Kwanza nawashukuru wana JF kwa michango yenu mingi mnayo itoa hapa kijiweni. nashukuru kwa kuamua kutumia muda wenu mwingi kutafuta habari na kuzileta hapa JF.
Pia nawashukuru kwa kuendeleza moto wa mapambano ya kuwakatilia mbali Mahabithi Mafisadi wakubwa ndani na nje ya serikali.
Wana Jf mmefanya kazi kubwa sana kutoa elimu ya uhakika na kutoa mfano wa namna ya kushikia bango uoza wa viongozi wa serikali na vyama vya kisiasa.
Naomba moto huu wa kwenda kinyume na maovu ya watendaji wa serikali undelee na udumu daima.
Juhudi zenu za kutumia uwanja huu wa Kisasa kabisa katika kufikisha ujumbe wa Mageuzi ya kweli Tanzania zimefanikiwa vyema na zimeonyesha wazi kwamba hakuna tatizo linalo shindikana kutolewa mwafaka pale wananchi wenye uchungu na nchi ya wakiwa na nia thabiti ya kulikomesha.
Ninaamini kabisa kwamba kijiwe hiki kitatoa wabunge wengi sana endapo tu wana JF walio wengi watakwenda sambamba na maneno yao na mawazo yao na kuyageuza vitendo halisi katika uwanja wa siasa.
Vita hii ndo kwanza imeanza tu, kuna mengi yanakuja yanayo hitaji busara kuu.
Ikumbukwe kwamba ushindi si kushika namba moja tu ni pamoja na kupambana kwa nguvu zote hadi kieleweke.
Mahabithi hawa wenye Roho za kifisadi watajaribu kufa na watu wengine ili ionekane ni kifo cha wengi, naomba tusiwape nafasi hiyo kwa kuichua maovu yao yote.
Mahabithi hawa watajaribu kuFight back ili kudhoofisha nguvu za wanamapambano na wana mageuzi wa kizazi hiki, jaribio hilo likitokea ni lazima wafikishwe mahakamni.
Nawaombeni wana JF mtumie busara zenu kuangalia nyendo zote za watu hawa nje na ndani ya Tanzania ili kamwe wasipate nafasi ya kuharibu taratibu na mipangilio ya kuwang'oa katika juhudi zao za kutaka kujijengea ngome zisizoshambulika.
Kumbukeni hata Ibilisi alipo fukuzwa Mbinguni hakunyang'anywa nguvu zake. Anazo zote hadi hivi niandikapo walaka huu.
Ukimwendea Ibili bila kufuata utaratibu wa kiroho atakupa maumivu ya mwanakoma.
Naomba Mungu awabariki wana JF wote wenye nia njema na kuwapa neema zote katika mawazo yenu katika ndoto zenu na katika mapito yenu yote.
Nawaombea kwa Mungu ili akwajaze hekima kuu ili muweze kupambana na tufani ya mageuzi haya ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini Tanzania.
Mungu yuko upande wetu, tumwogope nani?
Kwako MH Lowassa.
Mimi binafsi nimekuwa mpiganaji mkubwa nikipiga kelele juu ya Uhabithi wako.
Mungu amekulipa uovu wako, si haki kabisa kumlaumu Dr Mwakyembe wakulaumu ni dhamira yako chafu ya kupenda kutajirika bila kufanya kazi, na zaidi kutajirika huku ukiweka nchi katika lindi kuu la umasikini wa kujitakia.
Unaifilisi na kuiangamiza kwa hila na chuki nchi ambayo imekulea hadi umeota mvi ukiwa kijana.
Wewe na Wazebaki wenzako ni lazima mahali penu patoweke kabisa, libakie jivu tu juu ya mahali hapo
MH sana Mamvi hatimaye umevuna ulichopanda. Ulipanda bangi ili utuvutishe Mungu mkubwa umevuna bangi na sasa inabidi uivute mwenyewe na mashoga zako.
Bangi hailiwi kama mchicha bangi inavutwa katika msokoto. Nakuombea uvutaji mwema, angalie tu usiwape wanao hiyo misokoto.
Mungu akipenda nitakuja kukusalimu na kukujulia hali ukiwa Keko na kibaka chako kwenye mfuko wa shati.
Hii ni katika kukuonyesha kwamba kama unajua maana yake kimbilia ughaibuni.
Buriani ya kisiasa MH Lowassa.