Baraza la mawaziri la dharula usiku huu

Baraza la mawaziri la dharula usiku huu

mtoto akililia wembe mpe ajikate mwenyewe. Walililia madaraka sasa yako wapi baada ya kuyanasa kwa mlango wa nyuma.............
 
Kuna tetesi nzito kuwa kikao cha baraza la mawaziri cha dharula usiku huu. JK mwenyewe yuko Moshi lakini kaagiza kifanyike chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais.
Agenda kuu ni mgomo wa madaktari na kuona njia ya kuwaondoa Dr. Mponda na Nkya bila kusababisha political fallout. Lile zengwe la Pinda la hapo awali ilikuwa ni danganya toto ili kupima joto ya maji.

Mawaziri wengi matumbo yako moto. Kuku weusi, kondoo na ng'ombe wameteketea kwa kasi jana na leo katika familia za mawaziri.

Hili ni la kuvunda halina ubani. Amewanyima madaktari mgomo umerudi, akiwapa, walimu wanagoma. Afanyeje?

Itakuwa Huko Moshi kwa upeo wa jk ni muhimu kuliko mgomo wa madaktari??
Mbona kama hizi ni chokochoko zisizo na kichwa? Makamu wa Rais atasema nini kwa mawaziri wakati Rais yupo ndani ya nchi?
Rais wa Zanzibar yupo???
 
kwani kikwete yeye haoni hata Vyombo vya habari vinavyoripoti?
kuna vingine si vya kusubiri kuletewa!
tusijerudi kule enzi za Mkapa, ambaye alikuwa anapenda kusikia positive things!
wakuu wa Mikoa wakimweleza watu wanashiba kumbe wafa njaa, kwenye
,isafara yake wanafunzi wasiokuwa na sare na viatu wakifichwa ndani ya mashamba ya mahindi!

"Nacheka kwa masikitiko sana"
Nalaumu sana TISS na taarifa wanazompa mkuu wa nchi,hali ni dhahiri itachafua nchi lakini system nao kama wamechoka vile!!!
 
Itakumbukwa kwa haya iliyofanya, kila mkikumbuka ndgu zenu waliokufa kwa mgomo wa madaktari mutakumbuka hii serikali........
 
Hivi baraza la mawaziri huwa wanafanyia mikutano uwanja gani?
 
he he he he ngoja tusibiri matokeo kwanza tuone ni aje hapa maana hamna kitu kinaeleweka ni vurugu tupu kwenye hizi siasa za kibongo bongo
 
Kujiuzulu kwa mawaziri kwa makosa waliyotenda ni jambo sahihi kabisa, na nchi ikatawalika.
ufinyu wa demokrasia ndio unaowasumbua Waziri wa afya pamoja na naibu wake.
Sauti ikishapazwa na Madaktari watu ambao wapo chini ya uongozi wa wizara yako, hapo
itabidi uchukue hatua ya kuondoka, usitumie nguvu kulazimisha kukalia madaraka,
bali ni kuwajibika kufikisha demokrasia katika kiwango kinachotakiwa.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kujiuzulu kwa mawaziri kwa makosa waliyotenda ni jambo sahihi kabisa, na nchi ikatawalika.
ufinyu wa demokrasia ndio unaowasumbua Waziri wa afya pamoja na naibu wake.
Sauti ikishapazwa na Madaktari watu ambao wapo chini ya uongozi wa wizara yako, hapo
itabidi uchukue hatua ya kuondoka, usitumie nguvu kulazimisha kukalia madaraka,
bali ni kuwajibika kufikisha demokrasia katika kiwango kinachotakiwa.


Tatizo ni kuwa wenye madaraka wengi hapa Tanzania wameyavaa kama nguo za ndani. Shughuli inakuwa wanapotakiwa kuyavua madaraka hadharani. Heri wangekumbuka maneno ya busara ya mzee yule kuwa "cheo ni dhamana, sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu". Damana usiivae kama chupi maana saa mwenye dhamana akiitaka inakuwa vigumu kweli. Cheo vaa kama koti. Mwenyewe akihitaji wala husumbuki unam-bwagia na hasa ikiwa sehemu yenye joto kama Dar (waliko hawa mawaziri) inakuwa ahueni - umepunguziwa joto!
 
hadithi hiyo inatufundisha nini? teh teh @ satellite
hadithi inatufundii sha kuwa....mwenzako akinyolewa na wewe tia maji. na kwamba, kisicho ridhiki haivutwi kwa kamba. tena, mbio za sakafuni huishia ukingoni. zaidi, njia ya muongo ni fupi. na mwisho, Kikwete Mwisho wake huooooo.......!!!!!!1
 
Dah,naomba mungu iwe ivyo, nimsute pinda, pinda ana mkwara sana, yani patamu sanaaaa
 
Unaweza ku prove kama rais hakuchaguliwa na sisi ?

Your vision is myopic 9/20....consult an opthamologist am restraining myself from asking for psychiatrist for you just know that I care......not just for you.....
 
eti pinda anasema mponda jaman ana mwaka mmoja tu na nusu hivi haya matatizo ameyakuta nikacheka sana kwani madoctor ni wajinga kutaka hao viongozi wa wizara watolewe?jk angalia nchi inakushinda
 
habari nzito sana hii, Tanzania yazidi kuwa moto,ikijapoa sijui nani ataipoza.
 
Tatizo la viongozi wetu hawajifunzi. Sikutegemea Pinda arudie makosa aliyofanya juzi tu ya kuwafukuza kazi madaktari na baada ya watanzania kupoteza maisha akaanza kuwasihi warudi kazini. nilitegemea alipata funzo hapo lakini sivyo. Mungu atuokoe na hili ombwe!
 
Back
Top Bottom