Nakubaliana na Nape nguzo za Umeme zitumike pia kusafirisha Internet; ila namshauri liwe azimio la baraza la Mawaziri kusaidia utekelezaji

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Nape Nauye amekuja na suluhu ya kusambaza internet kwa kasi kuliko ilivyo sasa. Anasema kwa kuwa kila mwananchi anaumeme kwake basi miundombinu ya TANESCO itumike kufikisha mawasiliano kwenye makazi.

Nakubaliana naye kwamba tunakwenda kuondoa gharama za kununua nguzo ambazo ofcoz itapunguza ukataji miti lakini pia tunakwenda kuondokana na dublication ya resources.

Mawazo mazuri kama haya yanapaswa kuwa yalishafanyiwa kazi na inawezekana kabisa. Wasiwasi wangu mimi nikwamba wapenda tender waliopo TTCL na TANESCO wanaweza kuja na urgument kinzani kwako.

Ili kutekelezeka hoja hii nzuri kwenye wilaya napendekeza apeleke baraza la mawaziri wapitishe ili kila mmoja wa watoa huduma hizi awajibike kutekeleza maazimio ya baraza la mawaziri.

Hoja hii ikipitishwa na baraza la mawaziri itawafanya makatibu wakuu wote kuisimamia sambamba na wakurugenzi wa mashirika husika.

Natamani Nape afanikiwe wilaya zetu ziwe na fiber tuache utegemezi wa mawasiliano.
 
Nape Nauye amekuja na suluhu ya kusambaza internet kwa kasi kuliko ilivyo sasa. Anasema kwa kuwa kila mwananchi anaumeme kwake basi miundombinu ya TANESCO itumike kufikisha mawasiliano kwenye makazi...
Msikubali huo ujinga was Nape!

Kama nguzo zitatumika kusafirisha internet , internet itakua inakata kama umeme.!!yaani.wakijisikia kukata watakata kama umeme unavokata!!

Kutakua na mgao was internet!!
 
Wamesema hivi tangia 2021sijaona walichotekeleza zaidi ya hadithi
 
Mbona kama ndicho kinafanyika na mradi WA nguzo za zege unaambatana na mkonho WA Taifa (kama ntakua sijakosea)
 
Msikubali huo ujinga was nape!!

Kama nguzo zitatumika kusafirisha internet , internet itakua inakata kama umeme.!!yaani.wakijisikia kukata watakata kama umeme unavokata!!

Kutakua na mgao was internet!!
Mkuu kinachojadiliwa hapa siyo internet iwekewe switch ya TANESCO bali waya za internet zipite kwenye nguzo za Umeme; so umeme ukikatika internet haiwezi kukatika.

Nadhani umeelewa japo kidogo
 
Nape Nauye amekuja na suluhu ya kusambaza internet kwa kasi kuliko ilivyo sasa. Anasema kwa kuwa kila mwananchi anaumeme kwake basi miundombinu ya TANESCO itumike kufikisha mawasiliano kwenye makazi...
Mbona linafanyika hili mie nmetoka kufungiwa juzi tu tena na halotel
 
Mkuu kinachojadiliwa hapa siyo internet iwekewe switch ya TANESCO bali waya za internet zipite kwenye nguzo za Umeme; so umeme ukikatika internet haiwezi kukatika.

Nadhani umeelewa japo kidogo
Huyo nape ametoa wapi roho ya upendo wa internet Kwa watz kiasi hicho mwaka wa uchaguzi huu!!?

Kuna namna!ukiona jirani ambae ni Adui wako anakitendea wema ujue anataka unase kwenye mtego!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom