Baraza la Mawaziri: Nani atoke, Nani abaki, Nani aingie?

1003997_551237521606913_2095186244_n.jpg
"Zipo taarifa kwamba wapo baadhi ya wabunge wataingia kwa mara ya kwanza kwenye baraza hilo, huku wengine wakirudishwa kwa mara ya pili.

Taarifa za uhakika kutoka kwa watu wa karibu wa baadhi ya wabunge, zimebainisha kwamba jana(1 jan 2014) Rais Kikwete aliwaita Ikulu baadhi ya wabunge vijana, hata hivyo haikujulikana waliitwa kwa sababu gani.

Baadhi ya wabunge wanaotajwa kujumuishwa kwa mara ya kwanza kwenye baraza hilo ni Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Kahama, James Lembeli, sambamba na mmoja wa wabunge vijana kutoka mikoa ya Iringa na Njombe.

Wakati wabunge hao wakiitwa Ikulu, zipo taarifa za uhakika kwamba mawaziri wote wametakiwa kusitisha mapumziko yao ya mwisho wa mwaka na kurejea Dar es Salaam."

source: BARAZA LA MAWAZIRI LAIVA, MAWAZIRI NA WABUNGE WAITWA DAR « mtandao-net


Mwiguru amekuwa akitajwa sana katika baraza lijalo. kama atachaguliwa unafikiri nafasi ipi ITAKUWA SAWA KWAKE?
ZILIZO WAZI:


  1. Waziri wa Maliasili na Utalii,
  2. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
  3. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,
  4. Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ,
  5. Waziri wa Fedha,


ZA MAWAZIRI MIZIGO:


  1. Waziri wa Maji
  2. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
  3. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
  4. Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi,

 
Kwa jinsi alivyo hawezi kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi! Jamaa ni kimeo sana!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa mamlaka aliyopewa na KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,kuna habari kuwa lawrence masha atakula shavu..kwa kuteuliwa kama mbunge,then kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani..kwa mwenye any source please.
 
Kwa mamlaka aliyopewa na KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,kuna habari kuwa lawrence masha atakula shavu..kwa kuteuliwa kama mbunge,then kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani..kwa mwenye any source please.

ila jamaa kweli anafaa.
 
Kwa mamlaka aliyopewa na KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,kuna habari kuwa lawrence masha atakula shavu..kwa kuteuliwa kama mbunge,then kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani..kwa mwenye any source please.
Jamani hebu tuwe serious! Hizi tetesi nyingine hazina hadhi hata ya kuwa tetesi.
 
Rais Wangu Kikwete mimi nikijana wako katika Taifa unaloliongoza Mwigiru Chemba hafai kuwa kiongozi hasa kwa mafasi tajwa zilizo wazi haitaisha miezi miwili utabadilisha waziri tena katika wizara iyo Mh kingwara ni dumila kuwili Hamna shart linalomtosha hapo. Kuwa macho mzee
 
hata mimi naona PrOF Mwandosya huwa hana mashiko sana sana na pia amechoka na umri umekwenda apumzike siasa watu wapo.Kuongezea tu nafasi ya wizara ya fedha mpaka sasa naona Mh.Mwigulu anastahili kupewa sijui wenzangu mnasemaje
 
Tibaijuka amefanya nini wizara ya ardhi, aondolewe kabisa, waje watu wenye uwezo, profe bila taaluma na taaluma bila michango kwa maendeleo na maboresho ya sera ni kazi bure

Tibaijuka mwanzo nilimuheshimu sana, nikaona ni hazina iliyorudi nyumbani, kumbe bure kabisa,.

Nilisikitika hasa niliposhuhudia wakazi wa Mivinjeni wakibomolewa nyumba zao na kuishia kupewa viwanja Puna 50km kutoka kigamboni....!!!

Eneo lenyewe porini na unabomolewa nyumba unapewa kiwanja

Hii serikali hii!!!! Hakuna anayefaa
 
Kuna wizara moja tu ambao nashauri ,kama aliyekuwepo amefukuzwa basi naibu wake aliyepo hafai kuwa waziri maana alishatajwa kujihusisha na ujangili wa meno ya tembo, ninamwona ktk vyombo vya habari siku hizi akijipambanua kama mpambanaji na ujangili ,ukweli ni kuwa naibu waziri huyu anasemekna anahusika na kuuza ndovu hizo kwa mika mingi. Iweje apigiwe upatu wa kuwa waziri wa maliasili. Alikuwepo bosi wake kagasheki alikuwa anampinga leo eti anaonekana kinara. Ushauri ni kwamba wizara hiyo wapewe wabunge wengine na watz wengine. Huyu naibu wa sasa hapana na jangili naye. Anahusika na uhujumu wa meno ya temo nchini. Nathani usalama wa taifa mtasaidia kumfikishia mh. Rais hili suala , maana asije akamkabidhi fisi bucha. Tetesi za kumpa uwaziri huyu naibu wa maliasili ni janga kwa uhifadhi tanzania.
 
Kikwete...mpe jenerali waitara kitengo kwani ni jembe.acha mambo yako muache apige kazi upate sifa weye.
 
Hapo ni kubadilisha viungo tu lakini plau linabakia kuwa lile lile - kwa muda uliobakia hata ije safu gani hakutakuwa na cha ziada:

Nachokisubiria mimi na kinachonipa amani ni huu ujio wa katiba mpya nina imani inaweza kutibu majeraha ya watanzania!!

Hata ije safu gani,,, hakutabadilisha kitu maana watatumikia mfumo huu huu uliopo ambao ndiyo tatizo sugu.
 
upo sahihi. Taja taja yangu ililenga zaidi kuchokoza mada, natarajia wachangiaje wengine waje na mapendekezo yao au kupinga ya kwangu kwa hoja kuliko siasa.

Sent from my blackberry 8520 using jamiiforums
samweli sitta mambo ya ndani ya inchi,magufuli maliasili na utalii, mwakyembe elimu,kagasheki ujenzi
 
Hivi marehemu Kolimba si alishasema hiki chama KIMEOZA?Kimefufuka lini?

Mie nasubiria 2015,maana kwenye hii serikali dhaifu ya CCM,wabunge dhaifu wa CCM na rais dhaifu wa CCM sitegemei jipya!

Ndoto zangu zoote nimezihamishia kwa rais ajaye na najua nyote mwamjua!
 
Back
Top Bottom