macho_mdiliko
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 21,777
- 39,562
endeleeni kutumaini.....pandeni chelewa mtegemee itageuka kuwa mnazi... keep on hoping....Ni matarajio yetu ya kuwa JK kesho anateua baraza la mawaziri.....tutumie mwanya huo kuhoji yafuatayo:-
a) kila sura kwenye baraza hilo ina sifa hizi................
Uadilifu.............Watuhumiwa wangapi wa wizi na ubadhilifu wamo humo?............
Uchapakazi............Historia yao kiutendaji ikoje vile......................
Kama kuna uhusiano kati ya taaluma ya wizara husika na sifa za mteule...............
Uwiano wa wanaumme na wanawake.........Unarandana na sura ya utaifa iliyopo au kuna upande uliopendelewa...hususani katika ugawaji wa wizara nyeti kama vile Miundo mbinu, Fedha, Mambo ya nje, Elimu...n.k...................
Uwiano wa vikongwe na vijana.................na hapa ni muhimu tukafafanua kijana ana umri gani?
Uwiano kati ya wazenji na wabara una uhusiano wowote ule na idadi za watu kwenye maeneo hayo.....................au kuna upande ambao unapendelewa kwa sabau za kuwafurahisha kisiasa tu...................
Uwiano wa wale waliowahi kuwa mawaziri na wale ambao uteuzi wao ni wa mara ya kwanza..................Kuona hili baraza la mawaziri ni jipya kiasi gani?......
Kwa vile JK amekuwa akilia sana na udini tuone mgawanyo wa wizara alivyowapangia kulingana na dini zao.................Dini ipi imetoa mawaziri wengi zaidi....na kwa sababu zipi.......
Mikoa ambayo inasadikiwa kuwa ilimchagua Dr. Slaa........je .... JK ameishughulikia ki vipi.................Mikoa hiyo ni kumi nayo ni.......Dar, Arusha Mwanza, Iringa, Shinyanga, Mbeya, Kilimanjaro, Kagera, Mara na Manyara....................Je JK kawalipiza visasi wakaazi wa mikoa hiyo kwa kutomchagua au kawatendea ubinadamu?
Baada ya uchambuzi huu na mwingineo muonao unafaa basi tutakuwa kwenye nafasi ya kufahamu kama JK ni mkweli wa kuoanisha kauli zake na matendo au ni mtaalamu wa unafiki tu...........