PreGE2025 Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC): Wote waliokamatwa kwa kudai haki, wakiwemo viongozi wa vyama vya kisiasa, waachiwe haraka na bila masharti

PreGE2025 Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC): Wote waliokamatwa kwa kudai haki, wakiwemo viongozi wa vyama vya kisiasa, waachiwe haraka na bila masharti

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
kenge wewe, ulitaka ataje specific object wakati somo linaeleweka kwamba wote waliotiwa ndani kwa kudaia haki waachiliwa bila masharti
Hapa ndipo nasema nchi hii si chadema wala ccm. Yaani hakuna mwenye uvumilivu pale anapokutana na wazo tofauti la mwenzie.

Sasa kama huko chadema/tec hamuwezi kusahihishwa mpaka mnawaita wengine kenge, tukiwapa nchi halafu chauma wawakosoe, si mtatuchinja kabisa kama wanavyofanya wenzenu?

Kwa hekima ulitakiwa unieleweshe, badala yake umekuja na mtusi
 
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa wito kwa serikali ya Tanzania kuwaachilia mara moja na bila masharti viongozi wa kisiasa waliokamatwa kwa kudai haki, likisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda amani ya taifa, hasa kuelekea mwaka wa uchaguzi.

Rais wa TEC na Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, Mhashamu Wolfgang Pisa, amesema kuwa amani ya kweli haiwezi kupatikana kwa kutumia nguvu bali kwa maridhiano na haki, akisisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda amani ya nchi kwa kuhakikisha mifumo ya uchaguzi inarekebishwa ili kutoa nafasi kwa upatikanaji wa viongozi wa haki na wa kweli.

“Katika hali ya kawaida, nani anaharibu amani? Anayetumia nguvu na kusisitiza uchaguzi uende anavyotaka yeye au yule anayesema ‘jamani turudi mezani ili tuangalie mifumo yetu ya uchaguzi kwani mifumo ya sasa haiwezi kutupatia viongozi wa haki na kweli’?” amehoji Askofu Pisa.

Akizungumza katika mkesha wa Pasaka uliofanyika Kanisa Kuu la Mtakatifu Andrea Kagwa, Jimbo Katoliki Lindi, Askofu huyo amesema kuwa kama kurudi mezani ndiko kunakoweza kulinda amani, basi kila anayehamasisha hilo anapaswa kuungwa mkono, si kukandamizwa au kukamatwa.

“Kwa maana hiyo wote waliokamatwa kwa kudai haki, wakiwemo viongozi wa vyama vya kisiasa, waachiwe haraka na bila masharti, na wengine wasikamatwe wala kusumbuliwa. Pia mihimili isiingiliwe bali itende kazi zake kwa haki,” amesisitiza.

Amesema kuwa amani ni tunu adhimu inayopatikana kwa gharama kubwa, hivyo haipaswi kuchezewa, huku akisisitiza kuwa taifa linapaswa kuikataa dhana ya kuimba wimbo wa amani isiyotokana na haki.

Kauli ya Askofu Pisa imekuja wakati ambapo mjadala wa mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi na ushiriki wa vyama vya siasa umekuwa ukitawala anga ya kisiasa nchini, huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya vyama vya upinzani kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu kukamatwa kwa viongozi wao wakubwa akiwamo Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Tundu Lissu na ukosefu wa haki katika uendeshaji wa siasa.

unaiamru selikali utafikiri una bunduki>>..

kama kanisa lingekuwa limenyimwa haki ya kuabudu kwa uhuru hapo ungekuwa na sababu ya kuiamru serikali.hata hapo kanisani kwako hakuna haki kwa asilia mia moja
 
Hapa ndipo nasema nchi hii si chadema wala ccm. Yaani hakuna mwenye uvumilivu pale anapokutana na wazo tofauti la mwenzie.

Sasa kama huko chadema/tec hamuwezi kusahihishwa mpaka mnawaita wengine kenge, tukiwapa nchi halafu chauma wawakosoe, si mtatuchinja kabisa kama wanavyofanya wenzenu?

Kwa hekima ulitakiwa unieleweshe, badala yake umekuja na mtusi
Mtu anayesema Kuhamasisha Haki ni Udini huyo si kenge tu?

Yaani watu wanatekwa, Wanauwa, wanapotezwa. Mtu anaamka eti udini😀😀😀
 
Nadhini tatizo kubwa la sasa ni kamata kamata ya wanasiasa na utekwaji wa watu ambao ni tatizo la kijamii bila kujali dini
Tatizo liko kwenye Uthubu wa kutenda haki na utu, udini hauna nafasi.

Watu waliofeli kuongoza wanapwlenda kupandikiza ubaguzi kama ng'ao yao.
 
Ujumbe wa pasaka kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2025 kutoka kwa Rais wa Baraza la Maaskofu wa katoliki Tanzania (TEC).

Roma locuta, causa finita (Roma ikisema, mjadala umefungwa) comment ziwe fupi fupi mimi sitoshiriki uchaguzi kama maagizo ya viongozi wangu wa dini hayatafanyiwa kazi
 
Attachments

The colonial GOD will never save us!
 
unaiamru selikali utafikiri una bunduki>>..

kama kanisa lingekuwa limenyimwa haki ya kuabudu kwa uhuru hapo ungekuwa na sababu ya kuiamru serikali.hata hapo kanisani kwako hakuna haki kwa asilia mia moja
The Church system is never democratic, it is an autocratic by design, how

can they preach democracy?
 
Napenda haki, haki ilianza kuhuburiwa na CUF tangu miaka 1995, na ndiyo ilikuwa sera na slogan kuu!

Lakini NINYI mlikebehi dhana hiyo, mkawapiga vita CUF kuwa wanahamasisha ugaidi, mara dini na siasa! Simply kwa kuwa RAIS alikuwa ni mkristo mkatoliki!

Alivyokuja Kikwete mkamsumbua, akaanzisha mchakato wa katiba na reforms nyingi mpaka CHADEMA waliwez kupata wabunge zaidi ya 50! Mkamuiya DHAIFU mnahitaji dikteta!

Mungu akajibu maombi yenu akamleta aliyemleta! Tangazo la kwanza katiba mpya sio kipaumbele chake, haki haikuwa kipaumbele chake na Uchafuzi wa kura ukaasisiwa kwa kiwango cha kutisha!

Ninyi mkakaa kimya Kisa ni mtoto wenu!

Sasa mnaibuka na hoja ile ile ya haki!

Mnaijua HAKI? MNAPENDA HAKI ?

Haki ni zao la uadilifu na nyinyi hamuwezi kuhesabiwa kuwa ni waadilifu!

Hiyo mikwara yenu pelekeni kwenye vigangwe vyenu huko! Hakuna anayewaogopa!
Andiko lako limeelezea kwa uhalisia na ufasaha siasa yetu kama Nchi kuna Double standard kubwa

Hao wanao dai haki kuna muda walikuwa wadogo kwa hayo hayo wanayo yataka leo, ni kweli kama nchi tunapaswa kuwa na katiba mpya ili kujibu changamoto za kisasa lakini agenda hii na hizo za haki, hawa sijui TEC sijui nini wanazitoa kwa uwazi na shinikizo kipindi Rais ni wa Imani nyingine

Ndo maana kuwasikiliza au kuwafata hawa hata kama kwa juu inaonekana ni ombi jema lkn chini yake kuna hila na hawana huo uadilifu, ukiwa wa imani yao wana kukaanga kidogo lkn ikiwa imani sio yao wana kusurubu na hakuna rangi hautaona hawa nao wana tuharibia sana nchi hii

TEC na wachungaji wa kilokole kama kina Gwajima kwa juu wanasema mambo ya haki na katiba na ukiona ni mambo mema sema shida ni uadilifu wao unachagua nani kakalia ofisi kuu nao ni wale wale tu ni unafiki kwenda mbele wanahubiri haki, uadilifu na amani akiwa sio mtu wao lkn kwa mtu wao wanafumbia fumbia macho mambo mengi hawa nao ni tatizo na wanafiki tu kwa Taifa hili

Mfano kuna kauli aliisema Gwajima kwamba anatamani Madrassa ( sehemu ya vijana/watu wa dini ya kiislam kupata mafundisho ya dini yao) iwe Sunday school ( sehemu ya mafundisho ya vijana/watu wa imani ya kikristu) sasa mtu kama huyu anakuwa na hoja nzuri lkn tayari chini katanguliza imani yake na ibaguzi na hapo ndo inakua ukakasi kwa sie watu huru

Mfano mwingine , Chadema inaweza kuwa na sera nzuri na inapambania mambo mazuri lkn ni chama chenye structure mbovu na sehemu kubwa hasa viongozi wote waandamizi ni wa imani moja inakua hakiwakilishi mazingira ya nchi yetu na tena afadhali muundo (structure) wa CCM na ubaya wao lakini ni jumuishi kwa makundi,maeneo na imani mbalimbali

Chadema inakua kama kigango maana kina Lema ni ku quote vitabu vyao vya dini tu,
humo ni tumsifu nani sijui kwa kwenda mbele , sasa inawakwaza watu huru hata kama sera ni sahihi, set up ya nchi hii inataka ujumuishi na hasa kwa chama cha Siasa,

Hata kama Chadema wakija kuchukua Nchi watateswa na hii structure yao na wataibua upinzani mwingine
 
Udini utakuacha ukiwa maskini wa mali na roho. Achana na huo utumwa ndugu ukombolewe

Pinga hoja zangu usitumie hiyo sijui udini nacho sema kama Chama Tawala kilivyo tuletea shida pia hawa nao ni tatizo kwa amani yetu kama nchi na list hapa chini

1)Samia/CCM hawa kwa kukumbatia mifumo ya kizamani isiyotaka mabadiliko na kujibu changamoto za kisasa ndo imeleta balaa na shida hii na kutuingiza hata sie ambao hatupo kwenye Dunia yao ya kupigania madaraka, nguvu na vyeo

2)Lissu /Heche (Chadema) hawa ni vinara kwa kutaka mabadiliko , lakini wapo tayari kutumia hata njia za porini za ubabe na vitisho kwa mtaji wa vijana masikini na wasio na elimu kubwa na yote haya kwa faida yao ya Kisiasa na ni mabingwa wa ku manipulate ili mambo yao ya kupata nguvu (power) yatimie hata tukifa kwao ni sawa tu

3)Wanaharati kama Mange , Maria Sarungi hawa kwa kutaka kuleta mabadiliko wanashawishi kwa kila njia bila kuangalia upeo na ufahamu wa kundi lao hilo na mamlaka za dola (polisi na waandamanaji akili yao moja) na mwisho wake ni kuleta vurugu na uharibifu mkubwa na kupoteza maisha ya vijana wengi achia mbali matumaini waliyo yatoa sijui watalindwa na kina nani kama wakitoka kwa wengi

4)Baadhi ya Wachungaji (Gwajima na wengineo ) na TEC hawa nao ni tatizo jingine kuna muda wanaelezea mambo mazuri yanayotakiwa kufuatwa lkn nyuma ya kauli zao kuna ka uchochezi na wanakua wamechukua ka upande kwa faida wanayoijua wao iliyojificha badala ya kujikita kuhubiri utengamano na umoja

Na kama kutakuwa na tume huru ya uchunguzi hawa wote nilio wa orodhesha wachunguzwe kwa vifo, vurugu na machafuko yaliyotokea maana walihamasisha kwa namna moja ama nyingine yaani direct na indirect kwa kilichotokea

Na bado wanaoenekana kutuletea matatizo mbele ya safari kama hawatabadilika wote wamenyanyua silaha kumuumiza mtanzania kwa maslahi yao wanayoyajua wao

Tafadhali ICC anzieni kwa hawa kwa uchache hapo juu na hasa nilio wataja kwa majina maana hata mzozo wa Palestine mmetoa hati ya kukamatwa upande wa watu waandamizi kwa Israel na kwa Palestine na hapa iwe hivyo hao wa chama tawala , wapinzani na wanaharakati wote sukuma ndani, ni janga kwa Taifa letu hawa
 
Back
Top Bottom