You are very right hiyo bendera nani kaitengeneza? maanake hawa watu hawajawa organised kiasi cha kufanya mabadailiko kama haya.. Ni baraza gani lililoipitisha bendera hiyo? Hivi kesho yakitokea Mapinduzi Tanzania kisha kundi la waasi wakichukua madaraka wanaweza kubadilisha bendera ya Taifa letu na nchi zote duniani watalazimika kuitambua hata kama haijulikani nani anatawala?..ama kuna hatua na utaratibu wa kuunda serikali hiyo kufikia kutambuliwa kwake nje ya uhuru wa nchi husika..maana naona kama mnachanganya sana kutambuliwa kwa nchi na serikali..Kaka Mkandara,
Hata kama Balozi huyo anatetea maslahi yake:
(a) Hajavunja sheria yoyote ya Tanzania
(b) Hajakiuka sharti lolote ya kibalozi.
Kwa hiyo Membe hawezi kumchagulia balozi huyo bendera ya kupeperusha ofisni kwake. Je Membe anajuaje bendera halali ya Libya kama siyo kutoka kwa balozi huyo huyo? Ni jambo la kawaida kwa nchi kubadilisha bendera zao; hata Libya kabla ya Ghadaffi walikuwa na bendera nyingine tuliyokuwa tunatambua kulingana na taarifa tulizoletewa na ubalozi wao, halafu baada ya Ghaddafi kupindua utawala uliokuwepo kwa nguvu akaleta bendera mpya ambayo pia tuliitambua kutokana na taarifa za ubalozi wao, kwa hiyo hata baada ya Ghadaffi kupinduliwa kwa nguvu itabidi tukubali bendera mpya tutakayoletewa na balozi wao.
Kuhusu uhalali wa waasi wa Libya siyo swala la Membe kusema kama ni halali au la, bali inabid yeye asikilize kutoka kwa balozi wa Libya aliyeko hapa nchini kihalali. Inawezekana kabisa kuwa hao waasi ni kikundi kidogo tu, lakini kidiplomasia, mawasiliano kati ya Tanzania na Libya yanapitia kwa mabalozi siyo kwenye vyombo vya habari, kwa yeye afuate taarifa za kutoka kwa balozi tu, si vinginevyo..
Duuh...!! Thread kiboko hii usipime 🙂
Watu wanashuka nondo kana hawana akili nzuri vile.... lol
Madenti wa kozi za uhusiano wa kimataifa bila shaka lazima wai-reference hii sredi!!!
You are very right hiyo bendera nani kaitengeneza? maanake hawa watu hawajawa organised kiasi cha kufanya mabadailiko kama haya.. Ni baraza gani lililoipitisha bedera hiyo? Au kinachowauma sana ni matumizi ya bendera ya Ghadafi ambayo ina symbolizes - Islaam..Why bendera imekuwa issue kubwa sana ili hali imetengenezwa na watu ambao hawan mamkala ya uongozi wa nchi hiyo...
Sikutaka kuingia katika mjadala huu kwa kuwa naona hauna tija sana. Msimamo wa nchi nauunga mkono pamoja na wote waliotoa hoja sawia kuwa tatizo sio uasi au Ghadaffi, tatizo ni taratibu na misingi. Kinachofanyika na waasi wa Libya katika ubadilishaji wa alama hakikuwahi kufanyika na Waliokuwa Waasi wa Rwanda na wengine wowote unaowajua. Huwezi kuteua Balozi kama hujashika mamlaka ya nchi.Balozi wa Libya hakuwa anamwakilisha Gaddafi, alikuwa anaiwakilisha nchi na watu wa Libya na utawala wao. Utawala wa Gaddafi umeporomoka na kuondolewa uhalali wake na kwa maoni ya Walibya ulipoteza uhalali ule pale ulipoamua kuwageuka na kuwashambulia; na japo wengine tunafikiria labda uligeuka baada ya waasi kuanza Benghazi ukweli ni kuwa kwenye mioyo ya baadhi ya wananchi wa Libya ulikuwa umepoteza uhalali wake muda mrefu sana. Sasa watu wa Libya wapo, wananchi wa Libya wapo, na utawala mpya ulioongoza maasi upo na umekubaliwa kuwa ndio unajukumu la kutawala kama serikali ya mpito kuelekea utawala mpya.
Sikutaka kuingia katika mjadala huu kwa kuwa naona hauna tija sana. Msimamo wa nchi nauunga mkono pamoja na wote waliotoa hoja sawia kuwa tatizo sio uasi au Ghadaffi, tatizo ni taratibu na misingi. Kinachofanyika na waasi wa Libya katika ubadilishaji wa alama hakikuwahi kufanyika na Waliokuwa Waasi wa Rwanda na wengine wowote unaowajua. Huwezi kuteua Balozi kama hujashika mamlaka ya nchi.
Lakini kilichoniingiza kwenye mjadala ni sentensi yako kuwa Balozi si mwakilishi wa Rais ni mwakilishi wa wananchi. Ukweli ni kuwa, pamoja na kuwa ukweli huo unakera ni kwamba, Balozi wa Nchi husika kwanza ni mwakilishi wa Rais wa Nchi(Mkuu wa Nchi) na pili ni mwakilishi wa wananchi. Hii ndio desturi ya diplomasia tokea enzi na enzi na desturi hii inajionyesha katika lugha na taratibu za uwasilishaji wa Hati za Utambulisho (Credentials) na Hati za Kumrudisha Balozi ( Letters of Recall).
Katika credentials, Mkuu wa Nchi anayemtuma Balozi analazimika kusaini hati zile yeye mwenyewe kwa mkono wake ili ziwe halali. Hawezi kukasilimisha jukumu hilo kwa mamlaka yoyote nyingine. Lugha yake mule inasema "mimi binafsi kwa kumjua vyema mtu huyu, namleta kwako mtu huyu awe mwakilishi wangu kwako, lolote atakalolifanya au kulisema lichukuliwe kuwa analifanya kwa niaba yangu". Haya ni maneno mazito sana. Aidha, ikatokea Balozi aliyeteuliwa na kupatiwa barua hii akafika katika nchi aliyotumwa, na ikatokea bahati mbaya kuwa Rais aliyemteua akafariki kabla hajawasilisha Credentials zake, uteuzi wake unakufa itabidi ateuliwe upya na Rais atakayechukua madaraka.
Kwa maelezo hayo mafupi,naomba kurekebisha hoja kuwa Balozi si mwakilishi wa Kiongozi wa nchi bali mwananchi. Hayo mengine kuhusu bendera sitachangia maana ni jambo la wazi sana.
Mkuu ktk hili nitahitaji muda zaidi kwa sababu navyotambua mimi bendera ya nchi (sovereign) ina sheria zake lazima ipo sheria ktk uundwaji wake na kutambuliwa na nchi, African Union pamoja na Umoja wa Mataifa, .. Lakini hatuwezi kutumia bendera ilotumika vitani (war flag) kulitambua taifa.Ninachosema ni kuwa sisi hatujui utaratibu unaotumiwa na Libya katika kudesign na kutengeza bendera zao. Tunapewa taarifa hizo na ubalozi wa Libya. Sasa ubalozi huo ukituambia kuwa sasa bendera yao sasa ni mojawapo ya hizi hapa chini tuikatae ilhali hazijavunja sheria zetu? Bendera ya nchi nyinngine inatuhusu nini sisi kama taifa host la ubalozi iwapo balozi wao halalai katuambia kuwa bendera yao imebadilika? Je tunajenga utaratibu wea kuchagua taarifa zipi za kibalozi tutaamini na zipi tutakataa?
![]()
![]()
![]()
![]()
Mkandara:
Ukiangalia kwa Makini sana utagundua kuwa bendera jiuo ya "waasi" ina alama nyingi za uislamu kulingana na rangi zake kuliko ile ya Ghaddafi ambayo ilikuwa na rangi moja tu.
Mkuu ktk hili nitahitaji muda zaidi kwa sababu navyotambua mimi bendera ya nchi (sovereign) ina sheria zake lazima ipo sheria ktk uundwaji wake na kutambuliwa na nchi, African Union pamoja na Umoja wa Mataifa, .. Lakini hatuwezi kutumia bendera ilotumika vitani (war flag) kulitambua taifa.
Libya iliyo huru inajulikana na kama wanataka kubadilisha bendera basi waunde kwanza serikali yao, huyo balozi muulize kiongozi wake nani kama hatakwambia kapewa maagizo na NATO.. sasa tukubali kupeperusha bendera ya Chadema au CCM kwa sababu balozi wa Libya kaambiwa na NATO wapeperushe bendera inayofanana na ya CCM?..then tungekuwa na bendera zinazofanana maanake haiwezekani kila nchi ina bendera tofauti na nyingine..Libya haina kiongozi wala chama kinachoongoza huyu balozi kapata maagizo kutoka wapi?
...halafu rangi za Uislaam ni zipi? mkuu wangu - it's only Green color kama bendera ya CCM haya nimelianzisha zogo!..
Ndugu, taasisi kubwa ya kidiplomasia duniani sio Umoja wa Mataifa bali ni nchi (National State). Umoja wa Mataifa ni Mratibu wa matakwa ya nchi wanachama ambao ni 192, kati yao walioitambua Serikali ya Libya hawajafikia hata theluthi mbili. Hivyo, nchi nyingi zaidi duniani haziitambui inayojiita Mamlaka mpya zinasubiri kujiridhisha kwanza na masuala kadhaa ikiwemo uhalali wa Waasi na ushahidi wa kudhibiti kwao dola.Mkuu, umeona ile bendera ya Libya inayopepea leo pale umoja wa Mataifa? je kuna taasisi kubwa ya kidiplomasia kubwa kuliko umoja wa Mataifa hapa duniani?
Kichuguu mkuu wangu hakuna mamlaka hiyo isipokuwa ni nguvu ya shinikizo kutoka nchi za magharibi. Libya haina serikali na huyo Balozi hapokei maagizo kutoka chombo chochote zaidi ya NATO.. Libya has no leadership at the moment..Ninaelewa kabisa arguments zako kuwa Bendera aliyotumia balozi huenda siyo halali. Ila ninalosema mimi ni kuwa Membe hana mamlaka ya kutambua au kukataa bendera inaltumiwa na balozi wa nchi nyingine. Kama balozi huyo kakiuka sheria za bendera ya nchi yake, basi mamlaka iliyomtuma kuiwakilisja nchi yake itamvua madaraka, siyo Membe.
Rangi ya kijani ndiyondiyo rangi iliyotumiwa na kabila na Mtume Muhammadi kwa hiyo ni ya kiislamu, lakini pia Crescent na rangi neysi zina nafsi yake katika usilamu. Ninalosema ni kuwa kwa vile bendera mpya inayo Crescent, nyeusi na kijani, then ina alama nyingi za usiliamu kuliko rangi moja tu ya kijani ilyokuwa inatumiwa na Ghaddafi.
Balozi wa Libya ana haki ya kubadilisha bendera na Tanzania hain haki hata kidogo kuingilia. Sana sana wanatakiwa kutoa taarifa kwa Tanzania kuwa kwa sasa bendera ni tofauti. Hii bendera wanayotumia Libya kwa sasa ndiyo ilikuwepo kabla huyu Gadaffi hajapindua na kuleta bendera yake ya kijani. Sasa, the people of Libya are reclaiming what they belive is theirs. Hivi Membe anataka kusema kuwa Libya inapata order toka Tanzania? Huu ujasiri wa kumuita Balozi wa Libya ulikuwa wapi wakati wa mgomo wa mafuta? Priority ya viongozi wetu ni ipi?
Hapo umechanganya chumvi na sukari. Ulitaka aingilie suala la mafuta wakati hiyo siyo docket yake? Narudia tena, issue hapa ni kufuata taratibu za kidiplomasia kama Vienna Convention inavyotaka. Wanayo haki ya kubadilisha lakini wana wajibu wa kuarifu uamuzi wao kabla hawajatundika bendera hiyo au ku-display alama zingine walizozibadilisha.
Ndugu,Ninaelewa kabisa arguments zako kuwa Bendera aliyotumia balozi huenda siyo halali. Ila ninalosema mimi ni kuwa Membe hana mamlaka ya kutambua au kukataa bendera inaltumiwa na balozi wa nchi nyingine. Kama balozi huyo kakiuka sheria za bendera ya nchi yake, basi mamlaka iliyomtuma kuiwakilisja nchi yake itamvua madaraka, siyo Membe.
Rangi ya kijani ndiyondiyo rangi iliyotumiwa na kabila na Mtume Muhammadi kwa hiyo ni ya kiislamu, lakini pia Crescent na rangi neysi zina nafsi yake katika usilamu. Ninalosema ni kuwa kwa vile bendera mpya inayo Crescent, nyeusi na kijani, then ina alama nyingi za usiliamu kuliko rangi moja tu ya kijani ilyokuwa inatumiwa na Ghaddafi.
Hata hivyo, Balozi wa Libya nchini Zimbabwe, Taher El Magrahi tayari amekumbana na vipingamizi kutoka kwa Serikali ya Rais Robert Mugabe.
Kwa mujibu wa gazeti la The Standard la Zimbabwe, toleo la Jumapili iliyopita, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi hiyo ilimwamuru El Magrahi kushusha bendera hiyo haraka na kupandisha iliyokuwa ya Serikali ya Gaddafi.
Ubalozi huo wa Libya nchini Zimbabwe ulipandisha bendera hiyo ya NTC baada ya waasi kufanikiwa kuuteka Mji Mkuu wa Tripol, yakiwapo makazi ya Gaddafi.
Amri ya Serikali ya Zimbabwe ya kutaka ubalozi huo kushusha bendera ya waasi wa Libya ulipingwa vikali na El Magrahi.Yeye alijitetea kuwa bendera hiyo siyo mpya bali ni ya taifa hilo la Libya ambayo ilikuwa inatumiwa tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1951.
Msimamo wa El Magrahi ulisababisha Serikali ya Zimbabwe kutoa amri ya balozi huyo kufunga virago vyake na kurejea nchini mwao.Hadi jana, hakukuwepo na taarifa iwapo balozi huyo ametii amri hiyo.
Sina hakika kama huyu balozi kweli ni mwakilishi wa kidiplomasia wa wale anaowawakilisha maana alipaswa kujua kwamba bendera si kipande tu cha nguo ambacho unaweza kukibadilisha kama leso. Hata hivyo uamuzi wa kumtimua hautakiwi kuzingatia kilichofanyika Zimbabwe na wala isionekane kutochukua uamuzi huo wa Mugabe ni kukosa kujiamini au kushindwa katika majukumu ya Serikali.