Ujio wa ghafla (kama ni kweli ni ghafla)wa T.B. Joshua Tanzania na kupokelewa na Magufuli mshindi wa ccm kiti cha urais na kukanyaga ardhi ya Tanzania pekupeku (japo alikuwa kavaa soksi kwahiyo sio pekupeku kabisa) kulizua mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii na wengi wakitabiri kama ni uchuro na balaa ...mimi napingana nao
T.B. Joshua na umaarufu wake hawezi kuleta balaa lolote ni kiumbe mdogo sana kwenye huu ulimwengu yeye alishuka kama dismainder fulani hivi, wamekuja na ndege yake kavaa alivyovaa hajali protocol, safarini aliamua kuvua viatu miguu ipumue (waliopanda ndege hata magari ya masafa marefu wanakua ni kwanini). Kwahiyo kwake ilikuwa ni sawa tu hata angeamua kuvaa bukta ...halafu awaachie walimwengu waje na tafsiri zao lukuki
Kwahiyo yeye hana uwezo huo wa kutuletea mabalaa bali mabalaa yataletwa na wale walioshika misahafu na kula kiapo cha ushindi wao bandia tena mbele ya maelfu ya watu..hii ni dhihaka na dharau kubwa mbele za Mungu. Hakuna jambo baya kama kumshirikisha Mungu kwenye dhambi na kumuomba akusaidie kuhalalisha udhalimu wa waziwazi ulioufanya...Mungu si wa maskhara kihivyo
Kama kweli Mungu au whatever ataamua kushusha mabalaa na kuadhibu asilaumiwe T.B.Joshua bali wale wote walioshiriki udhalimu na kushika misahafu