Barabara ya Ujerumani kupewa jina la mwanaharakati wa Tanzania, Lucy Lameck. Alikuwa Waziri wa 1 mwanamke wa Tanzania

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
17,369
33,015
_115663504_6e784af5-43e1-4dc0-8d9d-43e0c4f4d3f3.jpg

Barabara hiyo ya Wissmannstraße inatarajiwa kubadilishwa jina mwaka ujao

Madiwani katika mji mkuu wa Ujerumani , Berlin wamepiga kura ya kuondoa jina la barabara moja linalompatia heshima gavana mmoja wa nyakati za ukoloni katika eneo la Afrika mashariki aliyeshutumiwa kwa kuagiza mauaji na kuweka jina la mmoja wa wanaharakati wa kupigania uhuru nchini Tanzania.

Barabara ya Wissmannstraße, iliopatiwa jina la Hermann von Wissmann, sasa itaitwa Lucy-Lameck-Straße.

Alikuwa waziri wa kwanza mwanamke nchini Tanzania pamoja na kuwa miongoni mwa viongozi maarufu katika vuguvugu lililopigania uhuru wa taifa hilo.

Von Wissman alikuwa gavana wa taifa la Ujerumani Afrika mashariki ambayo kwasasa ndio mataifa ya Tanzania , Burundi na Rwanda katika mwisho wa karne ya 19 na anadaiwa kuwa chanzo cha mauaji ya wakaazi wengi limetangaza gazeti la Ujerumani, Der Tagesspiegel .

Kundi la Berlin Postkolonial, mojawapo ya kundi lililohusika na mabadiliko liliunga mkono hatua ya serikali hiyo ya mtaa.

Katika taarifa lilisema kwamba kampeni hiyo ilizuia kuheshimiwa kwa ''Von Wissmann na mahala pake kuchukuliwa na mwanamke Mtanzania ambaye alipinga ukoloni na ubaguzi wa rangi''.
"Wissmann alikuwa mbaguzi na muhalifu wa kivita .

Lucy Lameck anawakilisha mchango ulioshushwa thamani wa wanawake wa Tanzania waliopigania uhuru wa taifa hilo'', alinukuliwa akisema mwanaharakati wa Tanzania Mnyaka Sururu Mboro.

 
Mji wa Berlin kuupatia mtaa mmoja jina la Mtanzania.

Madiwani katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin, wamepiga kura kukubali kuubadilisha mtaa mmoja wa mji huo kuwa na jina la Mwanaharakati Mwanamke wa Tanzania, kuchukua nafasi ya jina la Mtaa wa Wissmannstraße, ambalo linatokana na jina Hermann von Wissmann aliyekuwa Gavana wa koloni la Afrika Mashariki anayetuhumiwa kuamuru mauaji na mmoja wa Wanaharakati wa Kike wa Uhuru wa Tanzania.

Lucy Lameck mzaliwa wa Kilimanjaro alikuwa Waziri wa kwanza wa Mwanamke wa Baraza la Mawaziri nchini Tanzania na pia kama kiongozi wa harakati za uhuru. Von Wissman alikuwa Gavana wa Afrika Mashariki ya Ujerumani (sasa ni Tanzania, Burundi na Rwanda) mwishoni mwa karne ya 19. Gazeti la Ujerumani la Der Tagesspiegel limeripoti kuwa Gavana huyo anaaminika kuhusika mauaji ya umati ya watu wa eneo hilo.

Kutokana na hali hiyo kulikuwa na kampeni iliyozuia "kuheshimiwa zaidi" kwa Von Wissmann na badala yake kuweka "Mwanamke wa Kitanzania ambaye alipinga kikamilifu ukoloni na ubaguzi wa rangi". Mtaa huo sasa utaitwa Lucy-Lameck-Straße.

Chanzo cha Habari CRI Kiswahili
 
Tanzania hasa Tanga ina historia kubwa sana Ki dunia sema ndio hivyo we are a sleeping Giant.

Rais wa Mwisho wa South Africa ya Makaburu alizaliwa Tanga.

Malkia Elizabeth alitangazwa kuwa Malkia wa Uingereza baada ya kifo cha Baba yake 1952 akiwa anazuru Ziwa Victoria.

Viongozi kadhaa wa Kitaifa wa Ujeruman wamezaliwa Tanganyika.

Viongozi kadhaa wa Kiafrica wana historia kubwa sana na Nchi yetu. Mf Watoto wa kwanza wa 3 wa Museven wote wamezaliwa Tanzania

Lakin cha kusikitisha Nchi yetu hasa miaka ya karibuni imejizika kabisa.

Kuna Mwaka nilikuwa Nchi moja ya Kusini mwa Jangwa la Sahara sasa tukaingia mitaani tukawa tunafanya shopping huku tunapiga story na wenzangu, yule Muuza Duka akawa interested na lugha yetu akatuuliza lugha gani hii na ya wapi tukamjibu, cha kushangaza eti haijui Tz hadi alipo google akajijibu ooh its Ngorongoro.

Publicity yetu tunaifanyia Tandale na Hadi Nyakanazi si zaid ya hapo.
Hapo mjini Cologne kuna Usambara Strabe na mbele kidogo kuna TangaStrabe. Nafikiri kwa ujerumani sio kitu kigeni sana kuona mitaa yenye majina yenye asili ya Tanzania
 
Madiwani katika mji mkuu wa Ujerumani , Berlin wamepiga kura ya kuondoa jina la barabara moja linalompatia heshima gavana mmoja wa nyakati za ukoloni katika eneo la Afrika mashariki aliyeshutumiwa kwa kuagiza mauaji na kuweka jina la mmoja wa wanaharakati wa kupigania uhuru nchini Tanzania.

Barabara ya Wissmannstraße, iliopatiwa jina la Hermann von Wissmann, sasa itaitwa Lucy-Lameck-Straße. Alikuwa waziri wa kwanza mwanamke nchini Tanzania pamoja na kuwa miongoni mwa viongozi maarufu katika vuguvugu lililopigania uhuru wa taifa hilo.
Von Wissman alikuwa gavana wa taifa la Ujerumani Afrika mashariki ambayo kwasasa ndio mataifa ya Tanzania , Burundi na Rwanda katika mwisho wa karne ya 19 na anadaiwa kuwa chanzo cha mauaji ya wakaazi wengi limetangaza gazeti la Ujerumani, Der Tagesspiegel.

Kundi la Berlin Postkolonial, mojawapo ya kundi lililohusika na mabadiliko liliunga mkono hatua ya serikali hiyo ya mtaa. Katika taarifa lilisema kwamba kampeni hiyo ilizuia kuheshimiwa kwa ''Von Wissmann na mahala pake kuchukuliwa na mwanamke Mtanzania ambaye alipinga ukoloni na ubaguzi wa rangi''.

"Wissmann alikuwa mbaguzi na muhalifu wa kivita . Lucy Lameck anawakilisha mchango ulioshushwa thamani wa wanawake wa Tanzania waliopigania uhuru wa taifa hilo'', alinukuliwa akisema mwanaharakati wa Tanzania Mnyaka Sururu Mboro.

Chanzo: BBC Swahili
 
Back
Top Bottom