Akili za MUDI, za kijinga kabisa!
Kwa nini hii mada imekuwa ngumu kueleweka kiasi hiki? Rudia kusoma tena tafadhali hasa main n core points
Mimi nime challenge kiliandikwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa TB Joshua ataleta mabalaa nchini kwa kushuka kwenye ardhi ya Tanzania akiwa peku peku (kiukweli hakuwa pekupeku alikuwa kavaa soksi)
Kisha nikahitimisha kwa kusema kuwa kama ni mabalaa yataletwa na wale walioshika misahafu na kuapa huku wakijua kuwa kuna udhalimu mkubwa ulifanyika (hili nitalisimamia)
Sasa naona point muhimu zimeachwa tumebaki na personal attacks na wizi wa kura hebu tuwe watu wa tafakuri jadidi
Unaposema mabalaa yataletwa na walioapa kwa kushika "Misahafu" hapo ndipo ulipokosea,kwanini ukomalie kwa walioapa kwa Misahafu tuu?? Hakuna aliyeapa kwa Kitabu cha dini nyingine? Hayo mabalaa hayawezi kuletwa kwa vitabu vingine ila Misahafu tuu?? Hapo ndipo ulipo onyesha chuki zako za wazi kabisa kwa dini fulani,
Mabalaa yanaweza kuletwa kwa kumkasirisha Mungu kwa kufanya mambo mabaya aliyoyakataza, kama vile Zinaa na Wizi,
Mungu hasubiri mpaka uape ndipo alete mabalaa,lakini wewe kwa fikra zako umekimbilia kuisema Misahafu tu!!
Siku nyingine uwe unatafakari kabla ya kuandika kitu sio kukurupuka tu kama Chafya,
Huna issue piga kimya sio kutuletea chuki na mifarakano ya kidini humu,
Watu wanatangaza amani na upendo wewe unatuletea chuki zako kwa Kitabu cha dini fulani..
Hakuna mwenye ubavu huo. Wanadhani Mungu ni wakuchezewa.Hebu MTU hata mmoja ajitokeze na kusema kuwa huu ushindi ni 100% genuine na aape kuwa anao uhakika huo na yuko tayari Mungu amlaani kama kasema uongo.
Hao hawana hofu ya Mungu so they didn't care then and they certainly do not care now!Ujio wa ghafla (kama ni kweli ni ghafla)wa T.B. Joshua Tanzania na kupokelewa na Magufuli mshindi wa ccm kiti cha urais na kukanyaga ardhi ya Tanzania pekupeku (japo alikuwa kavaa soksi kwahiyo sio pekupeku kabisa) kulizua mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii na wengi wakitabiri kama ni uchuro na balaa ...mimi napingana nao
T.B. Joshua na umaarufu wake hawezi kuleta balaa lolote ni kiumbe mdogo sana kwenye huu ulimwengu yeye alishuka kama dismainder fulani hivi, wamekuja na ndege yake kavaa alivyovaa hajali protocol, safarini aliamua kuvua viatu miguu ipumue (waliopanda ndege hata magari ya masafa marefu wanakua ni kwanini). Kwahiyo kwake ilikuwa ni sawa tu hata angeamua kuvaa bukta ...halafu awaachie walimwengu waje na tafsiri zao lukuki
Kwahiyo yeye hana uwezo huo wa kutuletea mabalaa bali mabalaa yataletwa na wale walioshika misahafu na kula kiapo cha ushindi wao bandia tena mbele ya maelfu ya watu..hii ni dhihaka na dharau kubwa mbele za Mungu. Hakuna jambo baya kama kumshirikisha Mungu kwenye dhambi na kumuomba akusaidie kuhalalisha udhalimu wa waziwazi ulioufanya...Mungu si wa maskhara kihivyo
Kama kweli Mungu au whatever ataamua kushusha mabalaa na kuadhibu asilaumiwe T.B.Joshua bali wale wote walioshiriki udhalimu na kushika misahafu
mshana jr
Kuna wakati tumia extra vision kujua nini umjibu mtu kutegeneana na elimu/mada uliyotoa.
Hii ina maana hii hapa, ''mf. Ukiwa bank pale counter kuna karatasi imebandikwa ikiwa na maneno flani kama, 'hakikisha pesa zako kabla hujaondoka' kwani kuna aina ya binadamu huwa wanasubiri makosa au wameguswa vipi na kile kilichowakilishwa na mwingine!.
Msemo wa maneno ya Yesu kristo kwenye msaafu wa Biblia alisema "...asiye na kosa awe wa kwanza kumpiga mwanamke huyu kwa mawe," yaliitimishwa kwa wale waliomshitaki yule mama kuondoka mmoja mmoja kichwa chini.
Sawa kiongozi!Hapana waarabu ndo wanasema kalas wahindi wanasema kushney
Queen Esther, Wewe unaangalia upande mmoja wa maandiko. Biblia inasema haki siku zote huinua taifa methali 14:34. Misingi ya kiti cha enzi cha MUNGU Baba ni haki na hukumu Zaburi 89:14. MUNGU kamwe hawezi kwenda kinyume na neno lake ili kutimiza mapenzi, kwani YEYE huliangalia neno lake ili alitimize Yeremia 1:12, ikiwemo kutumia hila. MUNGU pia ni mwingi wa rehema kabla ya kuangamiza Ninawi alimtuma Yona kuwaonya wahusika na wahusika waligeuka. Kama wahusika waliletewa ujumbe wakapuuza, hawawezi kumlaumu MUNGU gharika likiwapata. Kumbuka pia mfalme Yehoshapat na miji yote ya Judah walifunga na kuomba ili MUNGU walipotaka kuvamiwa na moab and the amoon. Mfalme naye alijinyenyekesha hakuupuza kama wengine ambavyo hufanya soma 2 Nyakati 20 yote ukipata muda. Baada ya taifa zima alikiwepo mfalme kujinyenyekesha mbele za MUNGU kupitia nabii Jahaziel mwana wa Zechariah na kusema msiogope kwa ajili ya umati huu, vita hivi ni vya Bwana. Kumbuka mfalme hakupuuza. Ninawi baada ya kupata habari kutoka kwa nabii yona, Ninawi yote wakiwepo watawala na hata wanyama walifunga kuomba rehema, watawala hawakupuuza sauti ya MUNGU.
YESU alisema katika mathayo 10:14, If anyone will not welcome you or listen to your words, leave that home or town and shake the dust off your feet, 15: truly I say to you, it will be more tolerable for the land of Sodom and Gomorrah in the day of judgment than for that city.
Neno la MUNGU ni upanga ukatao kuwili, usitumie tu kwa kujifavor wewe, simamia ukweli kama wewe kweli umeokoka na umeitwa kwa jina la Bwana. Usipotoshe. MUNGU kamwe hadhihakiwi apandacho mtu ndicho avunacho, mshahara wa dhambi ni mauti. Kumbuka pia Whoever remains stiff-necked after many rebukes will suddenly be destroyed--without remedy methali 29:1. Ni kweli ni MUNGU wa rehema ndio maana anatoa maonyo kwanza, mtu akipuuza basi MUNGU anakuwa hana jinsi. Hiyo ndiyo torati na manabii, injili ya Kweli isiyogoshiwa.
Shalom! Shalom!
Mkuu jiheshimu,, misahafu hapo inahusikaje???
Sina shida na neno la Mungu mpendwa mtumishi mwenzangu. Shida yangu ni pale neno linapotumiwa kuufurahisha moyo au NIA ya mtu. Moyo wa mwanadamu umejaa uovu.
Kwanza maandiko yalitumiwa sana wakati wa uchaguzi kuwa Lowassa atakuwa Rais. Sasa matokeo yamekuja tofauti mnasema kura ziliibwa; Gwajima alisema ameweka walinzi ktk ulimwengu wa Roho hata kura moja haitaibiwa. Pia Mhe. Lowassa akasema atashinda saa asubuhi na mapema hata kabla watu hawajamaliza kupiga kura. Ina maana Mungu aliyaruhusu haya yote. Swali linakuja kwanini aliruhusu?? Je na hayo maunabii yalikuwa yauongo??
Sasa mmeibuka kuitakia TZ mabaya. Nyie ni watu wa namna gani jamani?? Sielewi ukristo huu hata kidogo wa kutafuta maandiko ili kutafuta mabaya kwa mtu mwingine.
Ngoja nimalizie kwa kukuambia wakati wengine wanatamani mabaya yaje TZ wengine wanamuomba Mungu mema yaje TZ (Zaburi 91). Mungu siku zote anapaa upande wa haki. Mabaya yenu yasipotimia msitafute mistari mipya, ingieni kwenye toba.
Queen Esther
huwez ukamuelewa tb joshua kwasasa had litokee jambo
........waabudu watu !
Sisi tunamuabudu Allah SWT.
'Na waambie wale wasio amini (makafiri): Fanyeni muwezavyo, nasi pia tunafanya (tuwezavyo).
'Na ngojeni (siku ya mwisho) nasi tunangoja !
'Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyo fichikana katika ardhi na mbinguni, na mambo yote yatarejeshwa kwake. Basi (nyinyi Waislaam) mwabuduni Yeye. Na Mola wako Mlezi haghafiliki na yale mnayoyatenda.
Qur'an: 11:121-123
Hukuona wale walioshika Biblia na Koran pale uwanja wa Taifa tena wakisema ee Mungu unisaidie