Baraza Kuu Taifa CWT mpo wapi? Zungumzeni watu wajue mbivu na mbichi

Oct 13, 2018
35
259
BARAZA KUU TAIFA CWT MPO WAPI? ZUNGUMZENI WATU WAJUE MBIVU NA MBICHI

Na Thadei Ole Mushi.

Inashangaza Misalaba anapata wapi nguvu ya kuzuia account za CWT zisifanye kazi wakati chombo cha juu kabisa cha chama Baraza kuu likiwepo. Hiyo Nguvu Misalaba aliyonayo inatoka wapi ndio ya kudili nayo kwanza na kwa uwezo wa Mungu Baraza Kuu taifa Mnaenda kushinda hii vita.

Eti kwa sasa Shughuli za Chama zote haziendi kisa Watu watatu waliopo nje ya mfumo wa CWT kwenda kuzuia bank zisitoe fedha za Uendashaji wa Chama!!!!

Kwa mujibu wa katiba ya CWT kwa sasa chombo cha juu chenye maamuzi na sauti ya Mwisho ya kusema ni Baraza kuu la Taifa.

Tulishukuru Baraza Kuu la Taifa hadi hapa lilipofikia kwa kufanikiwa kuzima kila aina ya mapinduzi yanayoratibiwa nje ya Chama.

Narudia.

Mgogoro uliopo CWT hautokani na Ugomvi kati ya Mwalimu na Mwalimu. Ugomvi ukiopo kiini chake ni watu waliopo nje ya mfumo wa ualimu (Viongozi) wa Serikali kutumia mabavu na nafasi zao kuendelea kuinyonya CWT.

Kwa maana hiyo Baraza kuu la chama Taifa kuna jambo moja tu hamjatusaidia sisi wanachama kukifanya. Kutokana na ukubwa wa Chombo chenu Baraza, kutokana na uzito wa majukumu yenu kama Baraza, tusaidieni sisi wanachama kufahamu nini kinaendelea ndani ya CWT.

Baraza kuu kwa kutumia katiba ya chama ibara ya 23 h ndio mliofanya maamuzi ya kuwasimamisha kina Misalaba na wengineo kujihusisha na shughuli za chama kwa sababu mlizoona zinafaa.

Ni wakati wenu sasa kumalizana na kazi mliyoianza kwa kuviita vyombo vya Habari kuwaelezea sababu za kuwasimamisha, sababu za kina Deus kuwa nje ya uongozi wa Sasa na kwa nini Wanachama wanahisi kuwa kuna viongozi wa Serikali wanaokivuruga chama bila sababu. Baraza kuu lina majukumu mengine makubwa ya uidhinishaji wa Fedha za chama, mpaka sasa Baraza halijasema popote kwa nini waliotuhumiwa kutafuna fedha za kofia 2021, hawajachukuliwa hatua, baraza halijafafanua chochote kuhusu Fedha za mabati zilizoliwa na viongozi waliopita na madudu mengine ambayo jamii inatakiwa ifahamu.

Kwa kufanya hivi mtakuwa mmemsaidia kwanza Rais wa Nchi kufahamu nini kinaendelea ndani ya CWT.

Ifahamike kuwa migogoro ya CWT mpaka sasa imeshafika mezani kwenye mashirika ya kimataifa kama ILO, UNESCO na mengineo mengi.

Kitendo cha Mashirika haya kuanza kuandika kuhusu Serikali kuingilia Shughuli za CWT ni kuichafua taswira nzima ya uongozi wa Mama Samia bila sababu za Msingi.

Tukumbuke Rais Samia ameijenga Demokrasia ya nchi kwa gharama kubwa, kwa jasho na Damu na huko nje taasisi mbalimbali zimeshaanza kumfikiria Rais Samia kumpatia tuzo za Heshima za kimataifa kwa uongozi wake uliotukuka.

Nina Imani Rais akisikia kutoka Baraza kuu taifa atapata picha halisi ya nini kinaendelea kwenye chama chetu. Yapo mengi ya kuzungumza, zipo jinai nyingi za kuweka hadharani na kikatiba mna jukumu hilo kwa sasa.

Viongozi wa Serikali waliojishika na CWT kwa sasa sio wakati mzuri sana, waungwana husema ukitaka kuachana na msururu wa Inzi tupa kibudu ulichokibeba. Kuna watu hawabebeki tena, kuna watu kwa Makusudi ya Mungu hata kama hawana fedha na Mali Mungu huwinda wasionewe.

Mfalme Daudi alikuwa na wake 99 lakini hakutosheka alimtamani mke wa Askari wake akafanya njama hadi akafa ili amuoe tu lakini baada ya azma yake hiyo kutimia alijutia maisha yake yote.

Kuna viongozi wana Kila kitu kwenye Maisha yao, lakini kidogo cha wengine wanakitaka nacho wakichukue, Hili neno linaenda kusimama kwenye hili hawatatoka salama.

Ole Mushi
0712702602
 
Back
Top Bottom