Balozi/Mwalimu Edward Mhina amefariki Dunia Leo Jijini Dar-es-Salaam Tanzania.Mzee Mhina amefariki Dunia nyumbani kwake Makongo Juu.Habari za Msiba na mazishi Mtaarifiwa Baadaye.
Heshima mbele Balozi Mwawado,
Mungu awape faraja wafiwa, na amuweke mahali pema peponi marehemu, Balozi Mwawado tupe wasifu wa marehemu ikiwezekana.
Respect.
Mkuu naomba uiondoe hiyo hadhi ya Ubalozi!!...Niite Mjasiriamali.
Wasifu wa Balozi Mhina aliwahi kuwa Mkuu wa shule ya kati/sekondari wa Kwanza Mwafrika huko Malangali - Iringa,Aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Elimu Kibaha kabla ya kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu.
Mwaka 1972/73 Mwalimu Nyerere, alimteua kuwa Balozi wetu wa kwanza huko Scandinavia (Sweden,Norway,Finland na Denmark),alikaa Sweden kwa kipindi cha Miaka 10 na kurudi Tanzania 1984.Alipokuwa Stokholm alikuza kwa kiwango kikubwa Ushirikiano wetu na Sweden...Familia yake ina urafiki wa karibu na Familia ya Marehemu Waziri Mkuu olof Palme.
Aliporudi Tanzania alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Elimu na Baadaye kuwa Mwenyekiti kwenye Bodi ya SIDO.
Marehemu ameacha watoto (nane) Lucy,Anita,Eva,Tino,Peter,Teddy,Samwel na Kicheba na Wajukuu kadhaa.Mwili wa marehemu utasafirishwa kwa ajili ya mazishi huko kwao Tongwe - Muheza,Tanga kwenye Tarehe itakayopangwa na wanafamilia.
Msiba upo nyumbani kwa Marehemu Makongo,na wanasubiriwa watoto wa Marehemu kutoka Sweden,Us,Ethiopia na Jordan kwa ajili ya utaratibu wa mazishi.
Mwenyezi Mungu amlaze marehemu mahali pema peponi!!