Baraza la Iddi: Mahakama ya Kadhi ni suala la Waislamu wenyewe - Kikwete

1. Dodoma Secondary

2. Kizunguzi Secondary

3. Kondoa Secondary

4. Kwamire Girls

5. Hijra Secondary

6. Takwa Secondary

7. Jabal Hila Secondary

Hapo namba sita kama unamisha ile ya Mwanza bado iko mikononi mwao pamoja na Thaqhafa.

Kwa maneno hayo ya jk waislam hakuna haja tena ya kuipa kura ccm na wala ccm haitaji kura za waislam!

On a positive note kuhusu swala la shule kurejeshwa kwa wahusika siliafiki kwani mimi ni liberalist (yaani naamini uhuru wa mtu) sidhani kama ni sahihi kurudisha shule kwa viongozi wa dini halafu ziendeshwe kidini kwani utawanyima haki watoto wengine wasioko katika dini husika. Kwa mfano wahindu na wapagani nao wakoseme wapi zikirudishwa shule kwa taasisi za kidini?

On a negative side nasubiria nisome kwa ufasaha speech yake kuhusu suala la mahakama ya kadhi kwani halieleweki anapopakusudia ni wapi. Kikubwa naweza kusema anasupport kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi ila je ni mahakama ipi anayoitaka yeye nasubiria speech yake niisome kama unayo tunaomba utuwekee. Ila nimeongea na baadhi ya viongozi wa waislamu hapo mjini kwakweli hawakufurahishwa na tamko hilo sasa sijui kama hawakufurahishwa kweli au ushabiki we will see ila nawasiwasi CCM inaelekea kufa kabisa kwani ngome yake kuu ni kwa waislamu kupitia bakwata na wakiipoteza hiyo I guarantee CCM inaanguka kwa kupoteza kura maeneo yote ya pwani, kusini na katikati na magharibi mikoa ya Tabora, shinyanga na Kagera na Kigoma. Sasa ukiangalia na nguvu ya Chadema kaskazini CCM 2015 inaanguka sijui wacha nisubiri statement yake in writing .

Uko right katika mtazamo wako kuhusu shule ila hata mimi kwenye mahakama ya kadhi bado nafikiri kwa kuongea vile ndo moto utaanza tena kuwaka kwani ni kweli Masheikh wamechukizwa kwa kitendo cha JK kutotaka kodi za waTZ kuendesha mahakama ya kadhi pamoja na kuinyima meno kinyume na matarajio ya waislam. Sina hiyo speech ila nafikiri kuna watu watakuwa nayo au itawekwa kwenye mtandao wa BAKWATA

leo kikwete kaamua kusema na kutoa hotuba kama rais wa nchi na kwa kweli kwa hotba ya leo nadhani itarudisha heshima yake iliyoanza kupotea. na ameweka bayana masuala ya kadhi, ,maana wengi wa waislamu, ambao hata wengine waridiriki kusema amewaahidi kuwaachia mahakama ya kadhi ikiwa inasimamiwa na serikali, leo kawaweka bayana.

Ni kukosa vipaumbele, tatizo waislamu hata wakirudishiwa shule wanazodai..... kama zipo watazigeuza zote madrasa....

Aliyekufikisha hapa, hawezi kukutoa hapa.
Hii ni formula rahisi na inayojulikana duniani kote.
Aliyekuingiza kwenye tope, hawezi kukutoa!

leo kikwete kaamua kusema na kutoa hotuba kama rais wa nchi na kwa kweli kwa hotba ya leo nadhani itarudisha heshima yake iliyoanza kupotea. na ameweka bayana masuala ya kadhi, ,maana wengi wa waislamu, ambao hata wengine waridiriki kusema amewaahidi kuwaachia mahakama ya kadhi ikiwa inasimamiwa na serikali, leo kawaweka bayana.

Natofautiana na wewe hasa hapo kwenye red. Kama aliwaahidi waislamu mahakama ya kadhi alafu amewageuka bila kuomba radhi bado ni tatizo. Kwavile "maneno" yake yameridhisha percent fulani ya watu haimaanishi kitu kwasababu: bado matendo ni tatizo kwenye uongozi wake. Inawezekana deliverance ya speech ni nzuri i.e. imeku-wa delivered ikaeleweka lakini kwa mtizamo wangu, that does not add anything kwenye utendaji wa Kikwete. Ni sawa sawa leo aende Mwanza wamuulize mbona Mwanza haijawa kama California alafu awaambie it is impossible angalieni ramani ya jiji, resources etc. Haimaanishi hajaongea point lakini aliahidi; hivyo anawajibika kwa kile alichoahidi mwanzo (accountability). Either 1.)aliwadanganya akawafanya mtaji wa kujipatia kura (more likely) or 2)alifikiri itawezekana na sasa baada ya kushauriana na watu fulani fulani na kuangalia kwa undani ahadi alizowapa ameona haliwezekani (less likely). Kwa mtizamo wangu alitakiwa aombe msamaha ndio aeleze why realistically mpango A, B, etc hauwezi kufanikiwa kinyume cha hapo ni yale yale yakuachana kwenye mataa.

Njozi ipi?

Mwembechai au Islam and the state?

Hasa Mwembechai; kwa sababu kwa kiasi kikubwa ameonesha kile ambacho serikali ya CCM haikutaka wananchi wakijue kuhusiana na uhusiano wake na masuala kadhaa ya Waislamu - na hapa nazungumza kwa ujumla tu. Nashukuru niliwahi kufanya naye mahojiano ya kina sana kuhusu kitabu chake hicho.

Lakini katika hili pia kuna suala la hekima. Sidhani - katika kufikiri kwangu - ilikuwa ni proper channel kuwateremshia Waislamu jambo hili siku ya Idi na kwa namna ya kisiasa jinsi ilivyotolewa.

• Thanks
Reactions: FJM
Nafuatilia hotuba ya mh raisi kikwete kwenye baraza la iddi kuoitia tbc 1.

Kwa kweli amejitahidi kuainisha ukweli wa mambo hususan katika sekta ya elimu,

japo naona kuna ma ustaadh wanamuangalia kwa roho mbaya kweli

hasa hasa anaposema baba wa taifa hili mwalimu nyerere alitaifisha

shule zote za dini na mashirika ziwe za serikali ili elimu itolewe bila ubaguzi.

Kudos j.k

n.b:

Mimi ni chadema, ila kiongozi wa ccm akisema jambo likanigusa hakika sitaacha kumfagilia.

Siasa sio uadui na kuona maovu ya mwenzako tu bila kuona mazuri wajameni.

Ninaona ile mikoba ya Yahaya inaelekea baharini. Sasa yuko huru.

Hakika leo JK ametoa hotuba ambayo mi binafsi imenifurahisha kuanzia mwanzo mpaka mwisho.Ila nina wasi wasi kuwa huenda haikupokelewa vizuri na viongozi wa dini ya kiislamu kwani hawakuonyesha sura za furaha.

YEYE MWENYEWE,KAONA NYUSO ZAO,AKASHTUKA,AKASEMA NAJUA HAMTAFURAHIA MANENO HAYA LAKINI NDO UKWELI!Amekuwa kinyume na kila jambo waliloomba kwenye hotuba yao.kuanzia la kurudishiwa shule mpaka la kadhi.lakini alichokiongea ndo ukweli wenyewe.

Tuache Unafiki na udini, Kwanini jk tumsifu kwakuwa amewararua waislamu?
Anapofanya hivyo kwa mapadri mbona alipondwa?

Gadafi amekuwa akitoa misaada mingi Afrika na Tz ,ila sijawahi sikia amesaidia kujenga shule au chuo,kwanini Bakwata hakumshawishi Gadafi awajeenge shule kuliko kudai shule ambazo kiuhalisia ni chache sana..!

Mkuu ndani ya Bakwata hakuna mtu mwenye nia ya kuendeleza Uislamu na Waislamu, wengi ni wachumia tumbo tu, wazo la ujenzi wa shule watalitoa wapi? wanachowaza ni namna ya kuuza nyumba za wakfu, kuomba misaada ya tende ili nazo waje wauze na kusubiri mbuzi wa sadaka toka Saudia ili wagawane wao na jamaa zao!!!

Tuache Unafiki na udini, Kwanini jk tumsifu kwakuwa amewararua waislamu?
Anapofanya hivyo kwa mapadri mbona alipondwa?

Unapotaka kuwa mtu mwenye mawazo huru sharti ukubali lawama kama unazotoa. Mkuu si kwa sababu amewararua waislam bali kwa sababu ameongea pointi na angeongea popote tunge fagilia tu.

Gadafi amekuwa akitoa misaada mingi Afrika na Tz ,ila sijawahi sikia amesaidia kujenga shule au chuo,kwanini Bakwata hakumshawishi Gadafi awajeenge shule kuliko kudai shule ambazo kiuhalisia ni chache sana..!

simba ingrishy noti lichabo, gadafi kiswazi not availebo

Back
Top Bottom