Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,019
- 142,905
Watanzania hatutaendelea maisha yetu yote, labda wajukuu wa wajukuu zetu ndio wataanza kuleta maendeleo ya kweli.
Utakuta hapo contractor Mtanzania, client Mtanzania, consultant Mtanzania. Wote wizi, waongo, wazembe, wala na wapokea rushwa.
Kuna kuendelea hapo?
Inashangaza sana, engineer Mtanzania anapima ana design barabara yenye ubora wa hali ya chini, ili iweje? na ma consultant wanakubali na ilhali wanaona, wamesoma na wanajuwa kuwa hii barabara inajengwa chini ya kiwango, wanalishwa kitu kidogo wanapitisha certificates za uongo, na mkaguzi wa mwisho anakuja kuipitisha, utakuta huyu kaajiriwa pale wilayani kama district engineer, anapewa kitu kidogo nae anapitisha.
Hii nchi wanataka Rais aje kuwakagua mpaka chupi wanazovaa, kama wanavaa, kama ziko safi au chafu.
Inaudhi sana.
Nnasema Tanzania ni wakati muafaka kuanzishwa sheria ya kuuwa watoa na wapokea rushwa, bila hivyo tutalalamika usiku na mchana hakuna tija.
Pointi tupu!