Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya Kamati Kutathmini Ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo tarehe 12 Oktoba, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Akisoma mapendekezo ya Kamati ya Kutathmini Ufanisi na utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mwenyekiti wa kamati hiyo Balozi Hassan Simba Yahya amesema Majukumu ya utangamano wa Afrika Mashariki yahamishwe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, na iundwe wizara kamili itakayoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.
Ushauri huu umetolewa ili kuongeza usimamizi madhubuti wa Maslahi ya Tanzania kwenye Jumuiya hii, Ongezeko la idadi ya wanachama wa jumuia hiyo huku nyingi zikiwa na matarajio makubwa ya mchango wa Tanzania katika mstakabali wa jumuiya hiyo, kukua kwa uchumi wa nchi wanachama pamoja na kuenzi heshima ya Tanzania ya kuwa makao makuu ya umoja huu.
Majukumu mengine ya utangamano yataendelea kusimamiwa na Wizara ya Mambo ya nje.
Aidha, kamati imeshauri kuhamisha kwa muda majukumu ya Wizara ya Mambo ya nje kuwa chini ya ofisi ya Rais kama hatua ya mpito ili ijengwe upya pamoja na kubadili jina la wizara kuwa Wizara ya Ushirikiano wa Kimataifa (Ministry of International Cooperation) ili kuaksi azma ya Serikali ya kutumia diplomasia ya uchumi katika kujenga ushirikiano wa kimataifa. Jina la "Mambo ya nje" haliakisi vizuri majukumu ya wizara.
Pia, Kamati imeshauri kuwa na stability ya viongozi kwenye wizara hii.