Nafikiri cha kuangalia sasa hivi ni jinsi urafiki wa Lowassa na Kikwete utakavyo play..kama wataendelea kuwa marafiki wakubwa na Lowassa kuwa na no ill feelings then itakuwa a win win situation kwa Kikwete, lakini kama Lowassa na Kikwete wakiwa maadui kutokana na hii resignation, basi ninaamini asilimia 100% Lowassa atafanya kila awezalo ku sabotage Presidency ya JK. Ninamfahamu Lowassa ni mtu wa kulipiza visasi. Kule Monduli wakati wa uchaguzi wa ubunge mwaka 2005, alimfungia mwananchi mmoja bucha lake la nyama maeneo ya stendi ya basi Monduli kwa sababu huyo mwananchi alionesha nia ya kushindana na Lowassa kwenye kiti cha ubunge kwa tiketi ya chama pinzani. Cha kushangaza ni kwamba huyo mwananchi hakuwa na threat yeyote ile kwa mheshimiwa, ila kwa sababu jamaa anapenda kupita bila kupingwa ilibidi afanye ubabe. Baada ya kujitoa kwenye kinyang'anyiro huyo mwananchi aliruhusiwa kuendelea na biashara yake ya nyama.
Lowassa and Company...(ana ngome kubwa sana Arusha) wamefanya kazi ya nzuri sana ya ku raise hela na pia kumuuza Kikwete kwa wananchi japokuwa Kikwete alikuja na mvuto wake wa kipekee kutokana na wananchi kuchoka na regime ya Mkapa. Itakuwa interesting kuona..Ikiwa Lowassa atahama mji na atakuwa bitter basi Kikwete will have a very difficult time kumalizia term yake. Yetu macho.
Lowassa hana ujanja wowote wa kujifanya mtemi nchini Tanzania.
Ukiwa nje ya System Makende yote yananywea ndani kama mtu mwingine yeyote.
Watu wangapi walipo kuwa na vyeo serikali walionekana wana Hirizi ya Simba mla watu?
Wako wapi sasa hivi! Wamepotelea kwenye udhaifu wao wenyewe.
Wengine wamepat Stroke kwa kuzomewa kila wapitako.
Hata hizo biashara zake zitakufa moja baada ya nyingine, kama alipata tenda kwa sababu yeye ni waziri mkuu ajiandaye tu.
Na huyo mwanaye analelewa kama kinda la mwewe ni vema aanze kuota manyoya na kukomaa vipapatio, wakati wa kutapikiwa msosi na mzee wake mamvi umekwisha. Sasa inabidi aendeshe biashara kwa misingi ya faida na hasara siyo Spoon Feeding.
Bado tuna genge kubwa la Wahuni ndani ya serikali, kule wizara ya Fedha na wizara ya sheria wamejaa wahuni wengi ni lazima waadabishwe wote. Bila kusahau mama lao BOT.
Wizara ya mali asili nako kuna Genge la Mafia ambao wameuza serengeti kwa magaidi wa dunia na fedha yote kuitia ndani.
Tunataka nchi yetu tena tunaitaka yote siyo kipande.
Tukiiweka mikononi mwetu ninyi akina Lowassa msifikiri yamekwisha,
ni lazima tuwapeleke Mahakamani mkajibu mashitaka ya kuhujumu uchumi.
Hili la kuwashitaki tutalivalia njuga kweli kweli, anaye Save ni yule anayerudisha namba kwa Muumba tu kama yule mzee wa ENRON.