Barabara ya Mabatini, Kijitonyama: Nani kala 10%?

Barabara ya Mabatini, Kijitonyama: Nani kala 10%?

Dahh inaniumiza sana kuona upuuzi unaoendelea nyumbani..........hizi barabara zote zirudishwe Ujenzi kwa ajili ya administration.....hawa Madiwani kwenye halmashauri wanaua uchumi wetu mchana kweupe.......
 
Mkuu huko halamshauri, hela ya ujenzi wa barabara ni chakula cha wanasiasa.
Na mpaka hivi sasa hakuna tamko lolote lilitolewa juu ya hii barabara mbovu ya Mabatini.
Kisa?
10% imetulia.
 
Mkuu. I wanted to post something like this a long time ago mkuu lakini kuhusiana na ile barabara tokea shule ya msingi k,nyama na kutokea mwananyamala that was poorly built, nilichukizwa kupita maelezo
 
Samahani kidogo wana JF, na GT. Hivi barabara hiyo mkataba wake kwa maana ya wearing course umesema nini! Je, ni Asphalt Concrete, Triple/Double/ Single surface dressing, Flexible/Rigid... Gravel or the like?
 
Hii tunaweza kuipigia kelele hapa hapa JF ili wahusika wapewe taarifa.. Invisible atusaidie kwa hili.......sio barabara hii tu...hata zingine zilizojengwa chini ya kiwango........sihitaji kuwa ENGINEER kuona wizi huu wa mchana kweupe.......hizi halmashauri ziko chini ya Wizara gani? Ofisi ya Waziri Mkuu?....
....kama ziko chini ya Waziri Mkuu......namshauri Invisible amuandikie PS Dr. Frolence Turuka ili aliangalie hili suala......Big Results Now....haimaanishi tufanye vitu chini ya viwango.......damn!.....kama kuna watu walipelekwa mahakamani kwa jengo kuanguka....basi na issue kama hizi tunataka kuona watu wanafikishwa mahakamani.....na ikiwezekana kufutiwa leseni zao za uhandisi....
 
Last edited by a moderator:
Nahisi barabara bado iko kwenye uangalizi wa mkandarasi hivyo atarudi ku repair. Kwa kawaida kazi za ujenzi zinakuwa na kipindi cha maangalizi/defect period. Ndani ya kipindi icho sehemu korofi zinajitokeza na kurekebishwa. Is not an issue of 10%.
 
Samahani kidogo wana JF, na GT. Hivi barabara hiyo mkataba wake kwa maana ya wearing course umesema nini! Je, ni Asphalt Concrete, Triple/Double/ Single surface dressing, Flexible/Rigid... Gravel or the like?

Ni muhimu kufahamu/kujulishwa facts ulizoulizia........however...mleta mada ambaye pia ni mtumiaji wa barabara hiyo regularly...anasema hata mwaka haujapita......crack za wazi kabisa na potholes zimejitokeza......either material yalikuwa sub-standard au poor workmanship and compaction.......hii ni dhahiri kuwa quality control and assurance.....ilikuwa na walakini.......hebu watupatie test results record za hiyo barabara....ili akina Sikonge na Lole Gwakisa watusaidie na assessment zao.......
 
Last edited by a moderator:
Nahisi barabara bado iko kwenye uangalizi wa mkandarasi hivyo atarudi ku repair. Kwa kawaida kazi za ujenzi zinakuwa na kipindi cha maangalizi/defect period. Ndani ya kipindi icho sehemu korofi zinajitokeza na kurekebishwa. Is not an issue of 10%.

....mazee...that is a very good point!....however, kwenye defect liability period hatutegemei kuona failure kubwa za aina hii.......hebu jiulize lifespan ya flexible pavement kama hii ni miaka mingapi kwanza......!
 
Nahisi barabara bado iko kwenye uangalizi wa mkandarasi hivyo atarudi ku repair. Kwa kawaida kazi za ujenzi zinakuwa na kipindi cha maangalizi/defect period. Ndani ya kipindi icho sehemu korofi zinajitokeza na kurekebishwa. Is not an issue of 10%.
Hiyo barabara ni ya kuirudia yote na si repairs kama unvyosema mkuu.
Barabara imechanika toka Afrika Sana hadi junction ya barabara ya kwend Uzuri.
Na mengi ya magari yanayopita hapo ni madogo, hii ni barabara ya mchepuko kupunguza traffic toka Bagamoyo Rd.
Nasema hapo 10% imetulia.
 
Tujadili hizo defect from both perspective( Design & construction)
Iteam of design: Hilo eneo water table hiko juu na hakuna wheep holes za ku drip underground water kutoka barabarani to side drainage. So maji Yana force kutokea ndani ya road kama inavyoendelea kujitokeza.
 
Kwa hiyo design na yenyewe ina walakin......ndio sababu wadau wanasema hizi 10% zinatuua....inawezekanaje Mhandisi mahiri ukaweka mkono/saini na mhuri wako kwenye design kama hiyo........huyo Mhandisi hana tofauti na yule aliyeruhusu sub-standard work kwenye zile nyumba zilizoanguka na kuua watu.......hai-ishii hapo tu...hata aliyesimamia na aliyejenga kazi na wao wana sehemu yao ya kulaumiwa...

...huyo Mkandarasi naye atakuwa ni Mkandarasi njaa kwa sababu atakuwa amekubali kujenga kitu sub-standard.....

Hii issue iwe reviewed in its totality......kila aliyehusika kwenye huu upuuzi awajibishwe kisheria.......
 
Watanzania hatutaendelea maisha yetu yote, labda wajukuu wa wajukuu zetu ndio wataanza kuleta maendeleo ya kweli.

Utakuta hapo contractor Mtanzania, client Mtanzania, consultant Mtanzania. Wote wizi, waongo, wazembe, wala na wapokea rushwa.

Kuna kuendelea hapo?
 
.....Yaani inauma na inaudhi sana.....yaani tunajiibia sisi wenyewe halafu tunabaki kulaumiana........
 
.....Yaani inauma na inaudhi sana.....yaani tunajiibia sisi wenyewe halafu tunabaki kulaumiana........

Inashangaza sana, engineer Mtanzania anapima ana design barabara yenye ubora wa hali ya chini, ili iweje? na ma consultant wanakubali na ilhali wanaona, wamesoma na wanajuwa kuwa hii barabara inajengwa chini ya kiwango, wanalishwa kitu kidogo wanapitisha certificates za uongo, na mkaguzi wa mwisho anakuja kuipitisha, utakuta huyu kaajiriwa pale wilayani kama district engineer, anapewa kitu kidogo nae anapitisha.

Hii nchi wanataka Rais aje kuwakagua mpaka chupi wanazovaa, kama wanavaa, kama ziko safi au chafu.

Inaudhi sana.

Nnasema Tanzania ni wakati muafaka kuanzishwa sheria ya kuuwa watoa na wapokea rushwa, bila hivyo tutalalamika usiku na mchana hakuna tija.
 
Watanzania hatutaendelea maisha yetu yote, labda wajukuu wa wajukuu zetu ndio wataanza kuleta maendeleo ya kweli.

Utakuta hapo contractor Mtanzania, client Mtanzania, consultant Mtanzania. Wote wizi, waongo, wazembe, wala na wapokea rushwa.

Kuna kuendelea hapo?
Hiyo nyekundu ni wezi sio wizi. Hii ni kwa sababu wewe ni mkosoaji mkubwa wa kiswahili humu jamvini. Halafu kingine wewe usijitoe akili, nyie sisiemu hapa hamuwezi kujitoa. Mmefanya nini kuwawajibisha hawa watu?
 
Unafikiri ma engineer wote ni CCM? wakandarasi CCM? Ma consultant CCM?

Punguani wahed.

Na wale wanaowauzia Mafuso chakavu mawili kwa millioni 600 ni CCM?

Kwenye makosa lazima pawekwe wazi na pakemewe, CCM siyo malaika kama aliwahi kusema Nyerere kuwa yeye si malaika na ana makosa yake kama binadam.

CCM ni chama na chama kina binadam hakina malaika. Kumbuka hilo.
 
Mimi nadhani mleta mada ameleta wazo ambalo lipo ziku zote kuhusu hizi barabara zetu na 10% juu yake.

Mimi ingawa sio mtaalam saana wa kujenga barabara lakini nafikiri kutokana na kujifunza kutoka kwa wenzetu walioendelea, nimeona kuna matatizo kuanzia kwenye wizara husika hadi pale TANROAD.

TANROAD akiwa wakala wa usimamizi wa barabara wana jukuu la kuhakikisha barabara zote hasa za mijini zina hali bora kabisa.

Kabla ya kujengwa barabara mpya inabidi wadau wote wahusishwe wakiwemo wataalam wa upimaji na ramani,wataalam wa mazingira, wale wa uchoraji na hata wataalam wa jiolojia inabidi washirikishwe, inawezekana pia kwamba lami haikai kutokana na wingi wa mchanga na sababu zingine.

Pia kabla barabara haijajengwa hadi itumike kunakuwepo hatua kadhaa ambazo zimechukuliwa ukiwemo upimaji, ubunifu na njia za mifereji ya maji machafu na mvua.

Kwa mfano kwenye uubunifu na uchoraji wa barabara hiyo kuna mambo ya kuzingatia kama vile eneo, ardhi na mteremko, uwezo wa kupitisha maji ya mvua na machafu, wingi wa magari, kiasi cha magari, malori na mabasi yakayopita hapo, uwezekano wa kuendeleza eneo hilo baadae kama vile maduka pembezoni mwa barabara hiyo( na sio kuruka kidaraja cha mbao kwenda dukani kununua mkate) na athari kwa mazingira na wananchi walio karibu na barabara hiyo.

Pia kuna suala la uwiano wa ardhi au Earthwork ambapo kunatafutwa ujazo wa barabara na uwiano wake na mifereji ya maji. Barabara yoyote ile lazima iwe na ujazo wa juu katikati ili kuwezesha maji yatiririkie kwenda kwenye mifereji hasa pale mvua inaponyesha na kuondoa maji hayo yasituame katikati ya barabara hiyo na kusababisha madimbwi na hatimae lami kumomonyoka.

Sasa hii barabara ya mabatini ni moja ya barabara za zamani sana na isingeweza kuwa katika hali hiyo iliyo nayo leo.

Mji wa Dar-es-Salaam bado kuna barabara nyingi tu zinahitaji kujengwa upya na pesa ya kufanya hivyo inaweza kuwepo kwenye makabrasha tu na sio pale hazina.

Lakini lawama inabidi ziende kwa manispaa ya Kinondoni kwani wao ndio wenye kujibu watatafuna vipi pesa za walipa kodi na wanagawana vipi na kwanini Wilaya hiyo yenye biashara lukuki inashindwa kujenga barabara nzuri na zenye hadhi?
 
Back
Top Bottom