PostGE2025 Balile: Lissu alifanya uchochezi

PostGE2025 Balile: Lissu alifanya uchochezi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,179
Reaction score
4,295

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile ameeleza kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania imetenda kwa mujibu wa sheria katika kumtia hatiani na kumhukumu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Antiphas Lissu, kifungo cha miaka minne jela kwa kosa la uchochezi.

Balile ameyasema hayo akizungumzia uamuzi huo wa Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, uliomvua Lissu mashtaka ya uhaini na kumtia hatiani kwa kosa dogo la uchochezi, huku akisisitiza kuwa njia pekee ya kuijenga nchi ni kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

“Bado ninaamini mlango wa kuzungumza upo kwamba mheshimiwa Rais anayo nafasi katika hili, hakuna kosa ambalo Rais hawezi kusamehe, hakuna hukumu ambayo rais hawezi kusamehe kwa mujibu wa sheria.

Kwahiyo hapa mazungumzo yaendelee kwamba CHADEMA, CCM, Watanzania kwa ujumla tuangalie tunaijengaje nchi yetu, maana nimesema mara kadhaa hata tukipambana kwa kiwango gani mwisho wa siku tutarudi kwenye meza ya mazungumzo”, ameeleza Balile.

Pia soma: BREAKING: Tundu Antipas Lissu afungwa miaka 4 kwa kosa dogo la Uchochezi
 
Serekali yetu na vyombo vyake imetumia utu wa hali ya juu sana,ingelikuwa ni ""Pyongyang"" mpaka muda huu hatunaye!
 
Serekali yetu na vyombo vyake imetumia utu wa hali ya juu sana,ingelikuwa ni ""Pyongyang"" mpaka muda huu hatunaye!
Serikali yenu na nani acha usenge bwana mdogo! Alafu si tulikubaliana serikali yako sikivu lazima imnyonge TAL sasa mbona mmebadilisha tena mapambio mnafurahia tena hukumu ya Jana? Hii inaonyesha watawala wanawafaidi sana nyumbu kama wewe
 
Utaruka ruka tu,lakini ndiyo serekali yetu,sikuwahi kusema neno kunyonga kamwe,nilisisitiza kifungo cha miaka mitano,cha nje!,huku akizuiwa kufanya shughuli za kisiasa ndani ya kifungo.
 
Huyo ndiye kiongozi wa wahariri ambao wanategemewa wafanyakazi wao wafànye kazi mujibu wa muongozo wao unaowataka bila upendeleo Wafuate utaratibu wa 5W, 1H.

Ili taarifa inapomfikia mlaji yaani msomaji, msikilizaji na mtazamaji yeye ndie awe msemaji au muamuzi wa alichokipokea kutoka kwenye chombo cha habari, kwa viongozi kama hawa.

Bado tuna safari ndefu sana kwenye tasnia ya habari.
 
Back
Top Bottom