Balaa halitaletwa na T.B. Joshua

Balaa halitaletwa na T.B. Joshua

Ujio wa ghafla (kama ni kweli ni ghafla)wa T.B. Joshua Tanzania na kupokelewa na Magufuli mshindi wa ccm kiti cha urais na kukanyaga ardhi ya Tanzania pekupeku (japo alikuwa kavaa soksi kwahiyo sio pekupeku kabisa) kulizua mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii na wengi wakitabiri kama ni uchuro na balaa ...mimi napingana nao

T.B. Joshua na umaarufu wake hawezi kuleta balaa lolote ni kiumbe mdogo sana kwenye huu ulimwengu yeye alishuka kama dismainder fulani hivi, wamekuja na ndege yake kavaa alivyovaa hajali protocol, safarini aliamua kuvua viatu miguu ipumue (waliopanda ndege hata magari ya masafa marefu wanakua ni kwanini). Kwahiyo kwake ilikuwa ni sawa tu hata angeamua kuvaa bukta ...halafu awaachie walimwengu waje na tafsiri zao lukuki

Kwahiyo yeye hana uwezo huo wa kutuletea mabalaa bali mabalaa yataletwa na wale walioshika misahafu na kula kiapo cha ushindi wao bandia tena mbele ya maelfu ya watu..hii ni dhihaka na dharau kubwa mbele za Mungu. Hakuna jambo baya kama kumshirikisha Mungu kwenye dhambi na kumuomba akusaidie kuhalalisha udhalimu wa waziwazi ulioufanya...Mungu si wa maskhara kihivyo
Kama kweli Mungu au whatever ataamua kushusha mabalaa na kuadhibu asilaumiwe T.B.Joshua bali wale wote walioshiriki udhalimu na kushika misahafu

Umenena vema Mshanajr Like
 
Anayetakiwa ktuoa ushahidi ni yule anayedai kuibiwa kura na kupinga matokeo yaliyotangazwa katika utaratibu uliowekwa. Sasa mtu au watu wanakuja na ngonjera kuwa tumeibiwa kura hawatoi hata jimbo moja au nusu ya jimbo ambapo kura zilizotangazwa na Tume zinatofautiana na kura zilizobandikwa na kusiniwa halafu mtu mwenye akili timamu unawasikiliza watu wenye madai upuuzi kama hayo??? Ina maana wameshindwa kutoa ushahidi hata 10%, sio 100% unaouzungumzia wewe. Watanzania tusiwe tunapeleka ufahamu wetu likizo zisizo za lazima. Angalau angetoa data za jimbo moja tu kwenye hiyo discrepancy. But none and yet some Tanzanians entertain this nonsense.

Hebu MTU hata mmoja ajitokeze na kusema kuwa huu ushindi ni 100% genuine na aape kuwa anao uhakika huo na yuko tayari Mungu amlaani kama kasema uongo.
 
Samia Suluhu aliapa kwa kutumia kitabu gani? Jibu hilo kwanza achana na blah blah nyingine

Kwahiyo wewe unawahesabu watakao apa kwa Msahafu tuu?? Wengine huwaoni??

Wewe Kiumbe huna jipya unajishushia heshima tu kadiri siku zinavyokwenda,nilikuwa nakuona wa maana sana ila toka umeanza hii tabia ya kudharau dini za watu nimekudharau sanaaaa!! Na hiyo mi topic yako ya kichawi wapelekee wachawi wenzako!!

Watu wapo kwenye ulimwengu wa Sayansi na teknolojia wewe unapoteza time ya umri wako kuponda dini fulani!! Ili ikusaidie nini??

Kama huna cha kufanya jaribu hata kufuga Kuku kuliko kutuletea Chuki za kidini humu..
 
Hivi wewe unalaana na huo uislamu wako wakigaidi mpuuzi wewe?mnaswali mara tano lakini haiwasaidii!ndo maana Hamna elimu wajinga nyie!


Jifundishe kuwa MUELEWA
hapo unahukumu waislamu wote huoni kama akili yako ina Upofu wa hali ya juu?? Ujinga nao ni kipaji Hongera sana
 
hebu mtu hata mmoja ajitokeze na kusema kuwa huu ushindi ni 100% genuine na aape kuwa anao uhakika huo na yuko tayari mungu amlaani kama kasema uongo.

chaguzi zimeisha tupige kazi mambo ya kujadili huyu kafanya nn si sahihi. Rais tumempata tujumuike pamoja kujenga nchi.
 
Darsa naona limekuingia na haukurudia kujifanya hujui Qur'an.

Huyo mchonga ndiyo nani?

Umeanza kuwa mpole! Halafu Leo humjui mchonga...what a shame...!!! Between ff una shida moja kubwa sana una umri mkubwa lakini akili yako haitofautiani na Mtoto wa miaka 16 huu ni ulemavu wa kubemendwa udogoni
 
Hapa JF uliletwa ushahidi wa lori lililo kamatwa na mabox ya kura zilizopigwa tayari. Kule Kagera/ Geita karatasi za kura zilizopigwa tayari tulionyeshwa zikiwa zimetupwa shule ya sekondari. Unataka nini tena kudhibitisha kuwa kulikuwa na wizi?

Kumbe uko mbali sana na UKAWA na Lowasa wao. Wanachodai wenzio ni kuwa kura zilizobandikwa ikiwa ni pamoja na hizo kwenye malori unayosema zinaonyesha Lowasa alishinda alipata zaidi ya kura 10milioni. Akiambiwa atoe ushahidi wa data analeta ngonjera. Kumbe hata wengine hamjui kuna kesi gani ila mnashabikia tu. Kwa kweli wajinga ndio waliwao
 
Shibe ya tumbo si shibe ya ubongo. Unaweza kuwa libaba lizima na familia lakini ukawa na akili za litoto lidogo lenye makamasikamasi.
Note: Kama huna hoja ya maana juu ya jambo lolote ni bora kuliacha kama lilivyo.
 
Unajua humu si kama mnavyodhani, waweza kuwa unaropoka unadhani uko sahihi kumbe kona ya pili yupo atakayekusaidia kesho nawe hujui unajitanabaisha jinsi ulivyo wa ajabu ndio sababu Mtoa mada akasema kama huelewi si vyema kuchangia pita kimyakimya nenda zako sasa kujionyesha kuwa wewe ni usiyepitwa ndio unajikuta ukurupuka tu kutaka kuchangia kila uzi humu na uzi ukiwa haushabihiani nao ndipo unatafuta vijikasoro tu upate pa kuanzia kujidhalilisha kwa lugha chafu, dhihaka, chuki nk kumbe hata unachojidai kukitetea hata hukiishi ni mbabaishaji tu,
Tubadilike.
 
Kwahiyo wewe unawahesabu watakao apa kwa Msahafu tuu?? Wengine huwaoni??

Wewe Kiumbe huna jipya unajishushia heshima tu kadiri siku zinavyokwenda,nilikuwa nakuona wa maana sana ila toka umeanza hii tabia ya kudharau dini za watu nimekudharau sanaaaa!! Na hiyo mi topic yako ya kichawi wapelekee wachawi wenzako!!

Watu wapo kwenye ulimwengu wa Sayansi na teknolojia wewe unapoteza time ya umri wako kuponda dini fulani!! Ili ikusaidie nini??

Kama huna cha kufanya jaribu hata kufuga Kuku kuliko kutuletea Chuki za kidini humu..

Duu kwanza sihitaji heshima yako hata kidogo..! kwangu wewe si lolote si chochote, ushauri wako jishauri mwenyewe utasaidika
Usiwe na papara za kupost tulia tafakari pima kisha ujiridhishe kama unaweza kujibu ama la
Nimekuuliza swali moja rahisi sana lakini umeshindwa kujibu badala yake unakuja na mipasho ya kiswazi

Nakuuliza tena Samia suluhu alitumia nini kuapa pale national stadium? Halafu unionyeshe hiyo dharau unayozungumzia wewe
 
nabii alichoonyesha kwa hii nchi takatifu ya tz ni unyenyekevu na kuachana na misifa. kavua viatu katembea bila viatu ni unyenyekevu. kasema mara nyingi mungu huonyesha baraka na ushindi penye masononeko lakini kubwa ni kuonyesha unyenyekevu kwa hiyo yaliyotokea tuyakubali kwa kadri mungu alivyoyaleta. tuache kusononeka tusonge mbele.
 
Huo ni ukweli 100% yeye Tb Joshua anachoweza kufanya kwa hilo tendo la kuja pekupeku anaweza kutabiri tu yanayoweza kutokea ila si kusababisha.

Sababu za vurugu ni Haki kutotendeka na Kukosekana kwa usawa ktk jamii baina ya wenye/wasionacho.

Niulize hivi wana Ccm wote huwa wanaenda ikulu kila ijumaa kugawiwa pesa?maana naona hali ngumu ya maisha wanaona kawaida.wanaenda masoko gani?

Thread iko okey.
 
Back
Top Bottom