Balozi Kairuki asema biashara ya China na Tanzania imepanda thamani kutoka Dola za Kimarekani Milioni 200 hadi 600

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Balozi anayemaliza muda wake Nchini China, Mbelwa Kairuki ambaye kwa sasa amepangiwa Kituo kipya cha kazi Nchini Uingereza, amefanya Mahojiano Maalum na Kituo cha TV Mjini Beijing yenye lengo la kupata ufafanuzi wa yale aliyofanya ndani ya miaka sita ya Ubalozi Nchini humo.

Balozi Kairuki amesema, ndani ya Miaka sita Tanzania na China zimeendeleza na kuimarisha ushirikiano wa Kidiplomasia, Uchumi, Afya, Elimu na masuala mbalimbali ya Kiuchumi na kubadilishana Teknolojia.

Ameeleza kuwa kwa sasa biashara ya China na Tanzania imepanda thamani kutoka Dola za Kimarekani milioni 200 mwaka 2017 mpaka Dola za Kimarekani milioni 600 huku ikitarajiwa kupanda zaidi mwaka ujao.
243b0f0d-cae9-48c9-8e7e-62fd27ea46b5.jpg

Kairuki ameongeza kuwa, wakati wa Uviko19 Mataifa mengi yalipitia hali ngumu Kiuchumi lakini bado China iliendeleza ushirikiano wa Kiuchumi na Tanzania kwa njia zilizozingatia masharti ya Uviko19 huku akiipongeza Kampuni ya Silent Ocean ambayo ilikuwa kipaumbele katika kutafuta njia mbadala wa kusafirisha mizigo ya Wafanyabiashara wa Kitanzania.

Amefafanua kuwa hata sasa baada ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kuongeza ratiba zake za safari na usafirishaji mizigo, imefungua milango zaidi ya kibiashara na Mahusiano na China jambo ambalo litawarahisishia Watanzania kuwa na uhakika wa kufika China moja kwa moja bila kuwa na ulazima wa kuunganisha Ndege maeneo mengine.
8e07d9cc-de50-4a63-a723-1f1735d65e08.jpg

Wakati huohuo ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais kwa kuendelea kumuamini, Mawaziri waliopita na wa sasa, Stregomena Tax kwa ushirikiano waliompa huku akimtakia kheri Balozi mpya wa China, Khamis Mussa Omar ambaye ameeleza kuwa ni Kiongozi mwenye weledi na uwezo mkubwa ambaye anaamini ataendeleza na kufanya mengi makubwa katika wakati wake wa uongozi Nchini humo kwa sababu anaijua China na ana weledi wa masuala ya Mahusiano na Biashara.
 
Back
Top Bottom