Baraza la Mawaziri Kukutana Jumamosi

hizi ni waziri gani yule licha ya mazabe yote lakini alithubutu kusema uchumi haujatetereka???????hakuwa mkubwa wa mawaziri kweli????
 
hizi ni waziri gani yule licha ya mazabe yote lakini alithubutu kusema uchumi haujatetereka???????hakuwa mkubwa wa mawaziri kweli????

Alisema pamoja na matatizo yote bado uchumi umegota kwenye 6% growth!.

Ni mwongo sana mtu mzima! Lakini bahati nzuri tunawajua kuwa ni mabingwa wa kupika takwimu!
 
Nimesikia kwenye BBC leo kuwa Baraza la Mawaziri litakaa siku ya Jumamosi hii (12/03/2011)kutathmini hali ya kuporomoka kwa uchumi nchini.

Akiongelea suala hilo, Waziri wa Fedha Mkullo amesema kuwa kuporomoka kwa uchumi kumesababishwa na :

i. uhaba wa chakula nchini,
ii. Kupanda kwa bei ya mafuta
iii. Matatizo ya Umeme.

Je wanajamvi, mnategemea Baraza la Mawaziri litaibuka na hoja gani ya matumaini kwa Watanzania?...Je tunawashauri nini kama altenatives za kiuchumi za ku'boost hali zilizotajwa hapo juu?

Hakuna jipya wakae wasimame hawana jipya hatuhitaji vikao kwa sasa haya yamejadiliwa since then nimechoka
 
Hivi hayo mafuta yamepanda Tz tu,zambia mafuta yanapita kwetu yanauzwa kwacha 3500,ambayoni sawa na tsh1100,wakati tz ni 2000,nafikiri kigezo sio mafuta,wTz tunalipa dowans au tunalipa zaid ya bilion 50 alizotumia mkwere kwenye kampeni.WAJINGA NDIO WALIWAO,

Mkuu haya tuliyataka wenyewe, tulipokubali kuuua kwa makusudi TIPPER!! Tukaji-submit kwa wezi waliotupa hii sera just kwa kuwa tulikuwa na shida. Nimeshangaa sana kusikia jana Mkapa anasema Africa itaendelea kwa juhudi za watu wake, rasilimali zake yenyewe!! Huyuhuyu ndo alifunga TIPPER!!!

Wazambia bado wana refinery yao, tunawapelekea crude kupitia TAZAMA!! Tumekalia wizi tu...
 
Nadhani ni muda mwafaka kwa wao kuangalia namna ya kupunguza gharama za maisha kwa wananchi, ikiwemo kupunguza kodi katika mafuta ili kuleta unafuu kwa wananchi.

Najua hakuna la maana litakaloongelewa, lakini watakuwa wamepata credit iwapo watagusia maisha ya Mtanzania wa kawaida!
 
Nimesikia kwenye BBC leo kuwa Baraza la Mawaziri litakaa siku ya Jumamosi hii (12/03/2011)kutathmini hali ya kuporomoka kwa uchumi nchini.

Akiongelea suala hilo, Waziri wa Fedha Mkullo amesema kuwa kuporomoka kwa uchumi kumesababishwa na :

i. uhaba wa chakula nchini,
ii. Kupanda kwa bei ya mafuta
iii. Matatizo ya Umeme.

Je wanajamvi, mnategemea Baraza la Mawaziri litaibuka na hoja gani ya matumaini kwa Watanzania?...Je tunawashauri nini kama altenatives za kiuchumi za ku'boost hali zilizotajwa hapo juu?

mkuu mbona Pinda alisema uchumi unakua?
 
Mkuu we subiri sana, watapongeza hutuba ya jk ya mwisho wa mwezi february . Hukusikia wakisema imetoa matumaini?
 
mkuu mbona Pinda alisema uchumi unakua?
Kujipa matumaini!

Umeona wapi uchumi wa nchi ukakua na dhiki zilizotajwa hapo juu?
Huyo bwana alikuwa anasoma data za 2009 na kurudi nyuma!

Hukusikia Mkuu majuzi alilidanganya taifa kuwa mabomu ya Gongolamboto yalilipuka tarehe 17/02?. kisa tu ameandikiwa hivo kwenye karatasi?
 
sina uhakika kama kunajambo jema watalileta lenyekuleta mabadiliko
ni kujilipa pesa zetu, sikubaliani na hicho kikao chao cha kupeana pesa.

kwani hakuna wa kuikemea serikali kwa mambo inayoyafanya ambayo yanachangia kupolomoka kwa uchumi
 
hivi miaka ya nyuma vikao vya baraza la mawaziri vilikuwa vinatangazwa???
 
Nimesikia kwenye BBC leo kuwa Baraza la Mawaziri litakaa siku ya Jumamosi hii (12/03/2011)kutathmini hali ya kuporomoka kwa uchumi nchini.

Akiongelea suala hilo, Waziri wa Fedha Mkullo amesema kuwa kuporomoka kwa uchumi kumesababishwa na :

i. uhaba wa chakula nchini,
ii. Kupanda kwa bei ya mafuta
iii. Matatizo ya Umeme.

Je wanajamvi, mnategemea Baraza la Mawaziri litaibuka na hoja gani ya matumaini kwa Watanzania?...Je tunawashauri nini kama altenatives za kiuchumi za ku'boost hali zilizotajwa hapo juu?

Watamjadili babu na tiba yake ya Loliondo na kuangalia kama kuna possibility ya mawaziri wengi kwenda kwa babu akiwemo na JK pia.
 
Nadhani watajadili sasa kwa hofu zaidi ya nguvu ya umma...Na mbaya zaidi leo hii Nauli za daladala na magari mengine zinapanda rasmi, hivyo malalamiko yatazidi!

Nauli za daladala na mabasi kwenda mikoani juu. Umeme ulishapanda tangu Januari,Sukari bei inapaa kila siku,Petroli inaongezeka baei kila siku.

Nimemsikia Mustafa Mukullo -FM akitoa sababu za kudorora kwa Uchumi:
Kataja sababu kama matatizo ya umeme,kupanda kwa bei ya mafuta na upungufu wa chakula(ukame).

Mimi kwa mtazamo wangu hizi sababu si hasa zinazofanya uchumi wa Tanzania uwe ICU. Nitaeleza:

Tanzania siyo nchi ya uchumi wake kuwa wa kubahatisha. Nchi hii ina raslimali(resources) za mabilioni kwa mabilioni ya shilingi. Tuna madini ya kila aina mengine hayapatikani popote duniani k.m.TANZANITE.Tuna DHAHABU,tuna ALMASI,tuna MAKAA YA MAWE,tuna GAS na kuna kila dalili kuwa MAFUTA ya kuendesha mitambo tunayo.Huo ni upande wa MADINI.

Tanzania imejaliwa kuwa na MBUGA ZA WANYAMA wa aina aina ambao huwezi kuwakuta popote duniani isipokuwa Tanzania. Tuna MLIMA KILIMANJARO,tuna ardhi yenye rutuba,(virgin land)ambayo haijawahi kuguswa na mkulima yeyote. Tuna mito na Maziwa yasiyokauka.

Lakini pamoja na kuwa na raslimali zote hizi we are still poor,our economy is one of the worst in East Africa, Africa and the World as a whole! Hapa iko tatizo kubwa. izo sababu alizotoa Mkulo is just a tip of an iceberg. Kuna sababu concrete zinazofanya uchumi wetu usuesue.

Sababu iliyokubwa kabisa ni UFISADI. Nashangaa kwanini Mustafa Mkullo hakuianzia hii sababu. Kama FM hajuia sababu kuu zinazosababisha Uchumi wetu kudorora basi hafai kuwa FM.(namaanisha Finance Minister).

Ni kutokana na UFISADI huu huu ndiyo maana Watanzania hatuoni hata faida au manufaa ya Raslimali tulizonazo kwa vila VIONGOZI WETU(serikali ya CCM) WAMEIUZA NCHI YETU KWA UFISADI WAO.Hapa nina maanisha kuwa Makampuni yote yanayochimba madini yote HAWALIPI KODI na wala KIASI CHA MADINI WANACHOCHIMBA NA KUUZA HAKUNA ANAYEJUA. Kuna ndege huwa zina fly daily kutoka kwenye machimbo zikiwa na madini na kutokomea kwenye nchi za aidha wawekezaji wenyewe hasa South Africa,Canada na nchi za wajanja kama Kenya,Uganda n.k. Tujiulize inawezekanaje TANZANITE inayopatikana TZ pekee ionekana kwamba ati nchi ya KENYA ndiyo iliongoza kwa KUUZA TANZANITE DUNIANI. Hii haingii akilini. Hapa lazima kuna shida!

Kenya wana nchi ndogo ukilinganisha na Tanzania,Wakenya hawana ardhi ya kutosha kama Tanzania, sehemu kubwa ya Kenya ni jangwa! Still UCHUMI WA KENYA is the BEST IN EAST AFRICA!!!Why na kwanini???Sasa hivi kuna vi nchi vidogo kama RWANDA vinakuja kasi sana kiuchumi. Rwanda iliyokuwa imekumbwa na mauaji ya kimbari(genocide) leo ati inakuwa na uchumi bora kuliko Tanzania. Kagame anafanya miujiza gani pale Kigali???Kwanini Kiwete na viongozi wenzake hawawezi hata kwenda kupata ushauri kwa viongozi wenzao namna ya kuongoza na kusimamia uchumi.

Ukiangalia nchi hizi yaani Kenya na Rwanda utakuta kwamba UFISADI uko katika kiwango cha chini sana.

Lakini pia pamoja na UFISADI kuna tatizo la MATUMIZI MABOVU YA FEDHA ZA WALIPA KODI. Mfano uliowazi kabisa ni UNUNUZI WA MAGARI YA KIFAHARI maarufu kwa jina la MASHANGINGI kuwa mawaziri na wabunge. Ni juzi tu Bunge letu limemaliza kikao cha Februari na huku Mawaziri na Wabunge wakiondoka na MILIONI 90 KILA MTU sawa na 32.4 Bilioni hela ya Kitanzania.Shilingi Bilioni 32.4 kwa ajili ya magari ya WABUNGE TU!!!Halafu leo Mkulo anasema nchi haina pesa,sijui umeme,mafuta,njaa na longolongo chungu mbovu.Huu ni uongo.

Yako wapi MABILIONI YA KAGODA,DEEP GREEN,MEREMETA n.k. Hizo hela ziko wapi??? Hela za EPA ilikuwa ubabaishaji mtupu. Mara walioiba warudishe bila kushtakiwa,mara zimepelekwa kweny Kilimo Kwanza n.k. Kama ni kilimo kwanza NJAA IMETOKA WAPI? Ukame ni mwaka huu tu, kwanini serikali yetu inaishi kwa DHARURA kila kitu???Umeme DHARURA, chakula DHARURA, MABOMU YA MBAGALA/G.MBOTO Dharura!!!!

No,Serikali ya CCM msitutubaishe bana. Nchi imewashinda. You better step down to leave room for others to lead this NATION. Najua hiyo J1 mnakuja kulipana mamilioni ya posho tu lakini YOU DON'T HAVE A SOLUTION AND WILL NEVER FIND ONE.

Any way tuendelee kupeana habari nini watazungumza hawa mafisadi na wababaishaji wakubwa. Let's wait and see.
 
Ajenda kuu itakayotawala kikao hicho cha mawaziri Mkwere akiwa mwenyekiti ni ile ya maandamano ya nguvu ya umma kuwa ni uhaini wa Chama Cha Chadema.

Wataipitia pia ajenda ya kujadili haki miliki ya CCM kutumia dola kushinikiza nguvu ya umma.
 
Bora, umetandika ikulu!..
Janja ya hawa jamaa imeshajulikana...sijui kama wanapitia haya majukwaa
 
Mahojiano ya Abdallah Bawazir wa Nipashe-Jumapili na Mzee Timothy Apiyo(Katibu Mkuu Kiongozi wakati wa Nyerere) kuhusu utendaji wa Baraza la Mawaziri wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere. Natumai Baraza hili la sasa kabla ya kikao cha jumamosi watapitia kujifunza jinsi wenzao walivyokuwa wanafanya kazi kwa mtiririko unaoeleweka:

ANGALIZO:
(JamiiForum tunataka Tanzania iwe na uteuzi wa viongozi ambao ni wanaoweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa bila kusahau uadilifu ndiyo maana tunapenda kujifunza kwa bidii zetu zote toka kila chanzo cha mawazo bora):

SWALI: Kuna hili tatizo la rushwa, wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere mlikuwa mnalishughulikiaje kiasi kwamba watu walikuwa wakiogopa kujihusisha nayo?

Timothy Apiyo: Siyo kwamba wakati wetu kulikuwa hakuna rushwa, ila tulichofanya ni kubana kabisa mianya ya rushwa na kwa wale watakaobainika kujihusisha nayo walikuwa wakiwajibishwa na kuchukuliwa hatua kali bila ya kujali wadhifa au nafasi yake katika jamii. Serikali ya Mwalimu Nyerere ilikuwa haina huruma na walarushwa.

SWALI: Hivi sasa kuna mikataba iliyoingiwa na baadhi ya mawaziri ambayo inalalamikiwa kuwa ni mibovu na kwamba ina harufu ya rushwa. Je wakati wa uongozi wenu mlikuwa mnasimamiaje suala la mikataba?

Timothy Apiyo: Wakati wa utawala wa Nyerere mawaziri hawakuruhusiwi kusaini wenyewe mikataba mikubwa ya mamilioni ya fedha. Uliwekwa utaratibu ambao waziri alitakiwa kuufuata kwanza kwa kuhusisha ngazi mbalimbali wakiwemo wataalam kabla ya kuingia mkataba husika.
Kwa mfano kama waziri alikuwa akitaka kuingia mkataba fulani kwanza alikuwa akipeleka pendekezo kwa waziri mkuu, ambaye naye analipeleka kwa rais na baraza la mawaziri kwa ajili ya kujadiliwa kuangalia umuhimu wake na gharama zake.
Kama ombi litapita waziri haachwi peke yake kushughulikia, itaundwa timu ya wataalam kumsaidia huku vyombo vya dola vikifuatilia kwa karibu kuona kama taratibu zote zinafuatwa.
Hivyo kulikuwa na woga, hakuna mtu kwenda kusaini mkataba nje ya nchi kama alivyofanya waziri mmoja kwenda kusaini mkataba wa mgodi wa Buzwagi nchini Uingereza. Haiwezekani waziri kwenda kusaini mkataba peke yake nje ya nchi bila ya kibali, lazima kuwe na kitu fulani kina mtazama anatekelezaje hivyo ataogopa kujihusisha na rushwa kwa sababu anajua atajulikana. Hii ilisaidia sana.
Kama hili suala la Chenge (Andrew Chenge) katika ununuzi wa rada mimi sielewi kama aliachiwa ashughulikie mwenyewe katika wizara yake, wakati wetu hili lisingeweza kutokea.

SWALI: Je maadili ya viongozi wa umma mlikuwa mnayasimamiaje?

Timothy Apiyo: Tulikuwa na kitu kinaitwa Tume ya Tabia za Viongozi. Kilikuwa ni chombo kinachoogopwa sana na viongozi wa umma.
Kilikuwa kifuatilia kwa karibu nyendo za viongozi wote na mtu ulikuwa unaweza kuitwa wakati wowote na kuhojiwa mali ulizonazo umezipataje. Unaulizwa wewe tunakujua, kwenu tuna kujua, ndugu zako, tunawajua, kipato chako tunakijua hizi mali umezipataje? Usipotoa maelezo ya kuridhisha ulikuwa unawajibishwa mara moja na kuchukuliwa hatua nyingine zinazostahili. Kulikuwa hakuna kufumbiana macho wala kulindana.

SWALI: Mlikuwa mkitumia mfumo gani katika kutekeleza maamuzi ya serikali ili kuhakikisha mambo yanaenda sawa?

Timothy Apiyo: Kila Katibu Mkuu alikuwa na wajibu wake, tuliunda kitu kinaitwa Cabinet Secretariet, huu ulikuwa ni mkutano mkuu wa makatibu wakuu wote mimi nilikuwa ni mwenyekiti wao.
Na mimi pale Ofisi ya Rais (Ikulu) nilikuwa na wataalam ambao wako chini yangu, hawa kazi yao ilikuwa ni kuangalia baraza la mawaziri limeamua nini kuhusu tatizo lolote lililotokea na kila wizara inafanyaje jukumu lake kuhusu tatizo hilo.
Baraza la mawaziri likishaamua sekta fulani ifanye hivi sasa unajua kunauzembe wakati fulani, ofisi ya rais ilikuwa na jicho lake, tunatuma wataalam ambao wako katika Cabinet Secretariet kwenda kuhoji Katibu Mkuu ama Waziri hili suala au uamuzi huu wa Cabinet unautekelezaje? Wanapata maelezo kule wanarudisha kwangu kama mwenyekiti wao halafu taarifa inakwenda kwa rais. Kwa hiyo rais wakati wote anakuwa na taarifa muhimu na sahihi katika matatizo ya utekelezaji wa wizara zake, ndiyo utaratibu tuliofanya.

SWALI: Je suala la ubinafsishwaji viwanda unalizungumziaje maana imaelezwa Mwalimu Nyerere hakulifurahia jambo hili.

Timothy Apiyo: Mimi na Amiri Jamal wakati tupo Wizara ya Viwanda na Biashara, viwanda vyetu vilikuwa vinafanyakazi nzuri sana, tulikuwa na viwanda vingi kama Urafiki, Mwatex, Mutex, Kilitex, Sunguratex na vinginevyo, tulikuwa tunavisimamia vizuri na tuliwaweka Watanzania kuviendesha. Suala la kuvitaifisha lilikuja baada ya sisi kuondoka, nakumbuka Mwalimu hakutaka kubinaifsisha viwanda vyetu, alisikitika sana.
Source: 3 October 2010 Home
 
Hakuna kitakachofanyika,hakuna mwenye kuifikiria tanzania
Kwa nini Mkullo alipresent kwa wahisani bajet tofauti na ile iliyopitishwa na bunge?
 
Baraza lenyewe ni watu wa aina ya Sophia Simba (Ukimwondoa Sitta, Magufuli, Mwandosya na Mwakyembe) litajadili nini zaidi ya ngono na ufisadi?

Hakuna jipya hapo kwasababu wenye mawazo endelevu hawasikilizwi na rais mwenyewe ni kilaza, fisadi na mwenye jeuri!!
 
Kujipa matumaini!
Umeona wapi uchumi wa nchi ukakua na dhiki zilizotajwa hapo juu?
Huyo bwana alikuwa anasoma data za 2009 na kurudi nyuma!
Hukusikia Mkuu majuzi alilidanganya taifa kuwa mabomu ya Gongolamboto yalilipuka tarehe 17/02?...kisa tu ameandikiwa hivo kwenye karatasi?

Hivi wasaidizi wa viongozi huajiriwa kutumia vigezo gani? Kila kiongozi anaboronga kwa sababu kadanganywa na msaidizi wake
 
Back
Top Bottom