Nani kamfunga mdomo Paul Makonda? Sijasikia akiwasema Mawaziri Mizigo

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Salaam Wakuu,

Nimeshangaa kuona Paul Makonda kubadili gia angani. Alipoanza kujitangaza, alikuwa akiwasimamisha Mawaziri watoe ufafanuzi na Wengine alikuwa akiwapigia simu akiwa majukwaani huku akisema Mawaziri mizigo siku zao zinahesabika.

Alifika mbali na kuwataka Mawaziri wawe wanatuma Ripoti kwake kila mwisho wa mwezi kuonesha nini wamefanya, atakayeahindwa ajihesabu kazi imemshinda.

Ni Hussein Bashe tu aliyemjibu kwamba yeye anawajibika kwa watu Wanne, rais, makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Makami waziri Mkuu

Jana Paul Makonda akiongea na Wanahabari pale Lumumba alikuwa kapoa sana. Nilishangaa kuona akisia Wizara na kuwasifia Mawaziri.

Nini kimemkuta Makonda? Mbona mapema sana kawa mpole?

Au kaachana na mbio za kuutaka ukatibu Mkuu wa CCM?
 
Mteua mizigo kamchimba biti kilo nane. Lazima apoe😅
 
Juu ya kutuma ripoti kwake Kila mwisho wa mwezi umepotosha ,ni Kila baada ya robo mwaka( miezi mitatu)

Tanzania hatuna Makamu Waziri mkuu ila Naibu Waziri Mkuu(DPM).

Kama kazi wamefanya vizuri hawana budi kusifiwa na kupongezwa. Kiongozi bora anatakiwa kujua kuhimiza, kuhamasisha na kupongeza na inapobidi kukaripiwa na kuchukua hatua.

Kama ilivyo Kwa ukatibu uenezi, ukatibu mkuu pia uko hivyo anayepewa ni Kwa sababu ya wajumbe na sio Kwa sababu ya jitihada zake.

naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom