Baraza la Mawaziri Kukutana Jumamosi

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,723
Nimesikia kwenye BBC leo kuwa Baraza la Mawaziri litakaa siku ya Jumamosi hii (12/03/2011)kutathmini hali ya kuporomoka kwa uchumi nchini.

Akiongelea suala hilo, Waziri wa Fedha Mkullo amesema kuwa kuporomoka kwa uchumi kumesababishwa na :

i. uhaba wa chakula nchini,
ii. Kupanda kwa bei ya mafuta
iii. Matatizo ya Umeme.

Je wanajamvi, mnategemea Baraza la Mawaziri litaibuka na hoja gani ya matumaini kwa Watanzania?

Je tunawashauri nini kama altenatives za kiuchumi za ku'boost hali zilizotajwa hapo juu?
 
mbona walikutana juzi juzi na kubariki mitambo ya dowans kuwashwa, ina maana hali mbaya ya uchumi walikuwa hawajaiona, au people's power imewashtua?, anyway waje na ufumbuzi wa matatizo hayo sio siasa tena tumechoka.
 
Imekuwa ni wimbo wa taifa kila siku baraza la mawaziri kukutana na kujadili mustakabali wa nchi lakini hakuna ufumbuzi unaopatikana. waangalie na kufanya tathmini ya yale ambayo yatatekelezeka kiuhalisia katika ahadi zote alizozitoa JK kipindi cha uchaguzi.
 
mbona walikutana juzi juzi na kubariki mitambo ya dowans kuwashwa, ina maana hali mbaya ya uchumi walikuwa hawajaiona, au people's power imewashtua?, anyway waje na ufumbuzi wa matatizo hayo sio siasa tena tumechoka.
Nadhani watajadili sasa kwa hofu zaidi ya nguvu ya umma.

Na mbaya zaidi leo hii Nauli za daladala na magari mengine zinapanda rasmi, hivyo malalamiko yatazidi!
 
Wanaweza kutumia muda mwingi zaidi kwa ajenda ndogo kama za kukinzana akina Magufuli na waziri mkuu badala ya uchumi tata wa taifa.
 
wanachotakiwa kukifanya ni kumkemea rais aache ufisadi pia aombe ushauri kwa watu makini kama Dr.slaa na wengine na ausikilize na kuutekeleza
 
Waongelee pia na kukurupuka kwa Mawaziri mbali mbali na kutoa kauli ambazo zinapingana na kuonyesha wazi kwamba kuna ufa mkubwa katika utendaji na mawasiliano ndani ya baraza hilo la Mawaziri.

Kwa mfano yule Mwanasheria Mkuu Werema na Ngeleja walitoa kauli kwamba malipo ya Dowans ni lazima yafanyike na hayana jinsi ya kuyakwepa. Akaibuka Sitta na kuipinga kauli hiyo na kuhoji kikao cha baraza la mawaziri cha kubariki malipo hayo hakijafanyika na kuhoji kama Waziri mmoja anaweza kubariki malipo makubwa kiasi hicho bila kubarikiwa na Baraza la Mawaziri.

Magufuli naye akatangaza bomoa bomoa katika kupisha ujenzi wa barabara siku chache baadaye Pinda akasimamisha bomoa bomoa hiyo.
 
Wanaweza kutumia muda mwingi zaidi kwa ajenda ndogo kama za kukinzana akina Magufuli na waziri mkuu badala ya uchumi tata wa taifa.
Hiyo lazima waisemee!
Pia watamjadili kwa marefu Dr.Mwakyembe kwa kuwaanika UWT na njama zao za kummaliza!

Uwezekano wa kujadili seriously juu ya hatma ya taifa ni mdogo, maana pia imeripotiwa leo kuwa mawaziri 9 wameacha shughuli zao na kuanza rasmi kushughulikia malengo ya 2015!
 
Mbona mvua zinanyesha kwa kiwango kizuri tu mikoa ya kusini, kuna tatizo gani kwenye mabwawa ya kufua umeme? au ni hujuma ili mitambo ya dowans iwashwe?
 
Hiyo lazima waisemee!
Pia watamjadili kwa marefu Dr.Mwakyembe kwa kuwaanika UWT na njama zao za kummaliza!

Uwezekano wa kujadili seriously juu ya hatma ya taifa ni mdogo, maana pia imeripotiwa leo kuwa mawaziri 9 wameacha shughuli zao na kuanza rasmi kushughulikia malengo ya 2015!

Watakuwa wanaota kurudi madarakani wakati huo. Hawajui njia bora ya kurudi madarakani 2015 ni kukidhi haja za wananchi sasa.
 
Hivi hayo mafuta yamepanda Tz tu,zambia mafuta yanapita kwetu yanauzwa kwacha 3500, ambayoni sawa na tsh1100, wakati tz ni 2000, nafikiri kigezo sio mafuta, wTz tunalipa dowans au tunalipa zaid ya bilion 50 alizotumia mkwere kwenye kampeni.

WAJINGA NDIO WALIWAO,
 
Muasisi wa CCM mwenyewe aliishasema na mapema ya kwamba chama legelege huzaa serikali legelege, hivyo tutake tusitake serikali iliyopo madarakani ni legelege; hakuna kizuri kinachoweza kutarajiwa kutoka kwa serikali ya aina hiyo.

Tatizo la uchumi wetu siyo hayo yanayotajwa na Mkullo bali ni haya yafuatayo; uhamishaji wa rasilimali zetu kama magogo, madini n.k kwenda nchi za nje kwa bei ya kutupwa; matumizi makubwa ya serikali yanayotokana na kuwa na serikali kubwa sana, na hisiyo na tija yeyote, na vile vile inayojikita zaidi kwenye matumizi ya anasa kama misafara mikubwa ya viongozi, safari nyingi,ununuaji wa samani kutoka nje, magari ya bei mbaya n.k; kuwepo kwa rushwa kubwa kubwa katika ngazi za juu kunako sababisha fedha nyingi za nchi kuhamishiwa katika nchi za nje; kutao misamaha mingi ya kodi kunakosababishwa na mgongano wa kimaslahi n.k

Haya ndiyo mambo ambayo baraza hilo linapashwa liyashughulikie
 
Hivi hayo mafuta yamepanda Tz tu,zambia mafuta yanapita kwetu yanauzwa kwacha 3500,ambayoni sawa na tsh1100,wakati tz ni 2000,nafikiri kigezo sio mafuta,wTz tunalipa dowans au tunalipa zaid ya bilion 50 alizotumia mkwere kwenye kampeni.WAJINGA NDIO WALIWAO,

Na mafuta yenyewe yanapitia bandari ya Salama kwenda Zambia!...!!!!.Ni kitendawili hiki!
 
J'mosi Sio mbali, Meanwhile, tuendelee Kutafuta Ugali wetu kwanza (hata wao kwa Sasa ndo Wanachofanya!)

Wakishakaa tutawasikiliza Nasi Tutaongea tunavyotaka, lakini kwa Sasa hata tuseme Nini, yalokwisha Kusemwa yanatosha. Hebu tuwasikilize Kwanza!
 
Kikao hicho sikitofautishi na kijiwe cha wanywa kahawa, hakita kuja na maamuzi magumu ya kulikwamua Taifa na matatizo yanayopigiwa kelele na wananchi.

Watamsifia Rais wao, wataisema CDM na kuchukua posho wataondoka na mashangingi yao.
 
Mimi ninaona baada ya kikao wataibuka na hoja ya kupewa allowance zao za kikao bila kuwa na kitu cha maana kuhusu mustakabali wa Taifa kiuchumi.
 
Back
Top Bottom