Baraza la mawaziri la dharula usiku huu

Mbona hii habari imekaa kizushi sana?
I'm pretty sure hii habari si kweli. Hakuna uwezekano mkutano wa dharura wa Baraza la Mawaziri uitishwe halafu Raisi ashindwe kuhudhuria akiwa mzima na yuko hapa nchini, umbali wa saa moja kwa ndege. Nakubali inawezekana kuna kikao kinachohusisha mawaziri kadhaa, including waziri wa Afya lakini hakitakuwa na nguvu kama alivyosema mwanzilishi wa topic.
 
Hivi si waziri mponda aliyewaita madaktari wanaharakati na kuwa wao si muhimu bali watu muhimu ni wakalima na wafugaji wa jimboni mwake? Maneno ambayo hajayakanusha wala kuomba msamaha?
 
Tunateseka kwa sababu Rais aliye madarakani hakuchaguliwa na watanzania, alitumia pesa yake kupata madaraka, viashiria ndio kama hivi, jifunzeni kwa mfano wa nabii suleiman alipoletewa kesi mbele yake kuwahusu wamama wawili wakivutania kitoto kichanga ki-hai na mwili wa kitoto kichanga kana kwamba mtoto yupi ni wa nani huku kila mmama akidai aliye hai ndiye wake! (mmama mmoja wao alifanya hila, alimlalia mwanae usiku akafa, akamchukua wa mwenzie na kumuweka wake aliyekufa ubavuni pa mwenzie. walipoamka tazama mwenzie alipomtazama kwa makini aligundua kitoto kilichokufa si chake mzozo ukaanzia hapo) mfalme suleiman alipoona kila mmoja anang'ang'ania kuwa mtoto mzima ndiye wake, aliamua aletewe shoka ili amcharange vipande viwili awagawanyishe wale wamama. yule mwenye mtoto hai aliposikia hivyo akamwambia mfalme akasema mpatie huyu mama mtoto huyu hai usimcharange! lakini yule aliyemlalia kichanga wake akamwambia mfalme akasema "bora umcharange tukose wote!!!" ndiposa mfalme suleiman alipotambua ya kuwa kichanga hai kilikuwa cha yule mama aliyebambikiwa na mwenziwe, na akaamuru akichukue kichanga chake. AMINI NAWAAMBIENI kikwete hakuchaguliwa na watanzania. Ni baba gani watoto wake wakimuomba samaki akawapa nyokaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!
...ahsante sana mkuu kwa badiko lako hili,nimejifunza jambo moja kubwa sana...
 
I'm pretty sure hii habari si kweli. Hakuna uwezekano mkutano wa dharura wa Baraza la Mawaziri uitishwe halafu Raisi ashindwe kuhudhuria akiwa mzima na yuko hapa nchini, umbali wa saa moja kwa ndege. Nakubali inawezekana kuna kikao kinachohusisha mawaziri kadhaa, including waziri wa Afya lakini hakitakuwa na nguvu kama alivyosema mwanzilishi wa topic.

Ni kikao cha kufanya maandalizi ya kupokea madaktari zaidi ya elfu moja kutoka nchi za India, China, Misri na Cuba iwapo ma-Dr watatekeleza tishio lao la kugoma.

Na ma-dr wageni wakifika tu,..... dr kilaza atakayeendelea na mgomo kibarua kinaota mbawa.
 
I don't think there someone there serious in this issue. They are too politic.

The intention is not to come up with the solution once and for all. The intention here is about public reaction...about political consequences. Hela ya walipa kodi inatumiwa vibaya kama haina wenyewe.Kila siku tume zinaundwa na hakuna lolote la maana linalofanyika. Where there is no will....mhhh!
 
Mheshimiwa Mwanakijiji na wengine wote with all respect to you folks, hebu tuwe wakweli kidogo tu, hivi serikali ikianza kusalimu amri kwa madakatari, nchi itatawalika kweli? mtazame kwa mlango mpana

Tuongee kama waungwana siyo kwa sababu tu hatutaki CCM au hatumataki JK, lakini ki ukweri serikali kwanza ilifanya makosa kuwakubalia madaktari, hakuna fani iliyo muhimu zaidi ya nyingine hapa duniani, kila fani ina umuhimu wake katika jamii, mgomo wa madaktari na mstakabadhi wa posho za wabunge, ilikuwa ni wakati muafaka kwa serikali kufanyia marekebisho mishahara yote, kwani watu kwa miaka mingi walikuwa wakilalamika uwiano wa mishara ya ya Benki kuu, TRA ambapo kuna wakati karani wa BOT alikuwa anamzidi mshahara profesa wa chuo kikuu.
Laiki serikali yetu imeshindwa kutumia huu wakati na mwanya kufanya marekebisho, manasahau kuwa hawa madakatari mpaka kufikia hapo ni kazi nzuri iliyofanywa na walimu toka shule za msingi mpaka sekondari, huwezi kuataarishwa ukiwa chuo kikuu peke yake, kama msingi ni mbovu hata hapo hafiki, sasa leo tunataka kuwadharau hawa wengine why?

Serikali lazima isimamame kidete kupinga huu upuuuzi

Sawa sawa on complementing

Na kauli za viongozi wetu "ahadi" ni jambo la kuchukuliwa tahadhari sana wakati wa conflict....they should never say what they cant or not sure of thy implementation. Ndo inapelekea mgogoro huu kuwa katika hali hii leo as kauli zilizotolewa kwa kweli ziliashiria matakwa yao kutekelezeka
 
Ni kikao cha kufanya maandalizi ya kupokea madaktari zaidi ya elfu moja kutoka nchi za India, China, Misri na Cuba iwapo ma-Dr watatekeleza tishio lao la kugoma.

Na ma-dr wageni wakifika tu,..... dr kilaza atakayeendelea na mgomo kibarua kinaota mbawa.

Unajua gharama za kumulipa dr wa nje ya bongo?............nani atalipa hizo gharama?
 
Kama hizi taarifa ni za kweli nitashangaa sana. Moshi na Dar sio mbali ki-hivyo, kwa nini rais asipande ndege aje kutatua mgogoro yeye mwenyewe?

Rais mwoga utamjua tu. Kiwete ndiyo tabia yake. Anajua kabisa nini kinaendelea lakini anaogopa kukabiliana nacho! Naona this time amekataliwa au amekosa Nchi ya nje ya kutembelea maana angelikuwa tayari ameruka na ndege kwenda majuu kukimbia mgogoro wa Madaktari.

Haiingi akilini kwa Rais mzima na akili zake ati aende Moshi kuongea na Maafande uchwara wanaoua ndugu zetu huku akijua kabisa kuna mgomo wa Madaktari unafukuta! Kwanini hataki kuwatimua Mponda na Nkya? Ana ubia gani nao??? Au ndicho alichosema kwenye hotuba yake ya mwisho wa Mwezi kwa anaogopa HASIRA ZA WABUNGE WA CCM?

kiwete bure kabisa hafai kuwa presida wa Tanzania.
 
mwisho wa siku atasema sio mimi nimechukua maamuzi,ni mawaziri hivyo kumfanya akae mbali na mitego,si mnajua tena pasi za mess
 
Kama hizi taarifa ni za kweli nitashangaa sana. Moshi na Dar sio mbali ki-hivyo, kwa nini rais asipande ndege aje kutatua mgogoro yeye mwenyewe?

Unashangaa!! Kwani Moshi siyo TZ....................?? Kama mgomo wa kwanza aliu-ignore na kwenda Swiss sasa huu atashindwaje kuucontrol kutokea Moshi?? Au unataka akatishe safari zake za kikazi za muhimu mikoani kuja kushughulikia mgomo wa madaktari??
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom