Ni muhimu kufahamu/kujulishwa facts ulizoulizia........however...mleta mada ambaye pia ni mtumiaji wa barabara hiyo regularly...anasema hata mwaka haujapita......crack za wazi kabisa na potholes zimejitokeza......either material yalikuwa sub-standard au poor workmanship and compaction.......hii ni dhahiri kuwa quality control and assurance.....ilikuwa na walakini.......hebu watupatie test results record za hiyo barabara....ili akina
Sikonge na
Lole Gwakisa watusaidie na assessment zao.......
Mkuu
Ogah huwa napita maeneo yaliyotajwa mara nyingi tu.
Na kama alivvosema mtoa mada, barabara hii bila kuficha iko chini ya viwango vya ujenzi, na ndio maana tunaona matatizo kujitokeza katika kipindi kifupi tu, toka kukamilika kwa ujenzi.
Tatizo linaweza kuwa katika design, workmanship na hata supervision ya mkandarasi.
Kitu kinachoonekana dhahiri ni ile layer the juu ya lami.
Ile layer ya lami ni ndogo mno, kwa macho tu haizidi 15-20mm, wakati standards za urban asphalt concrete roads inatakiwa kuwa 50mm(na definately si chini ya 30mm).
Kwa layer ndogo namna ile sijui wa kulaumu nani, aliye design, aliyejenga au aliye supervise kazi hiyo.
Matokeo ni yale yale-kazi mbaya.
Ni kweli katika hili msema kweli ni Core drilling ili hiyo core ikafanyiwe test na kujua tatizo likowapi.
Najua mkandarasi aliyejenga hapo ni mzawa, lakini ni kazi kama hizi zinazoumiza jina la wkandarasi wazawa, na kuondoa imani ambayo imeanza kujengeka.