Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile ameeleza kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania imetenda kwa mujibu wa sheria katika kumtia hatiani na kumhukumu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Antiphas Lissu, kifungo cha miaka minne jela kwa kosa la uchochezi.
Balile ameyasema hayo akizungumzia uamuzi huo wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, uliomvua Lissu mashtaka ya uhaini na kumtia hatiani kwa kosa dogo la uchochezi, huku akisisitiza kuwa njia pekee ya kuijenga nchi ni kurejea kwenye meza ya mazungumzo.
“Bado ninaamini mlango wa kuzungumza upo kwamba mheshimiwa Rais anayo nafasi katika hili, hakuna kosa ambalo Rais hawezi kusamehe, hakuna hukumu ambayo rais hawezi kusamehe kwa mujibu wa sheria.
Kwahiyo hapa mazungumzo yaendelee kwamba CHADEMA, CCM, Watanzania kwa ujumla tuangalie tunaijengaje nchi yetu, maana nimesema mara kadhaa hata tukipambana kwa kiwango gani mwisho wa siku tutarudi kwenye meza ya mazungumzo”, ameeleza Balile.
Pia soma:
BREAKING: Tundu Antipas Lissu afungwa miaka 4 kwa kosa dogo la Uchoc