Balozi Juma Mwapachu atangaza kurejea CCM...

Balozi Juma Mwapachu atangaza kurejea CCM...

Amesema, Nanukuu " Narudi ili shughuli zangu na za washirika wenzangu zisikwamishwe na Serikali, Kwa sababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu" mwisho wa kunukuu.....
 
kama alimua kuiacha ccm kwenda ukawa kwaajili ya uwaziri wa mambo ya nje swali ni je! ameirudia ccm kwa lengo gani!,?

Kwenye hilo tamko amedai hataki mambo yake na bishara za rafiki zake ziletewe zengwe , in short alihama ukawa kwa ajili ya maslahi binafsi karudi kwa maslahi binafsi , bahati mbaya ndio kachelewa ...

Alafu ukawa inamaana wangeshinda huyu jamaa angekuwa waZiri .. Hahaha
 
'bumpkin au burlesk bully'

Ogopa a 'social climber'!
At this rate sioni tofauti ya the gentry and the social climber Tanzania.

Kina Mwapachu wamemkaribisha na kumtambulisha Nyerere Uingereza alivyoenda kusoma.

Wao ndio walikuwa matawi ya juu tangu enzi za ukoloni.

Sio watu waliokuja mjini juzi.

Wakitoa habari kama hizi wanaaibisha wasomi, wanaojiita wajanja mjini, vipanga wa foreign etc.

I would expect this from the Johnny come lately kina Sumaye, but I guess politics never ceases to surprise.
 
Kwa wenzetu, unaweza kumpa mbunge matatizo ukimnunulia lunch tu kwa kutegemea kitu kutoka kwake.

Tanzania balozi mashuhuri anasema alimuunga mkono Lowassa kwa sababu aliahidiwa uwaziri wa mambo ya nje, bila aibu wala woga!

Eti kiranga! Nimeogopa sana sana sana! Bado naendelea kusema hayo siyo maneno ya balozi Mwapachu
 
Kwa wenzetu, unaweza kumpa mbunge matatizo ukimnunulia lunch tu kwa kutegemea kitu kutoka kwake.

Tanzania balozi mashuhuri anasema alimuunga mkono Lowassa kwa sababu aliahidiwa uwaziri wa mambo ya nje, bila aibu wala woga!

Kwani alijiunga chama gani?


Na bado, kuna watu huwa hawaelewi tunaposema Chama Dola tunamaanisha nini!
 
Nina mashaka makubwa kama huyu mzee ndiye kaandika hii lisala. Kama hajaandikiwa basi hana marafiki wazuri wa kumshauri. Ni aibu Kabisa.

Check hizi sentensi:

"Nililewa mahaba ya Lowasa, nililewa ahadi ya Lowasa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowasa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo."

"Niliamua kulifanya jambo kubwa ili kumsaidia Lowassa. Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu."

Dah nimesikitaka sana na haya maneno. Sana tu, Sana tu, Sana tu, Sana tu, sana tu. Hawa ndiyo wanasiasa wetu. Dahhhhhhhh
Kansa kubwa ni Lowassa ametumwa kuhakikisha chadema inakosa pumzi....na kinachofuata kwa sasa ni migogoro...bila kikomo!...tuliopiga kura 1995 tunaijuwa ccm.
 
Kwenye hilo tamko amedai hataki mambo yake na bishara za rafiki zake ziletewe zengwe , in short alihama ukawa kwa ajili ya maslahi binafsi karudi kwa maslahi binafsi , bahati mbaya ndio kachelewa ...

Alafu ukawa inamaana wangeshinda huyu jamaa angekuwa waZiri .. Hahaha
hata hivyo ahadi ziliwekwa ili zivunjwe kwa hiyo nadhani huwenda asingepata alichoahidiwa
 
Yaani anaongea kama hana meno mdomoni ningekuwa ccm ningefukuzia mbAli kwanza kaonesha ubinafsi alikuja chadema kwa jili ya kupewa kitu anarudi ccm kwa kuogopa mambo yake kukwama akumbuke huyu si mkwele kama unajipu we ndiwe wa kwanza kutumbuliwa
 
Homeboy Mwapachu kwa maelezo haya? Bado nitakuwa naota katika hili
 
Naona lile shirika la Regional Aviation analoendesha mtoto wake pale Arusha ndilo limemfanya huyu mzee kurudi mbio CCM... Baada mtoto wake ana kesi kibao kule mahakama kuu ya Arusha za kulangua wafanyakazi wa hiyo Kampuni...
Chezea Chama usichezee Mkuu wa nchi. Juzi juzi Arusha kwenye mkutano wa EA Mkulu alimpita Kama hamjui..nafikiri hilo pia lilimshtua sana hakulitegemea. Na kasheshe anazozipata uraiani.
 
Au...inawezekana kweli karudi lakini kuna wajanja wajanja wakaandika kuhusu hiyo habari na kuiongezea binzari, paprika, nyanya chungu, na mengineyo.

Kama ni hivyo basi inanikumbusha ile habari potofu ya Donald Trump na Waafrika.

Donald Trump kweli ni mtu mwenye tabia ya kutoa kauli tata.

Lakini, si kweli kwamba keshawahi kuwasema vibaya Waafrika na/ au viongozi wake.

Huo ni uzushi. Lakini kwa vile tayari mtu mwenyewe ana historia ya kutoa kauli tata, watu wakisikia kawasema vibaya Waafrika, watakuwa wako inclined kuamini kuwa ni kweli kasema kwa sababu ya preconceived notions walizonazo dhidi yake.


Ila navyomjua mwapachu ana uandishi mzuri sana...sio kama huu

Nina wasiwasi kama andiko hili ni la kwake.......Kama ni la kwake basi Njaa mbaya
 
Hahahahah Mpwa umeona watu wanavyozeeka vibaya? Haya sijui kaahidiwa nini sasa hivi hahahaha maana pia anarudi kwa jili ya Magufuli
Duh mbona sisi tusiowahi shika hata cheo cha ukatibu kata hatuhangaiki hivi? Inakuaje wazee wasomi na walioogelea kwenye vyeo miaka nenda rudi wana kuwa waoga wa maisha namna hii?

Aisee Ndio maana nchi hii kupata maendeleo bado sana!!
 
Kumbe alienda ukawa Baada ya kuaidiwa waziri nilifikiri alienda kwa nia ya kuwatumikia wananchi hata kama hamna chemo
Anasema anaogopa shughuli zake kusimamia Huyu naye ni jipu atumbuliwe tu
 
Statement ya Mwapachu inathibitisha mambo yaliyokuwa yanaandikwa hapa jamvini, kwamba Lowassa kaiteka CHADEMA na watu wake ndio walikuwa mstari wa mbele kwenye kampeni. Sasa Mwapachu anathibitisha hata vyeo vilishaahidiwa kwa watu wa Lowassa. Wakina Mnyika, Nassari na wana CHADEMA wengine walikuwa wanapigwa virungu wametoswa baharini. Na hata sasa bado Lowassa ndiye anakiendesha hicho chama. Uteuzi wa Katibu mkuu unafanana sana na kitu walichokifanya CCM mara baada ya uchaguzi wa 2005 ambapo walimteua asiye na sauti mbele yao Mzee Makamba kuwa katibu mkuu wa CCM.

CHADEMA kinaelekea kizumu na wa kumlaumu ni Mbowe.
 
Back
Top Bottom