Bakwata yaishtukia serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bakwata yaishtukia serikali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ami, May 14, 2010.

 1. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mkutano ulioitishwa na ofisi ya waziri mkuu kati yake kwa niaba ya serikali na viongozi wa dini uliingia dosari hapo jana na kushindwa kuendelea baada ya ujumbe wa waislamu uliowashirikisha Bakwata tu kutilia shaka mwaliko huo.

  "Mheshimiwa mwenyekiti naomba uwakilishi wa Waislam katika mkutano huu uongezeke... tukitizama uhalisia, idadi ya Waislam na Wakristo haitofautiani sana, lakini ndani ya mkutano huu Waislam tupo 15 wakati wenzetu wapo zaidi ya 40! "...Nasema hivi kwa sababu na sisi Waislam tunayo Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu ambazo hazipo BAKWATA nao wana waumini wao na ninyi mlivyotuletea mwaliko mmeweka idadi ya viongozi 15 tu, sasa kwa mantiki hii lengo lenu kwa upande wetu halitatimia," alisema Sheikh Lolila.
  ...........................................................................................................
  Huu ni upendeleo wa wazi ambao hata hao waliokuwa wakipendelewa ili kujenga tabaka wameshtuka.
   
 2. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hawana hoja kazi kutafuta conflicts zisizo na msingi, idadi ya wajumbe inahusiana nini na michango ya mawazo kwani wanakwenda kupiga kura, kama wana hoja za nguvu hata wajumbe wawili wanatosha kuwakilisha kwa vile hazimnamo wanafikiri uwingi wa wajumbe ndiyo hoja, hovyooo.
   
 3. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  inferiority complex tu
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Mimi sidhani kama ni inferiority complex. Kama kwa mfano walioitisha mkutano walitaka kuzingatia uwakilishi wa kidini na wakafanya hivyo kwa wakristo (mfano wakawaalika KKKT, RC, AGT, etc) na kusahahu kufanya vivyo hivyo kwa waislamu na dini nyingine nadhani upo uhalali kwa waislamu au dini hizo nyingine kulalamika.

  Serikali ni lazima wawe sensitive kwenye masuala haya ya dini. Kwa mfano si sahihi kudhani kuna waislamu na wakristo pekee....wapo wengine hata kama ni monority ambao pengine hawana mahala pengine pa kusemea.
   
 5. M

  MJM JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hii nchi imekuwa hivi sababu ya viongozi wetu wa serikali kuendekeza matabaka. Mara ngapi wapinzani wamekuja na mawazo ya maana wakaishia kudhihakiwa kwa sababu tu si chama tawala? Suala la mjadala huu kuelekea uchaguzi mkuu mawazo yangetoka kwa wadau mchanganyiko kwa kuwajumuisha viongozi wa dini, NGOs, CBOs, nk. Kwa kuwabagua viongozi wa dini peke yao inamaana kuna agenda ya siri. Hapo ndipo uwakilishi wa sawa kwa sawa unapotakiwa kama walivyodai viongozi wa waislam.

  Mi naona sawa sawa tu hadi hapo viongozi wa serikali watakapoona umuhimu wa kuheshimu mawazo ya mtu regardless of political, religious or political background. Mimi ni Mkristo lakini kwa hili nasimama upande wa vikundi vya wakristo na waislam waliotoswa kwani nao ni muhimu kwa mustakabali wa Taifa hili
   
 6. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Huna hoja kazi yako kurukia conflicts tu! Usipoona ukweli uliopo basi umepumbaazwa na hisia!
   
 7. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #7
  May 14, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  No! Ni superior complex ya upande wa pili!
   
 8. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #8
  May 14, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  :target:Hawana hoja kila siku wanalalamika bila sababu za msingi,wanataka serekali iwaalike wale wahuni shura ya maimu.hakuna haja serekali kusikiliza hoja za walioishiwa hoja ikibidi serekali iwatimua Bwakwata.
   
 9. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #9
  May 14, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mi naona hapo hakuna sababu ya msingi sana, zaidi imekaa kiitikadi bila elimu, kwani uwingi ndiyo uchangiaji wa mawazo? wanaweza wakaambiwa waende waislamu wote kote nchini, lakini wakawa maamuma kwa hoja husika na kushindwa kuichangia, kuna haja ya kubadilika kimtazamo hasa kwa kipindi hiki cha sayansi na teknolojia, pale si mahari kutaka kuchagua nani awe mtume wa mambo ya dini, hvyo waweze kuhoji kuwa watashindwa kutokana na idadi ndogo ya wanachama wao,


  Mentally Change is needed for them to overcome the situation.
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  May 14, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwanza aliyeitisha huu mkutano mwenyewe hana akili..mkutano kama huu ni wa nini? yaani nchi hii haina vipaumbele kabisa sijui kwa nini
   
 11. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #11
  May 14, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Ninapata taabu sana iwapo wanajamii [baadhi] wanaona ni hoja kuzungumzia wingi wa waislamu katika NEC-CCM na wengine wakizunguzia wingi viongozi wa kiislam ndani ya serikali ya JK na zote hizi zikawa hoja nzito jamvini lakini wachangiaji hao hao wanaona hoja ya Bakwata ni Hovyo I just dont understand some of u guys and babes
   
 12. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #12
  May 14, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Suala hapa sio idadi ya watu ni uwiano wa uwakilishi! ukiangalia idadi ya wakristo walioalikwa ni wazi walizingalitia uwakilishi wa kila dhehebu, lakini kwa idadi hiyo ya ndugu zetu waislamu ni wazi kabisa walioitisha huo mkutano hawakuzingatia uwakilishi wa madhehebu, na hili ndio tatizo mara nyingi watu hufikiri kuwa uislam ni dhehebu moja tu!
   
 13. a

  alles JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2010
  Joined: Oct 14, 2006
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau, sio BAKWATA peke yao walioishtukia serikali.Hata viongozi wengine wa dini wameshtuka.
  Pitieni iyo nakala chini. Muone watu walivyochoka kudanganywa.

  Padri: Viongozi wa dini msinunuliwe na serikali

  *Awataka kuwa mstali wa mbele kulikomboa taifa leo
  *Aonya miaka mitano ijayo hali ya nchi itakuwa mbaya

  Na Tumaini Makene

  WAKATI viongozi wa dini wanakutana na serikali jijini Dar es Salaam jana na leo, padri mmoja wa Kanisa Katoliki ameibuka na kuwatakja viongozi wasikubali kununuliwa wala kurubuni badala yake waweke msimamo wa kuleta mabadiliko nchini.

  Huku akihoji kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kutawala mpaka lini wakati maendeleo ya nchi yanazorota, Padri Baptiste Mapunda ambaye amekuwa mmoja wa watu walio mstari wa mbele katika kutoa maoni na kuchambua mwenendo wa utawala na watawala nchini, amesema kuwa wakati umefika wa kukiambia ukweli CCM kuwa kimeshindwa kuendesha nchi, kuwakemea mafisadi na kuwaletea maendeleo wananchi.

  Padri Mapunda ambaye ni mmoja wa viongozi wa Kanisa Katoliki nchini ambao wamekuwa wakizungumzia hadharani masuala mbalimbali ndani ya nchi, amewaambia wananchi kuwa muda wa kutumia kura zao vyema kuleta mabadiliko umefika, huku akiwataka kuacha kuhongwa fulana, pilau, pombe, kofia na vitenge, akisema uongozi haununuliwi, bali hupewa mtu anayefaa.

  Katika taarifa yake aliyoituma kwa Majira juzi, Padri Mapunda ambaye kwa sasa yuko nchini Kenya kwa Masomo ya Uandishi wa Habari, alisema kuwa kura ni silaha kubwa ambayo haipaswi kuchezewa inayoweza kuleta mapinduzi ya siasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

  Katika uchambuzi wake huo alioupatia kichwa cha habari kisemacho "Viongozi wa Dini msiweke Mkataba na CCM wala kuhongwa", Padri Mapunda alisisitiza kuwa viongozi wa dini zote nchini wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuliokoa taifa, kwani hali itazidi kuwa mbaya kama Watanzania wataendelea kuongozwa kwa mtindo uliopo sasa.

  "Ninashangaa ujasiri wa CCM kuwaita viongozi wa madhehebu ya dini na kuwaandalia semina. Semina hii inatia shaka kwa muda kama huu. Kwanza lazima ijulikane miezi michache ya nyuma serikali ya CCM ilikuwa na 'madharau makubwa sana' kwa viongozi wa dini kufuatia matamshi na nyaraka mbalimbali walizotoa.

  "Serikali imekuja kugundua kwamba viongozi wa dini wanashika watu wengi sana kuliko wanavyofanya wao katika majukwaa ya kisiasa. Dini ni suala nyeti sana katika jamii, kama mtu hajui basi ni kipofu," alisema Padri Mapunda huku akitoa mfano wa jinsi viongozi wa dini nchini Kenya wanavyotishia kukwamisha Rasimu ya Katiba mpya.

  Pia alitoa mfano wa wa Uingereza ambako kilichokuwa chama tawala cha Labour kimeondolewa madarakani kwa kupigwa dafrao katika uchaguzi na kilichokuwa chama pinzani cha Conservative, huku akiwataka viongozi wa dini waache kukibeba CCM ili watu washuhudie kiyama chake na akahoji "CCM inataka itawale miaka 100?"

  Aliwataka viongozi wa dini watumie nafasi yao kikamilifu na wala wasiwe sehemu ya kuendeleza ufisadi nchini. Akiongeza kuwa nchi inanuka kila aina ya ufisadi, akisema kuendelea kuiacha CCM itawale ni kufuru kwa Watanzania na kwa Mungu.

  "Viongozi wa dini msikubali kuhongwa wala kuweka mikataba ya kurudi nyuma na kupoozwa. Mkumbuke kuwa miaka mingine mitano ijayo hali ya Tanzania itakuwa mbaya sana kama tutaendelea na serikali hii kwa mtindo huu uliopo sasa. Mimi yangu macho nataka kuona viongozi wa dini sasa waongoze mapambano ya kuleta mapinduzi katika nchi ya Tanzania.

  "Nafasi ya viongozi wa dini popote pale inajulikana, msiwe sehemu ya kuendeleza Ufisadi nchini, bila viongozi wa dini nchi leo hii ingekuwa wapi? Mmeona Uingereza wamefanya demokrasia ya kweli, Labour wameng'olewa madarakani. Na CCM inataka itawale miaka mingapi 100? Huku ni kutafuta kufuru kwa Mungu na Watanzania kwa ujumla. Semina inayoendelea sasa hivi kati ya CCM na viongozi wa dini iwe ya kuiambia ukweli CCM kwamba sasa ikubali kwamba imeshindwa kuendesha nchi na kuwaletea maendeleo wananchi.

  "Imeshindwa kabisa kuwakemea mafisadi. Kwangu, itakuwa ni aibu kubwa kama viongozi wa dini watakula njama na CCM ama kupoozwa makali yao, naamini mtasimama kidete katika uchaguzi ujao. Acheni kuibeba CCM halafu tuone kiama chake," alisema Padri Mapunda.

  Aliwataka Watanzania kutumia haki ya kura zao kuleta mabadiliko nchini na kuachana na zawadi za kupita wanazohongwa wakati wa uchaguzi na viongozi wanaosaka madaraka, "Dawa ni moja tu, kama ukipewa rushwa ya kura, chukua, lakini kamwe usimpe kura maana amejidhihirisha kuwa HAFAI kabisa kuwa kiongozi, uongozi haununuliwi bali unapewa na watu wakiona unafaa."

  Pia alizungumzia suala la viongozi wenye umri mkubwa kung'ang'ania madaraka akiwataka vijana kuacha kuwavusha wazee katika nafasi mbalimbali, kwani dunia ya leo inahitaji vijana katika uongozi.

  "CCM lazima ishikishwe adabu, kwa mara zote karibu na uchaguzi inajaribu kunyenyekea sana kwa viongozi wa dini. Mimi nasema ni wakati wa kufanya unabii, nchi inazaidi kudidimia...Na kwa upande wa vijana, nawaasa acheni kuwavusha wazee katika nafasi mbalimbali. Pitisheni vijana wenzenu katika nafasi mbalimbali.

  "Dunia ya leo inahitaji vijana Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon aliyenyakua madaraka ana miaka 43 tu, mpo hapo vijana? Sasa hawa wazee wengi nchini Tanzania kwa nini wanang'ang'ania madaraka? Kuna nini ndani ya uongozi?" alihoji Padri Mapunda.
  Source:http://www.majira.co.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=171:padri-viongozi-wa-dini-msinunuli
   
 14. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Wangetaka kutenda haki basi kila Imam wa msikiti angealikwa maana katika dhehebu la wa-sunni kila msikiti unasimama wenyewe, hakuna mfumo kama walionao wamisheni wamashemasi, mapadiri, maskofu, makadinali n.k. Kwa vile tumetofautiana kiutawala basi hatuwezi kila kitu ikawa sawa kwa sawa. Wadai kuongezwa uwakilishi lakini si kwa sababu wamisheni wako wengi!

  Amandla....
   
 15. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #15
  May 14, 2010
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hao watu wa serikali hawapo makini and they are not sensitive at all. Wamefanya a fatal mistake. Wana sababu zipi za msingi za kualika viongozi wa kikristo 40 na wa kiislamu 15? Ni kutafuta chochoko na mfarakano usio na lazima. Incompetence in this government seems to be widespread and unlimited, hata kwenye mialiko linawashinda kutumia mantiki? Yaani hawakujua kwamba hii lingelete shida??!
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  May 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Katika hili Bakwata wana hoja; Tatizo ni kuwa serikali bado haikubali kuwa kuna waislamu nje ya Bakwata! Jambo la maana ni kutoa mwaliko kwa madhehebu yote ya kidini na kuwaacha waamue nani aje nani asije; ni kuweka idadi tu kuwa dhehebu linaweza kuleta wawakilishi say wasiozidi watano tena kwa njia nyepesi tu.

  a. Mnatangaza semina ya serikali na madhehebu ya dini (siyo viongozi wa dini) - kila dhehebu linaweza kutuma wajumbe wasiozidi wanne kwa mfano
  b. Madhehebu yanayotaka kushiriki yanajiandikisha kati muda uliowekwa
  c. Nafasi za semina ni watu sema 50 tu kwa hiyo wanaofika kwanza kutimiza idadi ndiyo hapo
  d. Kutoka hapo waliojiandikisha kwa muda na kufuata masharti wanapewa barua ya kuwathibitishia kushiriki kwao katika hizo semina.

  Sasa mkishafanya hivyo kama at end mtakuwa na Waislamu asilimia 70 na Wakristu asilimia 30 hakuna atakayelalamika; au kinyume chake. tatizo ni mmoja genius ambaye amekaa kwenye kiti chache enzi na kuanza kuamua "nani tumualike"! BAKWATA wamefanya vizuri kuamsha dhamira za serikali.
   
 17. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #17
  May 14, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mi mtazamo wangu ni kuwa semina ya nini katika muda huu wa kuelekea uchaguzi?. Semina ingekuwa na mantiki mwanzoni mwa awamu ya nne kuita viongozi wa dini na kuomba maoni yao na ushauri wa nini nchi ifanye katika miaka mitano ijayo ya uongozi. Sasa kama wao walikuwa wanajua watafanya nini na wameshindwa kufanya hivyo hii semina itasaidia nini wananchi? zaidi ya kupigia kampeni walewale walioshindwa kutekeleza waliyoyaahidi katika miaka mitano iliyopita. Yaani wanataka viongozi wa dini wadanganye waumini wao wakati wanajua kabisa maandishi kuwa yanawakataza kusema uongo?.

  CCM silaha yao kubwa ni kudumisha amani, lakini ukweli ni kwamba amani si sera ya chama bali ni attitude ya wananchi, na watanzania by nature ni watulivu japo sasa uvumilivu unaenda ukipungua kwa kufanywa mazuzu na watawala wanaowaogopea kila uchaguzi unapofika. "CCM ni chama pekee kinachotishia amani ya watanzania, mara nyingi wakiona wanashindwa kwenye chaguzi mbalimbali hutumia mbinu chafu ambazo ni vyanzo vya uvunjifu wa amani (bila haki amani ipo mashakani) kwa kuwa wao wanapolisi, jeshi, hivyo hulazimisha watakayo wao na si wananchi- hii ni hatari sana kwa afya ya amani na maendeleo ya nchi yetu". Siku wananchi wakisema basi tutashuhudia watu wanapelekwa The hague baada ya upatanishi.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  May 14, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hakuna cha hoja wala nini... Huu ni ujinga mkubwa wa serikali kutaka kuwagawa watu wake.. Ni lini serikali iwe inatoa mwaliko kwa viongozi wa dini kushiriki ktk mkutano ili iwe nini?..

  Sijawahi kuona Ofisi ya waziri mkuu wala rais wa nchi yeyote akifanya hivyo pasipo sababu maalum inayohusiana na dini hizo.
  Tatizo la tanzania viongozi wetu wote wanatumia kivuli cha dini kujipatia kura. wanawatumia viongozi wa dini kuwawezesha kushinda ktk chaguzi na hali kama hii inazidisha uhasama wa wazi baina ya waumini.

  Na kibaya zaidi sisi wenyewe kwa Ujinga na Ulimbukeni wetu tunaendekeza sana ujinga kama huu na kuupa sifa za kufikiria mapuingufu ya dini nyingine, tunapenda sana mialiko ya Ikulu au ofisi wa waziri mkuu pasipo sababu ya msingi ili mradi tuonekane tupo karibu zaidi na utawala..
   
 19. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #19
  May 14, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mimi nadhani hapa hamuitendei haki serikali. Mnalinganisha machungwa na maembe. Kama serikali imealika viongozi wamadhehebu ya dini basi bila shaka tofaut ya waalikwa itajitokeza. Kwa wakristu wakatoliki, waangalikana, waluteri, assemblies, presbyterians, pentecosts, church of the latter day saints, kakobez,African Inland Church, Moravians n.k. wote watawakilishwa maana kila moja ni dhehebu na lina uongozi wake unaotambulika. Kwa waislamu kuna sunni na upande wa wama'shia kuna bohora, ismailia basi. Upande wa Sunni hawana uwakilishi unaokubalika na wote, Bakwata hawana mamlaka kidini kama vile walivyo hao wengine. Kwa Sunni kila msikiti na kila muislamu anajisimamia, hakuna mwakilishi au hierachy kama ilivyo kwa wamisheni. Washia ndiyo wanamfumo unaofanana na wamisheni, hierarchy inayoeleweka, tatizo ni kuwa wenzao wanawaona feki. Ndiyo maana nilisema awali kama tulitaka kweli haki ifanyike basi viongozi wote wa Misikiti Tanzania wangealikwa ili kuwawakilisha wa'sunni. Hii dhahiri isingewezekana, basi kilichobaki serikali ingejitahidi kupata wawakilishi kutokana na vikundi vinavyogombea kuwakilisha dhehebu la wa'sunni. Nakubaliana nanyi kuwa kuwakaribisha Bakwata kulikuwa misguided. Lakini vivyo hivyo kudai parity katika uwakilishi ni kuwa disingenious.

  Amandla......
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  May 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ni kweli ni ujinga! Lakini naamini katika utendaji wa kazi mbalimbali serikali itakuwa inakutana na viongozi au watendaji wa dini mbalimbali haijalishi mada ni nini. La maana kwangu ni kuwa wakati inafanya hivyo (iwe ni kuzungumzia masuala ya elimu, afya, siasa, uchumi n.k) serikali inatoa mialiko. Hili ni jambo la kawaida mahali pote huwezi tu kusema "njooni" bila utaratibu maalumu. Lakini unapotoa mwaliko pia ni lazima uwe mwaliko ambao hautasababisha mgawanyiko kama walivyofanya sasa. Lakini nakubaliana kabisa kuwa ni ujinga kufanya mikutano ya namna hii bila ya kutumia akili! au kutoifanya kwa sababu ya kutotataka kuwashirikisha viongozi wa dini.
   
Loading...