Nurdin said
Member
- Jan 12, 2014
- 29
- 3
tusubiri hivi wanatangaza saa ngapi
Kuna kila dalili kwamba mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri yapo njiani. Hii ni kwasababu sio tu kwamba upinzani na umma umekuwa ukilalamika kwa muda mrefu juu ya ubabaishaji wa mawaziri kadhaa kiutendaji, bali sasa kilio hiki kimeingia hadi ndani ya chama Tawala ambapo watendaji wake wakuu (kinana na nape) wametamka waziwazi juu ya umuhimu wa kufanyika kwa mabadiliko.
Iwapo Rais Kikwete atafanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri, hii baraza husika litakuwa ni kama la tano tangia aingie Ikulu. Kwa maana hii, na kwa kuzingatia kwamba mabadiliko haya yatakuwa ni ya mwisho kabla ya uchaguzi mkuu 2015, ni dhahiri kwamba selection ya mawaziri itafanywa kwa ustadi mkubwa ili kurudisha imani ya wananchi kwa serikali ya ccm, lakini hasa ili kutekeleza kauli za Kinana mikoani kwamba sasa ni wakati wa serikali ya ccm kurudi katika mstari na kuanza kutekeleza sera zake kwa vitendo.
Ingekuwa wewe ni Rais au mshauri wa Rais, je ungependekeza:
*Nani abaki, Nani atoke, na nani aingie?
*Je, kwa hoja zipi ambazo ni nje ya ushabiki wa kisiasa?
*Je, nje ya mabadiliko ya baraza la mawaziri, nini kingine inatakiwa kifanyike ili kuwezesha mawaziri watakaoteuliwa wawewe deliver katika kipindi kilichobakia kuelekea 2015? Je, sera na mikakati iliyopo ni mizuri, kinachokosekana ni usimamizi na utekelezaji? Je, kuna haja ya kubadili sera, mfumo na mikakati? Kama ipo haja, ni mfumo, sera na mikakati ipi ina mapungufu na ambayo haitasaidia sana mawaziri wapya kuboresha performance ya serikali katika kuhudumia wananchi?
Matarajio ya uzi huu ni mchango wa hoja zinazolenga kujenga, sio kubomoa kwa mujibu wa muktadha uliowasilishwa hapo juu, na mchango wa aina hiyo utathaminiwa sana. Isitoshe, hauwezi jua, pengine consistency ya hoja zenye kujenga zita influence mamlaka ya uteuzi baada ya sauti zetu wananchi kusikika ngazi husika. Mawaziri hawa wataenda kuendesha serikali kupitia kodi tunazolipa sasa na kwenda mbele, hivyo hata kama tumechoshwa na ubabaishaji wa viongozi, basi angalau tufanikishe kodi zetu zifanye kazi kwa ufanisi kwa kipindi kilichobakia, kabla ya kutumia haki zetu za kikatiba kwa ukamilifu kwa kuchagua viongozi wanao ona wanafaa, na kwa wale watakaoamua kwenda mbali zaidi, kuchagua chama cha siasa wanacho ona kinafaa, 2015.
Pengine kwa nia ya kuchokoza mada, nitaje watu watano ambao ningeshauri Rais Kikwete awape wizara zifuatazo:
1. John Magufuli - Waziri Mkuu. Kama alivyobainisha david kafulila bungeni, wa sasa hatoshi kwani ni mpole mno, hivyo mawaziri wanampuuza na kumdharau. Kafulila anasema kwamba anahitajika waziri mkuu mwenye uwezo na mwenye ushawishi au atakayeogopwa na mawaziri pamoja na watendaji serikalini. Kuogopwa sio sifa ya uongozi lakini kama itasaidia kunyoosha utendaji serikalini, kama anavyosema Kafulila, ni bora kuwa basi na waziri mkuu anayeogopwa iwapo hatopatikana waziri mkuu mwenye ushawishi na mwenye uwezo wa kutekeleza sera, maazimio ya bunge, ahadi za serikali bungeni, na kusimamia sheria. Magufuli anatosha kote - katika kusimamia sera, maamuzi ya bunge, sheria, lakini pia utendaji wake utawajaza woga viongozi legelege.
2.Mark Mwandosya - Nishati Na Madini kwa sababu ana uzoefu na hili akianzia kama kamishna wa nishati, katibu mkuu wizara ya nishati, mwanzilishi wa taasisi ya utafiti wa masuala ya nishati na mazingira inayotambulika kinataifa (CEEST), na ame publish tafiti nyingi sana zinazotumiwa ndani na nje ya nchi.
3. Samuel Sitta - Waziri wa Sheria na Katiba. Huyu ni mtaalamu wa sheria, amewahi kuwa waziri hapa awamu ya pili, na ameonyesha uwezo na nia ya kusimamia haki na sheria kupitia uspika na katika jamii kwa ujumla. Mtu wa aina hii atatusaidia kutupatia katiba bora na sio bora katiba.
4. Edward Lowassa - hapa, Rais aiondoe TAMISEMI kutoka ofisi ya waziri mkuu na badala yake ijitegemee kama wizara. Lowassa anaweza rekebisha mapungufu yaliyopo katika wizara hii nyeti inayogusa wananchi wengi kuliko wizara yoyote. Alionyesha uwezo mkubwa akiwa ardhi, na baadae maji, na kujizolea sifa nyingi za uchapa kazi pamoja na mrema awamu ya pili.
5. Anna Tibaijuka - Wizara ya fedha. Huyu ni professor wa uchumi mwenye uzoefu na uwezo unaotambulika, hivyo sina haja ya kumjadili kwa kirefu.
6. Professor Hassa Mlawa - mkuu wa kitengo cha IDS UDSM, amteue ubunge na kumpa wizara ya sayansi, mawasiliano na tekinolojia. Mlawa ni msomi na mtaalamu katika masuala ya innovation, science and technology, hasa roles za haya katika industrialization, na anaheshimika kimataifa katika utafiti wa maeneo haya. Moja ya vikwazo vikubwa vya kuendelea kiuchumi nchini ni nchi yetu kukosa msingi ya kutuwezesha kuwa na uwezo wa ushindani katika uchumi wa sasa wa dunia ambao upo more knowledge driven.
Hawa ni wachache ambao naamini watabadili sana sura ya serikali, hasa katika maeneo hayo. Nje ya kuteua watu wenye uwezo na sifa za kutosha, kuna haja ya kuangalia tena sera, mfumo na mikakati iliyopo ili kuongeza ufanisi katika utendaji serikalini. Tutayaangalia haya baadae.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mchambuzi swali lako hili kwa DK,, binafsi naungana nae kwa kilio cha mfumo [tumezoe SYSTEM].Nitajibu kwa upande wangu mimi kama ifuatavyo.Mh. Ndungulile, unaweza kufafanua kidogo juu ya suala hili muhimu la 'mfumo", hasa kuliweka vyema katika muktadha wake? Mfumo wa chama tawala au mfumo wa utawala wa nchi?

MKURUGENZI wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,MUWSA
mhandisi Cyprian Luhemeja amejikuta akiingizwa katika masuala ya
kisiasa bila ya kujua baada ya viongozi wa chama cha Mapinduzi (CCM)
kudaiwa kuugeuza uzinduzi wa mradi wa maji wa Kiboriloni kama kete ya
kisiasa kuelekea uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo.
Kata ya Kiboriloni iliachwa wazi mwishoni mwa mwaka jana baada ya
Diwani wake, Vincent Rimoy (Chadema) ambaye pia alikuwa Naibu Meya wa
Manispaa ya Moshi kufariki dunia.Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
ilitangaza chaguzi ndogo zitafanyika mwezi Februari mwaka huu.
Kutokana na hali hiyo viongozi wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro
walishtukia mchezo huo na kulazimika kwenda eneo la Mnazi mmoja ambako
kulifanyika uzinduzi licha ya kwamba hawakuwa miongoni mwa waalikwa.
Viongozi walifika katika eneo hilo ni pamoja na mbunge wa jimbo la
Moshi mjini ,Philmon Ndesamburo,wabunge wa viti maalumu Chadema,Lucy
Owenya na Suzan Lymo pamoja na madiwani wa kata za manispaa
wakiongozwa na mstahiki meya wa manispaa ya Moshi Jafary Michael.
Mipango ya CCM ilionekana kugonga mwamba baada ya kuwepo kwa muitikio
hafifu wa wakazi wa eneo la Kiboriloni ambalo linatajwa ni kuwa ni
ngome ya Chama cha demokrasia kwa kipindi kirefu huku watendaji kwa
kushirikiana na baadhi ya viongozi wa CCM wakijaribu kuokoa jahazi kwa
kubadili ratiba ya shughuli hiyo.
Awali ratiba ilikuwa inaonesha baada ya msafara wa Waziri Maghembe
kufika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Ofisi za mamlaka ya maji
safi na maji taka mjini Moshi na kupita katika mitaa mitatu ya kata
hiyo inaonesha mwenyekiti wa mtaa wa Mnazi Frank Kagoma ndiye alikuwa
afanye ukaribisho pamoja na utambulisho.
Hata hivyo hali hiyo ilibadilirishwa ghafla kufuatia maelekezo
yanayodaiwa kutoka kwa viongozi wa CCM kumuondoa katika ratiba
mwenyekiti huyo ambaye anatajwa kugombea nafasi ya udiwani katika kata
hiyo licha ya kwamba alikuwa eneo la tukio hakupata hata nafasi ya
kutambulishwa.
Akizungumza baada ya kupatiwa nafasi mbunge wa Moshi mjini Ndesamburo
alianza kwa kurusha vijembe huku akimsihi Waziri Maghembe kuwaonya
watendaji wasisababishe wanasiasa kugombana kwa sababu ya shughuli za
maendeleo.
"Ndesamburo kama mbunge wa Moshi Mjini na mkazi wa eneo hili la
Kiboriloni nimekuja hapa lakini sikualikwa, mradi huu unazinduliwa kwa
sababu tuna uchaguzi mdogo wa udiwani kwenye kata hii mwezi
ujao…Mheshimiwa Waziri (Maghembe) watendaji wasitugombanishe wanasiasa
kwa ajili ya shughuli za maendeleo,Nitaomba uchukue hatua na
nitakukumbusha hata tukiwa kwenye vikao vyetu kule Dodoma,"alisema
Ndesamburo.
Baada ya Ndesamburo kumaliza kuzungumza,Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Moshi Mjini,Elizabeth Minde, alisimama na yeye katika jukwaa hilo
akiwaambia wakazi wa Kiboriloni kwamba kinachofanyika Kiboriloni ni
utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kuwa kiliahidi maji
safi na salama wananchi wake.
"Kwanza hiki alichokisema mbunge wetu (Ndesamburo) wala hatujui huo
uchaguzi utafanyika lini maana hata tarehe
haijatangazwa.Kinachofanyika ni utekelezaji wa ilani ya CCM kwa sababu
tulipeleka kwa wananchi mwaka 2010 na wao Chadema walipeleka ya kwao
sisi tukashinda kuunda serikali kwa hiyo ndo mana tunatekeleza
tulichoahidi,"alisema Minde.
Akizungumza na Tz daima kuhusu hatua yake ya kugomea kwenda kuotesha
mti katika eneo hilo la mradi Meya wa Manispaa ya Moshi,Japhari
Michael,alisema kilichotokea ni kitu kibaya katika siasa kwa sababu
miradi ya maendeleo inataka kuwagawa wananchi badala ya kuwapa faraja
ya kufikia malengo yao katika mipango ya kichumi na hasa huduma za
jamii.
"Nilichokuwa namwambia mkurugenzi wa maji, nchi hii inaongozwa kwa
mujibu wa katiba,na wananchi ndio wanatakiwa wasimamie miradi
hii,walinde mabomba ,mali na vitu vingine na hao hao ndio wanatakiwa
wachangia huduma hii ya maji,ukiingiza siasa kwenye vitu kama hivi
mana yake unaanza kugawanya wananchi"alisema Michael.
Alisema mkurugenzi huyo asipokuwa makini atashindwa kuendesha miradi
ya maji katika manispaa kutokana na ukweli kwamba jukumu la kulinda
miundo mbinu ya maji liko kwa wananchi na wao wamekuwa wakiwatumia
madiwani kusimamia suala la ulinzi ya miuondo mbinu hiyo.
"Sisi hatujazoea haya mambo ya kugawanya watu katika maswala ya
maji,leo mradi wa maji mmeingiza watu wa CCM ,kama CCM wanataka kura
za udiwani wafanye kwa utaratibu wao sio kwa kutumia mamlaka ya
maji,"alisema Michael.
"Halmashauri manispaa ya Moshi tuna miradi ya maji ya kuchimba visima
ya kusapoti maji ya Moshi, kwa hiyo na sisi tuzuie hii miradi ya maji
isije kwa MUWSA maana tumekuwa tunashirikiana na mamlaka kwa sababu ya
Maji….yeye anawaatamia CCM waonekane kwamba ndio wanafanya hii
kazi,wasubiri wakati wa Uchaguzi."aliongeza Michael.
Hata hivyo,Waziri Maghembe alisema hakuna ubishi kwamba mradi huo
unatokana na utelelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi na kwamba
kikubwa wananchi wamepata huduma ya maji safi na salama na kwamba
suala la uchaguzi mdogo ni suala jingine.
Mradi huo wa maji Kiboriloni ulipangwa kutekelezwa kwa awamu
tatu,ambapo awamu ya kwanza ilihusisha ujenzi wa bomba kubwa umbali wa
kilomita moja kutoka mto Rau hadi KDC wakati awamu ya pili ilihusisha
ujenzi wa umbali wa kilimota 1.2 kutoka KDC hadi Kiboriloni mnazi na
awamu ya tatu ni uchimbaji wa kisima kikubwa eneo la KDC.
Mwisho.
Hapa I was dam wrong!, kumbe kupata uwaziri siku hizi, mtu sio lazima mpaka ukae mguu upande!. Uteuzi wa Mhe. Pindi Chana ni uthibitisho wa hili.Cabinet ijayo ni timu ushindi. Pindi Chana hawezi kabisa kuletwa, anajifanya tuu strictly mguu upande haweki!. Alipaswa awe waziri zamani tatizo sio mnyenyekevu!.
Pasco
Wenye macho hili wameliona!, si umeona?!.Ila Pindi Chana ana sura nzuri sana. She is cute!
Mkuu Salary Slip, angalau ulituandaa tusijeshangaa!, huvyo hatushangai!.Usishangae hata Kawambwa akaachwa kwasababu tu yeye na raisi ni mtu na......
Mkuu Salary Slip, angalau ulituandaa tusijeshangaa!, huvyo hatushangai!.
Pasco.
ni Deo Filikunjombe ili kumcontain....summon
Atakayeingizwa ni Deo Filikunjombe ili kumcontain, Dr. Mwaki pia atahamishwa to save his face na madudu ya Bandari na ATCL
Pasco