KERO Barabara za Jimbo la Kibaha Mjini (Pwani) hali ni mbaya, mvua ikinyesha Wananchi wanateseka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049

photo_2024-01-21_12-47-31.jpg
Hivi ndivyo ilivyo maeneo ya mitaa ya Kibaha, Maili Moja Mkoani Pwani, mvua zikinyesha tu basi miundombinu hasa barabara hazipitiki kirahisi kama hivi inavyoonekana.

Mbunge wa Jimbo hilo la Kibaha Mjini ni Silvestry Fransis Koka ambaye amekuwepo katika nafasi hiyo kwa muda mrefu lakini suala la barabara kwenye Jimbo lake ni changamoto tena changamoto hasa.

Kuna ndugu yangu anaishi Maili Moja hapo pichani na kwenye video ni Mitaa ya Muheza hapohapo Maili Moja, wanasema kila mvua ikinyesha basi mambo yanaharibika.

Nimeuliza kwa wenyeji kuwa kama Mbunge wao huwa anafika wanasema anafika kwa nadra, akifika ahadi na porojo zinakuwa nyingiiii wakati Wananchi wake wanateseka na barabara kila uchwao.

Nasikia kabla hajaenda huwa anauliza mazingira ya mvua kwanza kama imenyesha au ina uwezekano wa kunyesha, akigundua imenyesha au kuna dalili huwa haendi kwa kuwa ukienda na usafiri mitaa hiyo na mvua ikikukuta hauwezi kurudi ulipotoka.
photo_2024-01-21_12-47-34.jpg

photo_2024-01-21_13-07-39.jpg
 
Back
Top Bottom