Balozi wa Libya Tanzania akaidi kushusha bendera ya NTC!

Balozi wa Libya Tanzania akaidi kushusha bendera ya NTC!

Nadhani huyu Balozi asiejua Taratibu atimuliwe aende akapigane na hao wenzake wanaowekwa madarakani na NATO

Hicho ndicho ninachosubiri. Si amekaidi amri yetu ya kumtaka ashushe bendera ya NTC amabayo hatuitambui? What next? Tumtimue basi. Halafu hivi tutakuwa tuna monitor mpaka kwenye residence yake kuhakikisha kuwa haweki bendera ya NTC? Na gari yake tutai-monitor muda wote kuhakikisha kuwa hatundiki bendera ya NTC? Na suti zake tutahakikisha hazina bendera ya NTC? Kwa nini tuu tusimfukuze halafu tumwambie Gaddafi atuletee balozi ambaye hatakaidi amri?
 
If any of the following is incorrect, please post a correction.

In 1951 Libya was amongst the poorest nations in the world.

Before N.A.T.O invasion Libya enjoyed the highest standard of living in Africa, And ahead Of Russia Brazil Saudi Arabia.

In Libya homes are considered a human right, newly married couples receive 50.000 dollars to buy their new home.

Electricity is free.

Before Qaddafi less then 1/5 of the Libyans were illiterate, Now education is free and the literacy rate is 83%

Healthcare is also free and high-quality, and if Libyans cannot find education or health care they need in Libya the Libyan government will fund them to Other Countries.

All loans are interest free 0% By law. (This is about to change)

If a Libyan buys a car the government pays 50% of the price.

The price of gasoline is $0.14

Any Libyan wishing to become a farmer is given Free use of land A home and farm equipment livestock and seeds.

On 1 July 1.7 Libyans assembled in green square protest at the n.a.t.o bombings thats 95% of the population of Tripoli, And about one third of the entire Libyan population.

The Libyan bank is state owned And issues debt free Money, (This is also about to change)

In 1990 Libya was accused of the Lockerbie bombing, it has transpired that the US paid witnesses at the trial 4 million each to testify against the accused Libyans,And have since rescinded their evidence.!

Qaddafi was working to change payment for Libyans oil away from the US dollar To the gold dinar,
This move prompted Sarkozy to call Libya ' a threat to the financial security of mankind.

One of the first acts of the Libyan 'rebels' Was to create a new central bank, to create money And sell to the people at interest. (Just read our bankers And our debt.) Libya used to be debt free, not any more.

At least 30,000 Libyans have been killed by N.A.T.O air strikes and rebels


Thats why our GOD is punishing these killers in kind..i.e Kimbunga Irene
 
Mkuu, nimejiridhisha na maoni niliyoyatoa. Yanajitosheleza. Yametokana na kusoma desturi na tamaduni za kidiplomasia zilizohifadhiwa miaka na miaka, vizazi na vizazi.

Leo hii, huwezi kuibuka na bendera ya tanganyika ukayaambia mataifa yakubali bila kufuata utaratibu. Kisheria, bendera ya tanganyika ilishakufa. Inauma lakini ndio ukweli. Ikitokea watanganyika tukavunja muungano na kutaka kuweka bendera hiyo, wataichukulia kama bendera mpya na kuikubali ikiwa tutafuata taratibu za ku'replace' bendera ya jamhuri ya muungano ambayo wanaitambua rasmi kwa sasa.

Sawa assume kisheria bendera ya Tanganyika imeshakufa. Vipi sasa Watanzania tukiamua kuifufua na kuitumia ile bendera, Kenya watatukatalia kuipandisha kwenye ubalozi wetu Nairobi kwa sababu muungano bado haujavunjwa? Nani huwa anaamua bendera ipi itumike na ipi isitumike. Is it the sending or the receiving State?
 
halafu kinachoniudhi mimi they wiill never concede kwamba wamekosea msingi wa hoja yao. Mwingine hapo anafikiria watu wa Libya wanagombea mkate na maisha ya juu zaidi.. well.. kama hiyo ingekuwa issue.. mbona Afrika ya Kusini ilikuwa na maisha mazuri tu kabla ya kuingia kwa ANC in 1994 na wapo wanaotuambia kuwa maisha wakati wa Mwingereza yalikuwa bora kuliko wakati alipoingia Nyerere! Hili somo sijui ni gumu kiasi gani. Ndio maana watu wengine wakiambiwa "uwanja wa mpira wa kisasa, daraja la Mkapa, barabara, shule za kata, UDOM" wanafikiri thats what is all about. Ingekuwa hivyo maandamano ya Chadema au siasa za upinzani Tanzania zingekufa!

Nyerere aliwaambia lengo na kusudi la maendeleo ni watu siyo vitu.. still people don't get this philosophical maxim.
Mheshimiwa sana Mwanakijiji, naungana na wewe juu ya falsafa ya Mwalimu kuwa msingi wa maendeleo ni watu. Naomba pia ukubaliane nami kuwa Mwalimu Nyerere ni mtu ambaye alipenda sana na kuheshimu principles. Aliwahi kunukuliwa akisema " Principle is principle, if you break the principle, the principle will break you".

Tunapishana mahali. Tatizo sio Ghadaffi kupinduliwa. Ghadaffi naye alipindua na kupinduliwa kwake ndio njia pekee ya wananchi wa Libya kumuondoa madarakani. Sina tatizo na hilo.

Tatizo langu liko katika principle kuwa kutambua bendera ya waasi, Serikali yao na jina jipya wanalotaka kulipa taifa lao kabla hawajamaliza kazi ya mapinduzi.

Ghaddafi alipindua na kukamata mamlaka ya dola mikononi mwake,nchi zikajiridhisha kuwa amekamilisha mapinduzi, akajulisha nchi kuwa anabadili bendera na jina la nchi yake, nchi zikatambua. Tofauti na Ghadaffi, hawa hajafanya hayo. Hawajafanikiwa kuridhisha nchi nyingi duniani kuwa wamekamata na kuhodhi dola. Kabla hawajakamilisha hilo wanatutangazia mabadiliko ya bendera na jina la nchi. Hii si sahihi sasa, jana na hata kesho.

Kuingia mji mkuu si kudhibiti nchi na dola. Kukamata mji mkuu na dola ndio kushika nchi. Mji Mkuu ndio hutekwa mwisho na ndio kazi ngumu zaidi katika mapinduzi. Unaweza kuingia mji mkuu na ukatolewa baada ya muda mfupi. Serikali yoyote, itahifadhi na kutumia nguvu yake ya mwisho kudhubiri mji mkuu maana ndio ashirio la kukamata dola na mamlaka ya nchi. Waasi kwa bahati mbaya hawajakamilisha kazi hiyo na ndio sababu ya kuwia ugumu kwa nchi ambazo hazina maslahi ya moja kwa moja na vita hiyo kutambua mamlaka ya waasi.

Rejea Kigali na Kinshasa kama mifano ya karibu ya namna ambavyo dola ilikamatwa baada ya mapigano. Aidha, Tunisia na Egypt tumeona wazi ambavyo waliokuwa wakikamata dola walipotangaza kuachia dola aidha kwa kukimbia kama alivyofanya Rais wa Tunisia au kukabidhi madaraka kwa jeshi kama alivyofanya Rais Mbarak.

Sasa tunatumia principle gani kutambua bendera na mamlaka ya waasi wa Libya?

Nisaidie Mwanakijiji. Mimi ni muumini sana wa busara zako.
 
Serikali yetu eti imekomaa na Gaddaf wakati dunia yote inaona mzee huyu ameshindwa, tuwaacheni Libya waamue. Kama walisema hawamtaki Gaddaf si tuwapigie makofi wampe wanayemtaka?
 
What kind of legal evidence do you want? i am not here for political purpose like you!

Je unaelewa maana ya mahusiano ya kidiplomasia?...Suppose membe angemuuliza balozi hii bendera ya utawala wa ghadafi si bendera ya libyani people kwa sasa je balozi angejibu nini??

Balozi wa nchi haletwi kumwakilisha Rais kwa sababu amemteua yeye kwa ajili ya ujomba wala ushemeji!!!....ila huletwa kuwawakilisha wananchi wa nchi husika....so whatch-out!!

Mkuu pamoja na mambo mambo ya kidplomasia lakini ujue Balozi huwakilisha serikali halali iliyopo Madarakani!! sasa Libya wana serikali ipi unayoijua ama wale wauaji wanaobebwa na mabeberu kwa nia ya kupora mafuta!!! hivi sisi Waafrika tuna nini?!! yani kabisa unaunga mkono mambo ya ajabu ajabu tu..
 
<br />
<br />

Tatizo langu liko katika principle kuwa kutambua bendera ya waasi, Serikali yao na jina jipya wanalotaka kulipa taifa lao kabla hawajamaliza kazi ya mapinduzi.

Ghaddafi alipindua na kukamata mamlaka ya dola mikononi mwake,nchi zikajiridhisha kuwa amekamilisha mapinduzi, akajulisha nchi kuwa anabadili bendera na jina la nchi yake, nchi zikatambua. Tofauti na Ghadaffi, hawa hajafanya hayo. Hawajafanikiwa kuridhisha nchi nyingi duniani kuwa wamekamata na kuhodhi dola. Kabla hawajakamilisha hilo wanatutangazia mabadiliko ya bendera na jina la nchi. Hii si sahihi sasa, jana na hata kesho.

Kuingia mji mkuu si kudhibiti nchi na dola. Kukamata mji mkuu na dola ndio kushika nchi. Mji Mkuu ndio hutekwa mwisho na ndio kazi ngumu zaidi katika mapinduzi. Unaweza kuingia mji mkuu na ukatolewa baada ya muda mfupi. Serikali yoyote, itahifadhi na kutumia nguvu yake ya mwisho kudhubiri mji mkuu maana ndio ashirio la kukamata dola na mamlaka ya nchi. Waasi kwa bahati mbaya hawajakamilisha kazi hiyo na ndio sababu ya kuwia ugumu kwa nchi ambazo hazina maslahi ya moja kwa moja na vita hiyo kutambua mamlaka ya waasi.

Mkuu samahani najua hii post umeilengesha kwa Mwanakijiji lakini kuna post ya Nguruvi3 kwenye thread nyingine. Unaweza uka reconcile post yako na hii ya Nguruvi3?

Tunakumbuka kuwa Tanzania iliitambua FRELIMO kabla ya kuingia Maputo. Ilitambua MPLA kabla ya kuingia Luanda. Vyama hivyo vya kisiasa havikuwa na serikali wakati wa mapambano. Imekuwaje leo kuwe na masharti ya kuitambua NTC kama kuwa na baraza la mawaziri na kufanya uchaguzi hata pale palipo wazi kuwa Gaddafi hayupo na hatarudi!!
 
Sawa assume kisheria bendera ya Tanganyika imeshakufa. Vipi sasa Watanzania tukiamua kuifufua na kuitumia ile bendera, Kenya watatukatalia kuipandisha kwenye ubalozi wetu Nairobi kwa sababu muungano bado haujavunjwa? Nani huwa anaamua bendera ipi itumike na ipi isitumike. Is it the sending or the receiving State?
Kwa bahati mbaya Tanzania sio Kenya hivyo napata tabu kuisemea. Misingi yake ya kidiplomasia ni tofauti sana na misingi ya Tanzania.

Nachoweza kusema ni kuwa, nchi yoyote yenye kufuata misingi itachukua hatua kadhaa. Itamuita Balozi wetu huko na kumkanya kuwa kitendo chake cha kupandisha bendera inayoitwa ya Tanganyika wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika ipo ni kitendo kisichovumilika na cha kuvunja mahusiano kati ya nchi hiyo na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana kinaweza kutafsiriwa kama kitendo cha Serikali hiyo kukaa kimya ni kuunga mkono uasi dhidi ya Muungano wa Serikali ya Tanzania.

Lakini, nikirudi kwenye swali lako kuhusu nani ana haki ya kuamua bendera ipi ipandishwe kwenye ardhi ya Ubalozi ikizingatiwa kuwa eneo la ardhi ya kibalozi ina kinga ya kidiplomasia, naomba nikujibu kuwa kwanza kinsingi "hakuna haki isiyoambatana na wajibu". Ingekuwa hivyo, mabalozi wangeamua hata kuuza madawa ya kulevya ndani ya ardhi ya ubalozi na wasikamatwe.lengo la kinga yao chini ya Mkataba wa Vienna ni ku 'facilitate' kazi ya kujenga mahusiano kati ya nchi mbili na si uvunjivu wa sheria na mahusiano. Ndio maana Vienna Convention inatambua local laws na inatamka katika maeneo mengine kutambua mamlaka ya sheria za ndani.

Hivyo, kwa taarifa yako, Balozi zote na Mashirika yote yaliyoko nchini, mbali na Vienna Convention, yanatawaliwa na Sheri ya Nchi Na. 5 ya Mwaka 1986 inayoitwa Diplomatic Immunity and Priviledge Act No. 5. Humo kuna wajibu umeainishwa. Si kwamba ukishakuwa na Vienna Convention basi una mamlaka ya kimungu.

Naomba kuwasilisha.
 
Mkuu samahani najua hii post umeilengesha kwa Mwanakijiji lakini kuna post ya Nguruvi3 kwenye thread nyingine. Unaweza uka reconcile post yako na hii ya Nguruvi3?
Asante sana EMT, nachoweza kujibu kuhusu post ya Nguruvi ni kuwa,FRELIMO kilikuwa ni chama cha ukombozi, Tanzania iliunga mkono ukombozi na ilikuwa katika nchi ya mstari wa mbele. Tanzania ilikuwa ikitekeleza maazimio ya OAU na Kamati ya Ukombozi iliyoko Dar es Salaa.

Kwa kifupi, nyakati zilikuwa ni tofauti, mazingira tofauti na players tofauti. Leo hii waasi hawa hawatambuliwi na AU, jitihada za AU kuingilia kati zimezimwa na NATO na washirika wake.

Hivyo, wanaowajua waasi vizuri kwa maana ya NATO wameshawatambua na Tanzania haijalalamika. Hata sisi tulipokuwa tukitambua FRELIMO ambayo iliungwa mkono na OAU ziko nchi hazikuitambua na wala hatukuwa na tatizo. Tuliendelea na kazi hadi FRELIMO ilipokamata mamlaka ya dola, nchi zote zikajiridhisha kisha wakaitambua Serikali ya FRELIMO.

Waasi wa Libya hata kufika kwenye capitals za Afrika kujitambulisha hawajafanya, kwa nini kuwe na shinikizo la kuwatambua? Yaani wakitambuliwa na NATO sie ndio tutambue tu? NATO wanajua kwa nini wanawatambua. Sababu zao sio zetu. Tukiwatambua kwa sababu tu NATO wamewatambua na si kwa sababu zetu, tutakuwa WATUMWA.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
i like it when you say nonsense, halafu unaishia hapo.

Kwanini unataka kuhamisha mjadala kwenye legal bases na kukataa opinion za watu kwenye jambo hili?
Hajui kama vitu vingine ni common sense na reality tu, anaomba legal evidence, kwani waasi walitumia legal procedure gani kumtimua huyo nduli, na mbona wamefanikiwa. Mwache aendelee kusubiri hizo legal zake. Analeta theory za vitabuni hapa.
 
Waasi wa Libya kumbe na wenyewe ni hatari tena zaidi ya Gaddafi,
tayari wameunda kampuni ya mafuta iitwayo ACOCO. Msemaji wake Abdeljalil Mayouf, ametanganza kuwa watapewa visima vya mafuta
 
Balozi wa Libya hakuwa anamwakilisha Gaddafi, alikuwa anaiwakilisha nchi na watu wa Libya na utawala wao. Utawala wa Gaddafi umeporomoka na kuondolewa uhalali wake na kwa maoni ya Walibya ulipoteza uhalali ule pale ulipoamua kuwageuka na kuwashambulia; na japo wengine tunafikiria labda uligeuka baada ya waasi kuanza Benghazi ukweli ni kuwa kwenye mioyo ya baadhi ya wananchi wa Libya ulikuwa umepoteza uhalali wake muda mrefu sana.

Sasa watu wa Libya wapo, wananchi wa Libya wapo, na utawala mpya ulioongoza maasi upo na umekubaliwa kuwa ndio unajukumu la kutawala kama serikali ya mpito kuelekea utawala mpya.

Mwanakijiji,
Sio kwamba Membe haujui ukweli ulioueleza kwenye post #26 na maelezo haya mengine. Shida ni kuwa kuna hofu kubwa kwa watawala wetu kuwa: "People's Power" itawaengua. Hivyo alichokifanya Membe kwa tafsiri yangu ni kujaribu kuwaonyesha watanzania kuwa huwa kuna 'process' na hivyo siyo rahisi. Ukweli ni kuwa lwa vyovyote vile, Gaddafi ameanguka. Tulichelewa kuitambua Tunisia mpya, lakini tuliishia kuitambua na hicho ndo kitakachotukia hapa. Hoja sio lini tutaitambua. ... Hoja ni kuwa hatimaye tutaitambua!!!
 
Kwa bahati mbaya Tanzania sio Kenya hivyo napata tabu kuisemea. Misingi yake ya kidiplomasia ni tofauti sana na misingi ya Tanzania.

Mkuu pitia sheria ya Tanzania na ile ya Kenya then list misingi ya Kenya ya kidiplomasia ambayo ni tofauti sana na misingi ya Tanzania.
Sheria ya Kenya: http://www.law.co.ke/klr/fileadmin/pdfdownloads/Acts/PriviligesandImmunitiesCap179.pdf
Sheria ya Tanzanua: http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/5-1986.pdf

Nachoweza kusema ni kuwa, nchi yoyote yenye kufuata misingi itachukua hatua kadhaa. Itamuita Balozi wetu huko na kumkanya kuwa kitendo chake cha kupandisha bendera inayoitwa ya Tanganyika wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika ipo ni kitendo kisichovumilika na cha kuvunja mahusiano kati ya nchi hiyo na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana kinaweza kutafsiriwa kama kitendo cha Serikali hiyo kukaa kimya ni kuunga mkono uasi dhidi ya Muungano wa Serikali ya Tanzania.

Right. Sasa vipi ukimkanya na akaendelea kukaidi amri utafanyaje?

Lakini, nikirudi kwenye swali lako kuhusu nani ana haki ya kuamua bendera ipi ipandishwe kwenye ardhi ya Ubalozi ikizingatiwa kuwa eneo la ardhi ya kibalozi ina kinga ya kidiplomasia, naomba nikujibu kuwa kwanza kinsingi "hakuna haki isiyoambatana na wajibu". Ingekuwa hivyo, mabalozi wangeamua hata kuuza madawa ya kulevya ndani ya ardhi ya ubalozi na wasikamatwe.lengo la kinga yao chini ya Mkataba wa Vienna ni ku 'facilitate' kazi ya kujenga mahusiano kati ya nchi mbili na si uvunjivu wa sheria na mahusiano. Ndio maana Vienna Convention inatambua local laws na inatamka katika maeneo mengine kutambua mamlaka ya sheria za ndani.

Naomba basi unijibu swali. Nakubali kimsingi "hakuna haki isiyoambatana na wajibu" lakini swali lilikuwa ni nani huwa ana maamuzi ya bendera ipi itumike na ipi isitumike. Ni sending State or the receiving State?

Hivyo, kwa taarifa yako, Balozi zote na Mashirika yote yaliyoko nchini, mbali na Vienna Convention, yanatawaliwa na Sheri ya Nchi Na. 5 ya Mwaka 1986 inayoitwa Diplomatic Immunity and Priviledge Act No. 5. Humo kuna wajibu umeainishwa. Si kwamba ukishakuwa na Vienna Convention basi una mamlaka ya kimungu. Naomba kuwasilisha.

Mkuu the Diplomatic Immunity and Priviledge Act simply incorporates into the laws of Tanzania the Vienna Conventions on Diplomatic and Consular Relations. Hii sheria haitoi wajibu wala haki zaidi ya zile zilizomo kwenye Conventions. Kwa meneno mengine the Act simply gives affect to the Conventions in our national legal system. I am sure you know monist and dualist systems. Hii hapa sheria soma then niambie kama kuna haki na wajibu gani tofauti na zilizopo kwenye hizo conventions mbili: http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/5-1986.pdf
 
Nadhani tanzania tuna mahusiano ya kidiplomasia na libya ambapo libya inaundwa na wananchi wake kama vile tanzania ilivyo.. na Si mahusiano binafsi na mohamad Ghadafi!!

So the Libyani Ambassador he is very right and he have right to do it.

Wana libya wamemkataa ghadafi nyie mnamtaka wa nini?? Subirini akianzisha nchi yake inayoitwa ghadafi country mtapandisha bendera yake.
Viva libyan people mmedhubutu na mmeweza...si watanzania wanajivunia amani huku wakihujumiwa na kulala gizani ....50 years of independence!!! what is independence if there is no dignity!!!

Kwa nini usiandike kwa kiswahili tu kuliko kuharibu lugha za watu wengine!!!!? HE HAVE!!!!!!!!!?????
 
Mkuu pamoja na mambo mambo ya kidplomasia lakini ujue Balozi huwakilisha serikali halali iliyopo Madarakani!! sasa Libya wana serikali ipi unayoijua ama wale wauaji wanaobebwa na mabeberu kwa nia ya kupora mafuta!!! hivi sisi Waafrika tuna nini?!! yani kabisa unaunga mkono mambo ya ajabu ajabu tu..

Taratibu mkuu. Mbona mnarudia makosa yale yale? Balozi hawakilishi serikali bali anawakilisha nchi. Article 3(1) ya Viena Convention inasema the functions of a diplomatic mission consist of representing the sending State in the receiving State. Haisemi representing the sending goverment in the receiving government. Yaani vichwa vyetu basi tuu.
 
Watu mnachekesha. tehe...tehe....eeeeee

Hivi democrasia inasemaje? watu(wengi) si ndo wanaamua? si ndo kila siku tunasema majority rule? sasa walibya wamemuondoa Gadaff kilingeni, tena hajatoka kwa kupenda kalazimishwa, katukana waasi, kawaita mende. Kwa hivyo ni sahihi kwa wao kubadilisha kila kilichokuwa kinamtangaza gadaff. Wengi Libya wameamchoka Tanzania tunamtaka wa nini?

Nyie wanasheria uchwara, siku zote ukiziangalia sheria huwa hazitendi haki, zinatengenezwa na watawala kwa lengo la kulindana. Mifano ipo mingi hapa nchini. Wanacnhi tukiwachoka, hata sheria zao tunazichoka.

Tanzania tunaibiwa rasilimali zetu ni kwa sababu watawala wametengeneza sheria za kufanikisha wizi huo. sasa je siku tukiwatimua, tukataka madiliko, tuuendelea na sheria zao mbovu zinazotunyonya au tutawaondosha na sheria zao za kifisadi?

Kama kina MEMBE wanaipenda bendera ya Gaddafi, wangemshauri kuachia ngazi na kuitisha uchaguzi huru ambao ungezuia waasi kuwa na bendera yao, na kama ni kuwa na bendera, ingekuwa ya chama cha siasa, na Gaddaff angekuwa na bendera ya chama chake halafu hiyo ya nchi ingebaki kama ilivyo.
 


Mkuu pitia sheria ya Tanzania na ile ya Kenya then list misingi ya Kenya ya kidiplomasia ambayo ni tofauti sana na misingi ya Tanzania.
Sheria ya Kenya: http://www.law.co.ke/klr/fileadmin/pdfdownloads/Acts/PriviligesandImmunitiesCap179.pdf
Sheria ya Tanzanua: http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/5-1986.pdf



Right. Sasa vipi ukimkanya na akaendelea kukaidi amri utafanyaje?



Naomba basi unijibu swali. Nakubali kimsingi "hakuna haki isiyoambatana na wajibu" lakini swali lilikuwa ni nani huwa ana maamuzi ya bendera ipi itumike na ipi isitumike. Ni sending State or the receiving State?



Mkuu the Diplomatic Immunity and Priviledge Act simply incorporates into the laws of Tanzania the Vienna Conventions on Diplomatic and Consular Relations. Hii sheria haitoi wajibu wala haki zaidi ya zile zilizomo kwenye Conventions. Kwa meneno mengine the Act simply gives affect to the Conventions in our national legal system. I am sure you know monist and dualist systems. Hii hapa sheria soma then niambie kama kuna haki na wajibu gani tofauti na zilizopo kwenye hizo conventions mbili: http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/5-1986.pdf

Majibu yako wazi. Akiendelea kukaidi anafukuzwa nchini. Sina shaka kuwa akiendelea kufanya hivyo atachukuliwa hatua. Ni suala la muda.

Kuhusu misingi ya Kenya na Tanzania naomba nikusahihishe kuwa misingi haipatikani kwenye sheria tajwa. Misingi inatokana na Sera ya Mambo ya Nje, misimamo ya nyuma (precedences) na maslahi mapana ya taifa. Ukiangalia hivyo vitu vitatu, kuna tofauti kubwa sana kati ya kenya na tanzania. Ukubwa wa tofauti hiyo ni sawa na tofauti kati ya jua na mwezi.

Nakushauri soma posts zangu za nyuma katika thread hii utakuta nimesema kuwa tatizo sio bendera, tatizo ni taratibu za kufikia kupandisha bendera hiyo iwe kwenye ardhi ya ubalozi, kwenye gari au ubalozini, kwa maana hayo maeneo matatu yanatawaliwa na sheria.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Taratibu mkuu. Mbona mnarudia makosa yale yale? Balozi hawakilishi serikali bali anawakilisha nchi. Article 3(1) ya Viena Convention inasema the functions of a diplomatic mission consist of representing the sending State in the receiving State. Haisemi representing the sending goverment in the receiving government. Yaani vichwa vyetu basi tuu.
<br />
<br />

Naomba usome vizuri kipengele cha sheria ulichonukuu. Kisha zingatia tofauti ya neno Ubalozi na Balozi.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
[TABLE="class: infobox, width: 22"]

Flag of the Libyan Republic[TR]
[TD="colspan: 2"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"][/TD]
[/TR]
[TR]
Adopted[TD]February 27, 2011[/TD]
[/TR]
[TR]
Design[TD]Horizontal tricolor of red, black and green with white crescent and star in the center[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
The National Transitional Council, formed on 27 February 2011, adopted the flag previously used in Kingdom of Libya between 1951 and 1969[SUP][1][/SUP] as the "emblem of the Libyan Republic".[SUP][2][/SUP] The flag was officially defined in article 3 of the Libyan interim Constitutional Declaration.
The flag was initially used by protestors during the Libyan Civil War and is being flown at Libyan diplomatic missions supporting the National Transitional Council. On 10 March 2011, France was the first country to recognize the council as the official government of Libya.[SUP][3][/SUP] On 21 March 2011, the flag was flown by the Permanent Mission of Libya to the United Nations and appeared on their official website,[SUP][4][/SUP][SUP][5][/SUP] and thereafter in late August by the Arab League[SUP][6][/SUP] and by Libya's own telecommunications authority,[SUP][7][/SUP] namely the Libya Telecom & Technology, on its own website. Green in the flag chosen by founding fathers of the Kingdom of Libya represents Tripolitanian Republic from 1918 to 1923 or Islam, red represents Ottoman Caliphate rule and the prominent color on the flagships of Tripoli in the nineteenth century, and the black part is identical to the flag of the emirate of Cyrenaica. [SUP][8][/SUP]
[h=2][edit] Flag used by Gaddafi loyalists[/h][TABLE="class: infobox, width: 22"]

Flag of the Great Socialist People's Libyan Arab Jamahiriya[TR]
[TD="colspan: 2"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"][/TD]
[/TR]
[TR]
Use[TD]National flag and civil ensign [SUP][9][/SUP][/TD]
[/TR]
[TR]
Proportion[TD]usually 1:2[/TD]
[/TR]
[TR]
Adopted[TD]November 11, 1977[/TD]
[/TR]
[TR]
Design[TD]A Green Field[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2"]Variant flag of the Great Socialist People's Libyan Arab Jamahiriya[/TD]
[/TR]
[TR]
Use[TD]Naval ensign [/TD]
[/TR]
[TR]
Design[TD]A field of Light blue, with the National Flag of Libya in the canton and a white anchor with rope in the fly[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
The flag of the Gaddafi-led Great Socialist People's Libyan Arab Jamahiriya was adopted on November 11, 1977 and consists of a green field. It is the only national flag in the world with just one color and no design, insignia, or other details.[SUP][10][/SUP] It was chosen by Libyan leader Muammar al-Gaddafi[SUP][11][/SUP] and reflects the historical green banners of the Fatimid Caliphate, a state that included Libya. Green, the national color of Libya, symbolizes the predominant religion of Islam as well as Gaddafi's "Third Universal Theory".

kwa taarifa tafadhali
 
Back
Top Bottom