Aga Khan na Viongozi wa BAKWATA 1980s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,265
AGA KHAN PATRON WA EAMWS ALIPOKUTANA NA VIONGOZI WA BAKWATA MIAKA YA 1980

Nakusudia In Shaa Allah kuweka hapa makala mbili au tatu hivi kueleza yaliyotokea baada ya miaka mingi na Aga Khan aliyekuwa Patron wa EAMWS kujaribu upya kusaidia Waislam wa Tanzania lakini safari hii kupitia BAKWATA.

Naamini yapo mafunzo makubwa kwetu na Waislam na wananchi kwa ujumla wataielewa historia ya BAKWATA na viongozi wake.

Aga Khan si mgeni Tanzania na waliomuingiza nchini ni Waislam katika miaka ya 1930 kwa ajili ya kutoa misaada kwa Waislam.

Katika miaka ya 1930 baba yake huyu Aga Khan wa sasa Shah Karim Al Hussein, Sir Sultan Mohamed Shah alitembelea Tanganyika na katika mradi mmoja wapo aliofika kuuangalia ulikuwa ujenzi wa shule ya Al Jamiatul Islamiyya School, Mtaa wa Agrrey na New Street uliokuwa ukijengwa na Waislam chini ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Katika hafla ile mwanafunzi aliyesoma risala mbele ya Aga Khan alikuwa Abdul Sykes.

Miaka mingi baadae Abdulwahid Sykes sasa kijana na mwanasiasa akajachaguliwa kuwa mjumbe katika Bodi ya Elimu ya Aga Khan).

Aga Khan alivutiwa sana na juhudi zile walizoonyesha Waislam wa Tanganyika za kutaka kujiendeleza katika elimu na akatoa fedha zilizowezesha kumaliza ujenzi wa shule yote kwa ukamilifu wake.

Aga Khan akatoa changamoto kwa Waislam wa Afrika Mashariki kuwa Muislam akichanga shilingi moja kwa ajili ya maendeleo ya umma yeye ataoa shilingi moja vilevile juu yake.

Huu ulikuwa sasa wakati wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS).

Kitendo hiki cha Aga Khan kilikuwa msaada mkubwa kwa Waislam kwani wakati wa ukoloni ni Ukristo pake yake ndiyo ulikuwa na fursa ya kupata misaada kutoka nje.

Ushirikiano huu wa Aga Khan na Waislam wa Tanganyika uliendelea vizuri sana.

Aga Khan kupitia EAMWS alijenga shule nyingi hadi kufikia sasa kutaka kujenga Chuo Kikuu cha Kiislam chini ya usimamizi wa Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Tewa Said Tewa na Aziz Khaki aliyekuwa mwakilishi wa Aga Khan Tanzania.

Hii ilikuwa mwaka 1968 baada ya Tanganyika kuwa huru.

Aga Khan na EAMWS kutaka kujenga chuo kikuu hapo ndiyo matatizo yakaanza baina ya Nyerere na uongozi wa EAMWS.

Kisa hiki ni maarufu hapana haja ya kukirejea.

Sasa tuingie kwenye kisa chenyewe.

Miaka mingi ikapita na mwishowe Nyerere akatoka madarakani na serikali ikashikwa na Ali Hassan Mwinyi.

Kwa takriban miaka 20 Aga Khan hakupata kutia mguu Tanzania.

Katika utawala wa Mwinyi Aga Khan akaja Tanzania.

Katika mazungumzo na Rais Mwinyi, Rais Mwinyi akaomba msaada wa Aga Khan katika nyanja tatu - Elimu, Kilimo na Afya.

Aga Khan akamueleza Rais Mwinyi kuwa Aga Khan walikuwapo Tanzania miaka ya nyuma wakisaidia katika elimu kupitia EAMWS.

Hili suala la elimu likamgusa sana Aga Khan kiasi cha yeye alipomaliza mazungumzo na Mwinyi akamwamrisha Katibu wa Elimu wa Aga Khan Tanzania, Riyaz Gulamani awakaribishe viongozi wa Waislam wa iliyokuwa EAMWS pamoja na viongozi wa BAKWATA katika chakula cha jioni ili wajadili maendeleo ya Waislam.

Katika viongozi wa EAMWS walioalikwa katika hafla ile alikuwa Tewa Said Tewa.

Kutoka BAKWATA walioalikwa walikuwa Sheikh Mkuu wa BAKWATA Hemed bin Jumaa, Adam Nasibu aliyekuwa katibu wa BAKWATA, Mustafa Songambele mzee wa CCM na mwanakamati katika BAKWATA na Waislam wengineo.

Kutoka EAMWS aliyealikwa alikuwa Tewa Said Tewa.

Baada ya chakula Aga Khan akawaeleza nia yake ya kuwaita na akawataka watoe wanachotaka wafanyiwe na Aga Khan katika elimu.

Hapa ndipo ''drama,' ilipoanza.

Akasimama kiongozi mmoja wa BAKWATA na mzee wa CCM, Mustafa Songambele, akamwambia Aga Khan, ''Serikali ya Tanzania inawatosheleza Waislam katika elimu na hawahitaji msaada kutoka kokote.''

Mustafa Songambele
Naomba nisimame hapa.

Mkasa huu kwa mara ya kwanza alinihadithia Riyaz Gulamani.
Sikuamini kama inaweza kuwa kweli.

Kisa hiki nikaja kuhadithiwa tena na Tewa Said Tewa kama vile alivyonihadithia Riyaz Gulamani.

Hapo ndipo nikaamini kuwa kisa kile hakika kilitokea na Mzee Tewa akanipa na jina la huyo aliyesema maneno yale.

Tuendelee.

Aga Khan kwa upole kabisa akajibu kuwa jana yake alikuwa na Rais na yeye kaomba msaada wa elimu.

Hapo sasa ndipo likazuka zogo baina ya viongozi wa BAKWATA na Waislam wengine mbele ya mgeni Aga Khan.

Kufupisha mkasa.

Kabla hajaondoka kufuatia yale aliyosikia na aliyoshuhudia, Aga Khan akamwambia Riyaz, ''Inaelekea hawa ndugu zetu bado hawajawa tayari lakini ushauri wangu ni kuwa uache mlango wetu wazi.

Siku yoyote watakapokuwa tayari basi tutatoa msaada.''Picha: Aga Khan na Songambele.

1699029860581.jpeg


1699029897170.jpeg
 
Kwanini ndgu Songambele alikataa msaada?

Raisi si alikua muislam na alilibatiki hilo, sasa Songambele alikua na mamlaka gani ya kumpinga raisi?
 
Hapo sasa ndipo likazuka zogo baina ya viongozi wa BAKWATA na Waislam wengine mbele ya mgeni Aga Khan

Mzee fafanua hapo
Uzalendo...
Yale maneno ya Mzee wa BAKWATA kuwa serikali inawatosheleza Waislam katika elimu ndiyo lilipingwa na Waislam wengine ambao walitegemea wampe Aga Khan kile walichokuwa wanahitaji katika elimu mathalan shule.

Kwa kuwa BAKWATA ndiyo mkutano ule ulikuwa wao kama wawakilishi wa Waislam wa Tanzania ikawa BAKWATA imekataa msaada wa Aga Khan.
 
Uzalendo...
Yale maneno ya Mzee wa BAKWATA kuwa serikali inawatosheleza Waislam katika elimu ndiyo lilipingwa na Waislam wengine ambao walitegemea wampe Aga Khan kile walichokuwa wanahitaji katika elimu mathalan shule.

Kwa kuwa BAKWATA ndiyo mkutano ule ulikuwa wao kama wawakilishi wa Waislam wa Tanzania ikawa BAKWATA imekataa msaada wa Aga Khan.
Mkapa akawapa chuo Cha tanesco pale morogoro, hivi kinaendelea?
 
Kwanini ndgu Songambele alikataa msaada?

Raisi si alikua muislam na alilibatiki hilo, sasa Songambele alikua na mamlaka gani ya kumpinga raisi?
Vishu...
Nimeandika mengi kuhusu yaliyokuwa yakimkabili Rais Mwinyi wakati ni Rais wa Tanzania.

Magazeti ya chama chake ambae yeye alikuwa ndiyo Mwenyekiti yalikuwa yanamshambulia bila hofu.

Mwaka wa 1993 Ahmed Saleh Yahya aliyekuwa Mhariri wa Africa Events alikuja Dar es Salaam na aliniuliza kwa nini Rais Mwinyi anashambuliwa kutoka kila kona na mimi nimekuwa kimya?

Akaniomba niandike makala moja ya kumtetea.

Wakati huo Chuo Kikuu kimwemwalika Mtikila na akazungumza Nkrumah Hall na akamkanyaga Rais Mwinyi hali kadhalika Press Club ilimwalika Mtikila na akafanya hivyo hivyo bila hofu yoyote,

Yasikushangaze hayo ya Songambele.

Africa Events ikachapa makala yangu na cover ya toleo hilo ni hiyo hapo chini:

1704226164305.png
 
Kwanini unashindwa kua specific, EAMWS ilivunjwa na serikali au kanisa?

Leo tar 02/01/2024 tufanye nini ili unayoyasema yarekebishike/ yapate kufanyiwa kazi?
Mpaji...
Ntakujibu kwa kukuuliza.
Unadhani nani kati ya hao wawili atanufaika kwa kuwakosesha Waislam elimu?
 
Mpaji...
Ntakujibu kwa kukuuliza.
Unadhani nani kati ya hao wawili atanufaika kwa kuwakosesha Waislam elimu?
Waislamu hawajakoseshwa elimu, waliotaka elimu yenye tija waliitafuta kwa udi na uvumba mfano Mojawapo ni wewe! Wale walioaminishana elimu ya Dunia haina tija bas hawakuitafuta wakaenda madrasa na kuangalia sinema
 
Waislamu hawajakoseshwa elimu, waliotaka elimu yenye tija waliitafuta kwa udi na uvumba mfano Mojawapo ni wewe! Wale walioaminishana elimu ya Dunia haina tija bas hawakuitafuta wakaenda madrasa na kuangalia sinema
Mpaji...
Nimeandika hapa mara nyingi na kutoa ushahidi kuwa Waislam wamezuiwa mara mbili kujenga Chuo Kikuu.

Nimeeleza yaliyokuwa yakifanyika ndani ya Wizara ya Elimu na NECTA.

Madrasa ndiyo taasisi ya kwanza kutoa elimu Pwani ya Afrika ya Mashariki na iko research paper ya Dr. Ishumi Idara ya Elimu Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam.

Tatizo ni kuwa wengi wenu hapa hamjui na hamko tayari kujifunza yale msiyoyajua.
 
Back
Top Bottom