na tamithilia zote zinazohusu huo mradi na kadhalika mengine utaongeza na Ngeleja ngonjera za Kiwira zisizokwisha... Kwa hayo yote google 'Masha vitambulisho' na 'Ngeleja Kiwira' unambie wapi wametunisha misuli kama vijana na kama si kuimba nyimbo zile zile za waliowafikisha hapo walipo. Wote naamini wanaweza kama wakiwa huru, lkn hawana uhuru, afadhali ya January Makamba, hawezi kuburuzwa na Yusuf Makamba kwa kuwa unaweza kumkatalia baba yako lkn si aliyekuweka kwa maslahi (mjadala ni mpana).
 
Ndio maana nikasema hapo awali tusijudge watu kwa hisia kama ulivyofanya. Nakushauri uanze kwa kutafuta nini hasa kinakwamisha hivyo vitambulisho visitoke kama ilivyo ahidiwa?? tuache kua tunachukua quote ndogo ndogo namna hiyo halafu tuna-draw conclusion hapo hapo. Miradi kama hiyo inainvolve mamilioni ya hela, kama hela zipo na masha ameshindwa kupiga sign tu hapo ndio unaweza kuniambia kwamba ameshindwa. Lakini kama hela za mradi inabidi zitafutwe na kisha ziidhinishwe kwa kufuata maoni ya wataalamu basi sioni hapo Masha unamuweka wapi.

Kuna kitu wachumi wanaita "Scale of Preferences" ikiwa na maana orodha ya vitu muhimu. Sasa ukianza na Afya, ukaja Elimu, maji, barabara, ulinzi, n.k. je swala la vitambulisho liko namba ngapi?? Ni Tatizo la mapato tuliyonayo, yako limited kulinganisha na idadi ya matatizo yanayotukumba.. Ngereja Kiwira ulitaka afanyeje?? acha ushabiki hata kwenye mitandao, kubali kusahihishwa
 
Sijasema hata mahali pamoja kuwa Masha na Ngeleja walishindwa kazi.. au kusema walifanya kazi vizuri...
<br />
<br />
MM,

Ukiondoa tatizo la mafisadi jingine linalotuumiza ni wakongwe! Wazee lazima wawe na muda wa kusema basi kuna vichwa(vijana) kibao na wanauwezo wa kupambanua mambo

Wanikumbusha ule msemo wa 'experience??' Niliulizwa baada ya kunaliza skuli unaipata wapi experience bila kupewa nafasi?

Kweli hakuna wenye uwezo zaidi ya wale wale? Zakhia n.k?

It high time waanzishe baraza la wazee watumbukize wazee wote huko no matter chama gani wametoka!!

Ubunge, uwazir waachiwe vijana wanaochipukia?
 
Ndio maana nikasema hapo awali tusijudge watu kwa hisia kama ulivyofanya. Nakushauri uanze kwa kutafuta nini hasa kinakwamisha hivyo vitambulisho visitoke kama ilivyo ahidiwa?? tuache kua tunachukua quote ndogo ndogo namna hiyo halafu tuna-draw conclusion hapo hapo. Miradi kama hiyo inainvolve mamilioni ya hela, kama hela zipo na masha ameshindwa kupiga sign tu hapo ndio unaweza kuniambia kwamba ameshindwa. Lakini kama hela za mradi inabidi zitafutwe na kisha ziidhinishwe kwa kufuata maoni ya wataalamu basi sioni hapo Masha unamuweka wapi.

Kuna kitu wachumi wanaita "Scale of Preferences" ikiwa na maana orodha ya vitu muhimu. Sasa ukianza na Afya, ukaja Elimu, maji, barabara, ulinzi, n.k. je swala la vitambulisho liko namba ngapi?? Ni Tatizo la mapato tuliyonayo, yako limited kulinganisha na idadi ya matatizo yanayotukumba.. Ngereja Kiwira ulitaka afanyeje?? acha ushabiki hata kwenye mitandao, kubali kusahihishwa
lakini hao unao wasema akina ed milliband walianzia mahali, yaani walikuwa kama wabeba jezi wa brown na blair, kwa hiyo walijufunza toka kutengeneza sera/policy na shughuli za chama mashinanimikiki ya bunge na shughuli, sasa hawa wenzetu walianzia wapi mchezo wa siasa. matokeo yake wana kosa indepence katika maamuzi yao, ukiwa na experience unaweza kumkatalia mtu bila kistaarabu, lakini hawa wa sasa hawa wakwetu wana shindwa kuwaambia no walio waweka hata kama shimo wanaliona.
 
Ndio maana nikasema hapo awali tusijudge watu kwa hisia kama ulivyofanya. Nakushauri uanze kwa kutafuta nini hasa kinakwamisha hivyo vitambulisho visitoke kama ilivyo ahidiwa?? tuache kua tunachukua quote ndogo ndogo namna hiyo halafu tuna-draw conclusion hapo hapo. Miradi kama hiyo inainvolve mamilioni ya hela, kama hela zipo na masha ameshindwa kupiga sign tu hapo ndio unaweza kuniambia kwamba ameshindwa. Lakini kama hela za mradi inabidi zitafutwe na kisha ziidhinishwe kwa kufuata maoni ya wataalamu basi sioni hapo Masha unamuweka wapi.

Kuna kitu wachumi wanaita "Scale of Preferences" ikiwa na maana orodha ya vitu muhimu. Sasa ukianza na Afya, ukaja Elimu, maji, barabara, ulinzi, n.k. je swala la vitambulisho liko namba ngapi?? Ni Tatizo la mapato tuliyonayo, yako limited kulinganisha na idadi ya matatizo yanayotukumba.. Ngereja Kiwira ulitaka afanyeje?? acha ushabiki hata kwenye mitandao, kubali kusahihishwa

Pole sana. Ungesoma nilivyokwambia usome usingejibu ulivyojibu. Pole sana. Hujui hata Kiwira kuna nini na Ngeleja kama Waziri Kijana alitakiwa kuwa bold kwa maslahi ya Taifa,kuna maamuzi na yeye alitoa ahadi bungeni hadi leo kimya. Masha nakushauri usome topic zote zinahusu Masha na vitambulisho, then ndio useme kwa kutumia facts. Jaribu kuwa makini na mkweli mbele ya Mungu wako utajua Masha na Ngeleja wako kwa maslahi ya nani na kwann hawatumii elimu na uwezo wao kusaidia nchi na si watu wao?
 
Ndio maana nikasema hapo awali tusijudge watu kwa hisia kama ulivyofanya. Nakushauri uanze kwa kutafuta nini hasa kinakwamisha hivyo vitambulisho visitoke kama ilivyo ahidiwa?? tuache kua tunachukua quote ndogo ndogo namna hiyo halafu tuna-draw conclusion hapo hapo. Miradi kama hiyo inainvolve mamilioni ya hela, kama hela zipo na masha ameshindwa kupiga sign tu hapo ndio unaweza kuniambia kwamba ameshindwa. Lakini kama hela za mradi inabidi zitafutwe na kisha ziidhinishwe kwa kufuata maoni ya wataalamu basi sioni hapo Masha unamuweka wapi.

Kuna kitu wachumi wanaita "Scale of Preferences" ikiwa na maana orodha ya vitu muhimu. Sasa ukianza na Afya, ukaja Elimu, maji, barabara, ulinzi, n.k. je swala la vitambulisho liko namba ngapi?? Ni Tatizo la mapato tuliyonayo, yako limited kulinganisha na idadi ya matatizo yanayotukumba.. Ngereja Kiwira ulitaka afanyeje?? acha ushabiki hata kwenye mitandao, kubali kusahihishwa

…

www.tzlivenews.com/index.php
 
JK atafanya kosa kubwa sana kuwapa vijana wanaoingia Bungeni kwa mara ya kwanza uwaziri au Unaibu Waziri kama alivyofanya kwa Masha. Mimi binafsi ninaamini ni muhimu kuwaacha vijana hawa wajijenge kama wabunge kwanza kwa karibu miaka miwili hivi kitu ambacho Masha alinyimwa kwa kweli. Lakini hatari zaidi naamini kuwa madaraka makubwa kama uwaziri yanakuja na kile kinachoitwa "trappings of power".. na ina hatari sana ya kuwaharibu.. tumeona ya Ngeleja. Waacheni wajijenge kama viongozi wa kisiasa, waacheni waweze kuconnect na wananchi, kujifunza vurugu za Bungeni n.k

Ninaamini, kinyume na wengine wanavyoaamini binafsi ninaamini tatizo la serikali iliyopita halikuwa kwenye umri (wazee vs vijana). Ninaamini ni tatizo la uwezo. Hivyo, licha ya hilo nililolisema hapo juu ni muhimu kupima viongozi wanaokuja kwa kuangalia uwezo. Uwezo hauji kwa sababu ya elimu tu bali unakuja kutokana na uzoefu wa muda mrefu, uthabiti wa kushughulikia maatizo, ubunifu na maono yaliyo nje ya sanduku la yale yaliyozoelekea. Hivyo, hana budi kurudi nyuma na kuangalia uwezo kuliko majina na umri.

........

Mwanakijiji sidhani kama tatizo la Masha au Ngeleja au Kijana yeyote lilitokana na in experince yao ya siasa. Nitakubaliana na wewe ukisema Masha na Ngeleja walikuwa hawana experince ya kusafisha siasa na maamuzi mabovu yaonekane kama ni maamuzi mazuri machoni pa jamii.

Kusimamia Haki, Maadili ukweli na Uzalendo hakuitaji experince . Kusimamia na kuongoza opposite yake ndio kunaweza kuhitaji experince. Hata Huyo Mama Tibaijuka Hiyo wizaraya ardhi hawezi kupewa kwa hofu ya kuwaumbua Vigogo wengi. Ataishia kupewa Wizara ya Jinsia
 
Tetesi Kutoka vyanzo vya kuaminika zinasema kuna karatasi yenye majina ya mawaziri iliyotumiwa na kikao kizito cha watu saba wakiwemo JK, GB na MP kwa ajili ya kuyajadili imeonekana kuna jina la Zitto Zuberi Kabwe katika unaibu waziri wa Fedha na Uchumi.

Ilikuwa tuitoe hii habari tangu jana lakini imebidi tuhakikishe kuwa aliyetuvujishia yuko salama....wanaoelewa itifaki wataelewa na hili.
 
sasa tufanyeje???? umbeya unatuhusu??? subiri uone..... usile maharage ili uchafue hewa
 
Mwanakijiji sidhani kama tatizo la Masha au Ngeleja au Kijana yeyote lilitokana na in experince yao ya siasa. Nitakubaliana na wewe ukisema Masha na Ngeleja walikuwa hawana experince ya kusafisha siasa na maamuzi mabovu yaonekane kama ni maamuzi mazuri machoni pa jamii.

Kusimamia Haki, Maadili ukweli na Uzalendo hakuitaji experince . Kusimamia na kuongoza opposite yake ndio kunaweza kuhitaji experince. Hata Huyo Mama Tibaijuka Hiyo wizaraya ardhi hawezi kupewa kwa hofu ya kuwaumbua Vigogo wengi. Ataishia kupewa Wizara ya Jinsia

Sina shaka na uwezo wa mawaziri wote wa JK akiwamo Masha na Ngeleja, tatizo ni Influence ya mafisadi ktk CCM na serikali
 
Halisi,
Hapo umegonga msumari kichwani. Hawa wote walikuwa ni wawakilishi wa mafisadi.
 
Msimamo wa CDM ni kukataa uteuzi wowote wa KJ kwa kuwa hawamtambui km rais.

Ila Dogo km atavuta ulaji basi CDM itakuwa imepata majibu "who is HE".

Tusubiri tuone
 
Kuna taarifa kwamba JK amejifungia kuchakachua mapendekezo ya watu wa usalama na washauri wake (sio Sheikh Yahya na Maji Marefu).

Wizara zinazoumiza vichwa ni Mambo ya Nje, Mambo ya Ndani, Fedha na Uchumi, Maliasili na Utalii, Elimu, Afya na Ardhi.

Prof Anna Tibaijuka alitaka kumpa Mambo ya Nje,watu wakasema anafaa ardhi na makazi maana kuwa UN haina mana ni mwanadiplomasia. Hoja hiyo inatokana na Membe kuzidiwa na mizengwe ya kutaka kumtoa, kwa kigezo kile kile cha kumtoa Sitta kwamba eti makundi na wakose yote Membe na Lowassa!!!

Jina la January Makamba nalo liko juu, huku majina mapya ya vijana kibao yakijitokeza, baadhi wakiwa ni kutoka visiwani na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Bado tatizo la ukubwa wa baraza haliepukiki kwa sasa. Ila kwa kweli kundi la mafisadi lina nguvu kubwa kwa CCM na JK anapata shida sana kujitenga na nguvu hizo na sasa zinamtesa sana.

Wizara ya Miundombinu nayo inatakiwa na mafisadi kwa nguvu zote.

More to come from Msoga.

Unaweka Title ya maana halafu habari zinakuwa za kizushi unaongea habari za pillow talk, umejuwaje undani wa huyo Mkwere?, acheni majungu bana,
 
Back
Top Bottom