Baraza la Mawaziri: Nani atoke, Nani abaki, Nani aingie?

Watarudishwa kulingana na Mgawanyo wa mikoa Kangi hatoweza kupata kwa kuwa Mawaziri wa Mkoa wake hawajaguswa kabisa
 
Yaani mwigulu apewe uwaziri, tobaa!! Kweli jk atakuwa amechemsha, maana atakuwa anaingiza furushi zaidi ya mzigo!
 
Mkuu wa kaya ana kazi kubwa maana viongozi waadilifu wameadimika.ni mtihan mkubwa,yote haya na choko zote zimeaneishwa na cdm
Yeye mwenyewe hana maadili, atawapata wapi wenye maadili??*
Liwalo na liwe.
 
msifikiri mnayemuona nje ni mzuri sn akiwa ndani, hata hao walioko ndani walikua wazuri nje. Siasa za sasa ni kudanganyana ili siku ziende, hata kama ingekua ww au mm kuna uongo, na ukiritimba ungetokea kutokuaminiana. NA ILI UNIELEWE ZAIDI, SIDHANI KWAMBA KUNA RAIS YEYOTE, AIDHA UPINZANI, AU CHAMA TAWALA, ATAKAESHIKA DOLA AWAMU MBILI. (1) hamna mtu mwanasiasa wa sasa, atakayekua na subira za awamu 2, (2) kuna vijana wengi wako njiani kimasomo na siasa, wenye weledi mpana, kuliko hawa wazee wa 1900......., (3)// tekinolojia itapanda zaidi, kiasi kwamba mtu wa kudanganywa atabakia tu wale wasiojiweza. (4) mwisho kura hazitahesabiwa kwa mikono, zitahesabiwa na mashine kwa kumbukumbu na umakini zaidi.
 
Migilo banik moo kamtema hawezi kazi ndio maana ameshindwa kumaliza nae mihula miwili alikuwa mvivu kilasiku alikuwa ansingizia anaumwa ikapelekea muhula mmoja ulipo isha akamtema sasa jk akimteua migilo itakuwa vichekesho litakuwa balaza lilelile la mizigo tena nasema jk akishidwa kupata wachapa kazi akaleta waganga njaa afadhali awaache hawa hawa mizigo amlize nao maana akituletea mozigo watakuja wamejipanga kuja kuvuna pesa kwenye mawizara wajipange kwa uchaguzi wa 2015
 
ni upuuzi kufikiria mtu kuwa waziri kwa sababu ya matukio. mfano, huyo lugola kuchangia tu bungeni tena siku moja imekuwa tiketi ya kuukwaa uwaziri? narudia kusema ni upuuzi kufikiria mtu kuwa waziri kwa sababu ya tukio tena kwa kuongea tu bungeni badala ya utendaji kazi wake wa siku zote. kwa staili hii hata kibajaji, sugu, lema, kiwia na nkamia nao wanaweza kuukwaa siku moja. upuuzi.

siwapendi ccm wote lakini nafikiri kangi umjui vizuelri au huna records zake''if u have lack of infomation u have no right to speek''
 
Mchambuzi,

Zile sababu zilizomfanya Mh. Lowasa atoke madarakani hazitakuwa na mashiko tena? Na kama ni hivyo, kwanini basi asirudi kwenye nafasi aliyoondokea? Bado naamini ikija suala la utendaji atafanya vizuri zaidi ya Mh. Magufuli.

Uko sawa kabisa mkuu! Kama vipi Lowasa arudishiwe nafasi yake(PM)
 
Last edited by a moderator:
Nadania Mama Migiro anaandaliwa kuwa Waziri wa mambo ya nje ama Waziri Mkuu
Nifahamuvyo mimi Waziri Mkuu lazima awe mbunge wa kuchaguliwa. Asha ni mbunge wa kuteuliwa, hivyo hawezi kuwa PM, unless mkuu JK anataka kuisigina katiba
 
Nadhani JK hawezi kufanya kosa la kurudisha Mawaziri Mizigo na wale walioondolewa. Nina maana kuwa, hawezi kurudisha watu kama Nchimbi, Kagasheki, Nahodha, Mathayo, Chiza, Kawambwa, Hawa Ghasia, Malima na Maghembe. Hao ni ukoma kwenye Baraza lake la Mawaziri. Pia, aepuke watu wenye shule zao lakini wezi kama Dr. Kafumu ambaye aliondoka kwenye Ukamishina baada ya kupiga dili la nguvu la Kabulo. Yeye akijua wazi nia ya Serikali kumiliki eneo hilo, akapiga dili la USD 7 mil kumilikisha watu binafsi eneo hilo. Pia, wapo watu kama Ole Sendeka, Mwigulu, Lugola wanatajwa kuwa wanafaa, lakini wote hao ni 000000000000000000. Kuhusu Dr. Migiro, taarifa zake kule UN ziko wazi kuwa alichemka. Ni vyema akaachwa kupumzika. Mfupa uliomshinda fisi .............. Kinachofanya Baraza letu kuvunjwa mara kwa mara ni JK kuteua watu kwa majaribio. Nichinjeni lakini hayo ni yangu ya moyoni. Nataka uteuzi wa JK safari hii uwe makini ili aokoe chama changu. Tumechoka kutukanwa kwa sababu ya wazembe wachache. JK Pleaseeeeeeeeeeeeeeeeeeee, usifanye makosa safari hii. Weka watu Mwakyembe/ Magufuli style.
A judge and a prosecutor-the same person
 
Jamani huyu Tibaijuka akipewa uwaziri Mkuu si atakuja kusema wazanzibar wapigwe mabomu? itakuwa bora Pinda aliyesema tupigwe kwa silaha nyepesi nyepesi?
 
ni tarehe moja,siku ya kwanza ya mwaka!hizi ndizo fikra nilizoamka nazo leo.
mbunge yeyote kama alivyoaminika na wananchi wakampa ridhaa ya kuwa bunge wao naamini anaweza akawa waziri.CCM oyeeeeee!!!!
sasa basi ili kukamilisha baraza la mawaziri ikiwa hivi itakuwaje?!

-WAZIRI MKUU,pinda aachie ngazi na hii nafasi tumpe bwana JOHN KOMBA (Baba lulu).kama ameweza kuiongoza TOT kwa muda wote nadhan kuisimamia serikali itakuwa sio kazi ngumu kwake.

-MALIASILI NA UTALII, hii me naona rais amteue (provided that ana nafasi zilizobaki) bwana KINANA (ndovu boy). hii ni kutokana na experience ya muda mrefu aliyonayo katika hii sekta. (mchawi mpe mwana alee)

-WIZARA FEDHA.kwanza kabisa tuchukue sekunde kumi kumkumbuka Dr. mgimwa.RIP brother (i cant say "gone too soon" maana ulikuwa mtu mzima enough).sasa nafasi yake naomba rais ampe bwana LUSINDE.nadhan atafaa kabisaa,maana kumpindua katapila malecela jimboni sio kazi ya kitoto.

-WIZARA YA MIFUGO,hii naomba tumpe bwana NGONYANI (prof maji marefu).unajua huyu jamaa na uganga wake anaweza akafanya maajabu kwenye hii wizara mkashangaa ng'ombe na mbuzi hawali tena majani na wanaishi bila shida.

-WIZARA YA MAMBO YA NDANI,Hii bwana angepewa yule kijana wa iramba ndugu NCHEMBA ingekuwa safi sana.naamini atafanya maajabu kwenye hii wizara.

-WIZARA YA ULINZI,hii na wewe ndugu mjumbe unaweza ukatoa maoni yako


happy new year.
 
Kuna taarifa ambazo si rasmi sana kuwa Mhe. Lowassa anataka arudishwe kuwa waziri mkuu na hataki uwaziri wowote wa kawaida.Pia nadhani sasa ni wakati wa Rais Kikwete kuteua watendaji badala ya wanasiasa. Mawaziri wengi wamekuwa wanasiasa zaidi hata kutoka nje ya fani na taaluma zao na kujikuta wakiboronga. Umakini wa JK unatarajiwa sana kipindi hiki cha lala salama kuelekea 2015
 
Tibaijuka amefanya nini wizara ya ardhi, aondolewe kabisa, waje watu wenye uwezo, profe bila taaluma na taaluma bila michango kwa maendeleo na maboresho ya sera ni kazi bure
 
Back
Top Bottom