Baraza la Mawaziri Limevunjwa! (2008)

Wana Jf mmeona mchango wa wabunge ulivyo kuwa na kuzaa matunda..naomba tujikite kuingiza vifaa bungeni 2010. Tukiwa na bunge lenye watu wenye uwezo na wazalendo serikali haitacheza shere, haitafurukuta. Kwa kuanzia naomba ma wapiganaji kama akin Tundu Lissu, Mama Kijo Bisimba na wengi muwajuao wanaopigania haki za wananchi on daily basis..2010 waingie bungeni kwa wingi kuwapa nguvu akina Zitto, Slaa na wenzao na hata wale wa "kijani mpauko" ambao wameamua kulitumikia taifa pamoja na vitisho vilivyopo.


Please JK..let the next PM be Mr. Magufuli..he will do you a good job.

Magufuli ni fisadi mwingine huyo hastahili hata kupewa ujumbe wa nyumba 10. Lile sakata la kuuza nyumba za serikali kwa bei ya bure linatosha kabisa kumfanya JK amweke huyu pembeni maana limeiingiza serikali gharama kubwa sana za kuwaweka watendaji wake na familia zao mahotelini kwa muda mrefu.
 
Huenda akawa Prof. Msolla. Simpendi lakini naona kila saa yanakuja hayo majina mawili, Msolla na Membe.
 
Huenda akawa Prof. Msolla. Simpendi lakini naona kila saa yanakuja hayo majina mawili, Msolla na Membe.

Inasikitisha lakini inaonekana kama huu ndio ukweli hapa. Tujiandae kwa Premier Membe! Mtandao bado utaendelea kutawala Tanzania kwa sasa.......... Tik tak tik tak tik tak.....
 
MWAFRIKA WA KIKE HAIWEZEKANI KABISA HUYO JAMAA KUPEWA UPM TUTAANDAMA KWA NGUVU HATA WAKITUPIGA MABOMU.KWANI TZ HAKUNA MTU MPAKA ROSTAM FISADI

Subiri tu ndugu yangu, hii story bado haijaisha hapa, kuna mengi sana hapa hayajasemwa na yatasemwa karibuni ila so far hakuna anayemgusa Rostam. Just wait uone usanii mwingine wa Mtandao ambao hujawahi kuonekana kwenye duru za siasa za Tanzania
 
Nimetafuta jina la PM kutoka kwenye list ya Kamati kuu sijaona... naendelea kutafuta kutoka kwenye Halmashauri kuu ya CCM
 
Mwakyembe anaweza kuwa rewarded a cabinet post in next cabinet, hasa portifolio ya sheria ambayo ilionyesha kulega katika ripoti ya kamati ya Bunge

Neno hilo Dotori,nakubaliana nawe kabisa,nakwajinsi siasa za Tz zilivyo,lazima Dr.alikuwa na Baraka zote za juu kwa jinsi alivyo hitimisha Ripoti yake.
They say: God gives a Reward,Man gives an Award.Who knows JK might award Mwakiembe.
 
Si ampe Mwandosya tu mambo yaishe? watu anaowapenda akanywe nao chai, watu wanaowajibika awape tu ili wakichemsha aweze kuwapasha directly bila hili wala lile.
 
Masatu hii mada unaweza usipate thanks...ingikuwa vyema ungempenyezea JJ Mnyika akaimwaga hapa JF..ingepata hits kubwa sana...lkn wewe unajulikana ni mwana CCM damu...

Posts zingine hata zinachekesha kusoma. Yaani hits za JF zinategemea nani kazitoa au ubora wa habari!.....
 
Mie nahisi kujiuzulu kwake kumekuwa ni kama njia ya kuharakisha adhabu na kuwafanya watanzania waridhike na kilichotokea ili madhambi mengine yafunikwe kupitia njia hiyo. Wengine wengi waliotenda madhambi yao kupitia scandal hii watasahaulika. Ila sidhani kama atakuwa kalazimishwa bali ni kurahisisha hukumu.
 
Mwafrika wa kike
Ushajiandaa na hiyo prize ya 84 cents?

ha ha haha hahha haha,

Kikwete ameshindwa kuvunja baraza lake la mawaziri.
Lowasa amejiuzulu na hivyo kusababisha baraza la mawaziri kuvunjwa. In the essence, Kikwete hakuvunja baraza la mawaziri, ninajiandaa kumpa Lowasa hii 84 cents!
 
Neno hilo Dotori,nakubaliana nawe kabisa,nakwajinsi siasa za Tz zilivyo,lazima Dr.alikuwa na Baraka zote za juu kwa jinsi alivyo hitimisha Ripoti yake.
They say: God gives a Reward,Man gives an Award.Who knows JK might award Mwakiembe.

Nahisi Dr. Mwakyembe atakuwa naibu waziri kama njia ya kuonyesha wamefurahia kazi yake kumbe ni kumpooza.
 
Masatu hii mada unaweza usipate thanks...ingikuwa vyema ungempenyezea JJ Mnyika akaimwaga hapa JF..ingepata hits kubwa sana...lkn wewe unajulikana ni mwana CCM damu...
Chuma mkuu wangu,mtake radhi Masatu bwana! tunakata issue tuu,mambo ya u-CCM hayapo hapa.
Mbona mama Kilango kazoza ile mbaya ndani ya jengo ilihali yeye ni CCM? Tunapambana na ufisadi kwa pamoja bila kujali itikadi.
 
Back
Top Bottom