DOKEZO Barabara za Mitaa jimbo la Segerea ni mbovu, zinajaa maji na hazina mitaro

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Aug 31, 2022
54
99
Naenda moja kwa moja kwenye hoja yangu. Kuna vitu vinafanywa na Serikali vinakera sana. Mfano. TMA walitangaza zaidi ya miezi miwili nyuma kwamba kutakuwa na Mvua kubwa za e El Nino ambazo zitaendelea hadi mwezi wa 3 mwaka 2024 lakini Serikali ilitulia bila kufanya Marekebisho ya Barabara zake kwenye Mitaa mbalimbali

Hatimaye mvua zimeanza na Barabara nyingi kwenye maeneo mengi hasa jijini Dar sala Salaam zimejaa Maji yaliyotuama kwasababu hakuna Mitaro, zimejaa Mashimo, wananchi wasio na vyombo vya Usafiri wanalazimika kuvua Viatu na kutembea katika Madimbwi ya Maji machafu wakiwemo Watoto wanaokwenda Shule.

Nimepita maeneo mengi kwenye Jimbo la Segerea, Barabara hazifai na Mbunge Bonnah Kamoli yupo tu hata hazungumzii kero hizo. Nimeenda ofisi za kadhaa za Serikali za Mitaa mfano Mtaa wa Mfaume barabara ya Mangumi haijawahi hata kupitishwa Magreda ya kukwangua tu kusawazisha.

Maafisa wa Serikali za Mtaa wenyewe wanalalamikia Serikali Kuu ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutochukua hatua licha ya kufikishiwa kero za ubovu wa Barabara kwa muda mrefu.

Nashauri wenye Mamlaka kutatua shida za Wananchi mapema na sio kusubiri hadi nyakati za Uchaguzi zikikaribia Wagombea waje kuwahadaa Wananchi kwa kuomba Kura wakiahidi kushughulikia matatizo yaliyodumu kwa muda mrefu.


Soma >> Waziri Bashungwa atoa maelekezo kwa TANROADS kukarabati mifereji, Novemba 7, 2023
 
Huyo Bona Kamoli mara hii 2025 asijaribu kuomba ubunge jimbo letu la Segerea. Watu wa Tabata Kisukuru kuanzia Maji chumvi, Kwa Swai, Tabata Kimanga yote hatutaki kumsikia atuachie jimbo letu. Tutachagua hata jiwe ili mradi Tumebadilisha mbunge.
 
Dsm iko hivyo mitaa mingi, suala la mitaro wala hawahangaiki nalo. Hizo barabara wanazochonga kila kukicha zinaharibika sababu ya kukosa mitaro na makaravati.

Mvua kidogo tu maji yanakatisha barabarani na kukata barabara, kuna muda unajiuliza sisi ni watu wa aina gani, na hii ni DSM jiji linalotakiwa kuwa la mfano, sasa hayo maendeleo kwa nchi nzima yatakuja lini?
 
Wananchi vitu ningine kama kuchimba mitaro mnafanya hata nyinyi sio mpaka msubirie Serikali.

shauri yenu
 
Huyo Bona Kamoli mara hii 2025 asijaribu kuomba ubunge jimbo letu la Segerea. Watu wa Tabata Kisukuru kuanzia Maji chumvi, Kwa Swai, Tabata Kimanga yote hatutaki kumsikia atuachie jimbo letu. Tutachagua hata jiwe ili mradi Tumebadilisha mbunge.
Utashangaaa anapita

Ova
 
Back
Top Bottom